Thursday, January 15, 2009







Leo mchana Jijini New York, rubani wa shirika la ndege la US Airways nambari 1549, kwa ujasiri mkubwa aliweza kuokoa maisha ya watu 150 kwa uamuzi wake wa kulitumbukiza lidege kwenye maji ya Mto Hudson(unaotenganisha New York na New Jerseys) la sivyo lingeishia kwenye majumba ya Manhattan. Hii ilikuwa ni baada ya ingini zote za dege hilo kuleta mushkeli kutokana na inachosemekana kuwa ndege walioingia kwenye ingini hizo. Dege hilo ndio kwanza lilikuwa limeanza safari likitokea LaGuadia, New York kuelekea Charlotte, North Carolina.



No comments:

Post a Comment