FUNDI WA KOMBO

HII NI BLOGU YA JAMII INAYOLENGA KATIKA KUONYESHA MATUKIO MBALI MBALI KATIKA PICHA NA VIELELEZO VYAKE VYA MAISHA YA KILA SIKU YA BINADAMU, IWE NI MIMI, WEWE, SISI, YULE AU WAO, HALI MRADI TUU TUENDELEE KUELIMISHANA NA KUPEANA HABARI SAHIHI ILI TUENDELEZE JAMII YETU.

Wednesday, August 8, 2012

KANISA KONGO LAMFUNGISHA NDOA MUME NA WAKEZE WATATU, MKANGANYIKO WAIBUKA


Anikulapo Kuti akiwa na wake zake watatu wakati wa ndoa yao.


FELA Anikulapo Kuti, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ametoa mpya kwa walimwengu kwa kufunga ndoa na wanawake watatu.
Mtu huyo ambaye anatumia jina la mwanamuziki aliyevuma zamani wa Nigeria, hayati Fela Anikulapo Kuti, amefunga ndoa hiyo kufuatia mchungaji wa kanisa lake nchini humo kuwaambia waumini wake kwamba wanaweza kuoa wanawake wengi, jambo ambalo limeleta mkanganyiko mkubwa kwa waumini wa madhehebu ya Kikristo barani Afrika.
Ndoa hiyo ilifungwa kama kawaida, ambapo watu hao wanne waliapa kuwa mume na wake zake, wakishuhudiwa na watu kibao huku kiongozi aliyeifungisha ndoa hiyo akinukuu vifungu vya Biblia ambavyo hutumiwa na Wakristo wote.
Tukio hili limeleta mkanganyiko mkubwa na kuwaacha watu wengi wakijiuliza mengi kuhusu madhehebu ya Kikristo yanavyojiingiza katika matendo yasiyoendana na imani yao, ambayo inasisitiza mke au mume kuwa na mwenza mmoja tu.
Chanzo: 
www.informationnigeria.org
Share

No comments:

Post a Comment

‹
›
Home
View web version

KUHUSU SISI

  • Ebra
  • Unknown
Powered by Blogger.