HII NI BLOGU YA JAMII INAYOLENGA KATIKA KUONYESHA MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA NA VIELELEZO VYAKE VYA MAISHA YA KILA SIKU YA BINADAMU, IWE NI MIMI, WEWE, SISI, YULE AU WAO, HALI MRADI TUU TUENDELEE KUELIMISHANA NA KUPEANA HABARI SAHIHI ILI TUENDELEZE JAMII YETU.
Sunday, April 19, 2009
Katika hali ambayo haikutegemewa, Mzee Mandela ajitokeza katika mkutano wa kampeni za mwisho mwisho kabda ya uchaguzi wa tarehe 22 mwezi huu, kuonyesha kumuunga mkono kwake mgombea wa ANC bwana Jacob Zuma. Mzee Mandela alitumia nafasi hiyo kuwakumbushia ANC ya kuwa wanajukumu la kuondoa umasikini na kuleta umoja nchini Afrika ya Kusini. Mamilioni ya watu bado wanaishi katika hali ya dhiki kama inavyoonyesha picha ya pili toka chini. Picha ya juu anaonekana Mzee Mandela akisaidiwa kushuka jukwaani na Zuma mara baada ya mkutano huo wa kampeni.
No comments:
Post a Comment