Thursday, August 16, 2012

RUDISHA HABAKIA ULAYA


Rudisha

Bingwa wa Olympiki na dunia kwenye mbio za mita 800, David Rudisha, hakuwa miongoni mwa kikosi cha nchi hiyo kilichotua Kenya asubuhi ya leo kutoka London kwenye michuano iliyomalizika ya Olimpiki.
Rudisha na baadhi ya wanamichezo wameamua kubaki katika Ulaya ili kujianda kwa michuano inayokaribia ya Diamond League itakayoendelea Ijumaa wiki hii jijini Stockholm, Sweden.

Rudisha ambaye alivunja rekodi yake mwenyewe ya dunia aliposhinda kwenye michuano ya Olimpiki kwa kukimbia kwa dakika moja, sekunde 40 nukta 91, ameamua kwenda Ujerumani kushiriki hatua ya pili kutoka mwisho ya michuano ya Diamond League itakayofanyika Agosti 30.

Huenda pia naodha huyo wa timu ya riadha ya Kenya akashiriki mbio za Rieti, nchini Italy, ambapo anaweza kuvunja tena rekodi yake katika moja kati ya mbio hizo.

No comments:

Post a Comment