Hii ni haki kweli jamaa nusra apoteze jicho
Kituko cha mwaka kimetokea leo mchana muda wa saa saba huko Arusha mjini, baada ya Trafiki mmoja (hayupo pichani) kumkamata Dereva wa Bodaboda (pichani aliyeumia) na kumpa maelekezo ya kupeleka Pikipiki hiyo kituo cha polisi! cha ajabu wakiwa njiani Dereva Bodaboda alibadili nia na kutaka kuelekea sehemu tofauti na kituoni! hali hii ilimfanya Polisi kustuka na kuanza kushika usukani na kulazimisha pikipiki ipelekwe kituo cha Polisi, kwa hatua hii Pikipiki hiyo iliendeshwa na watu wawili hadi kituo cha Polisi ilipotokea ajali hii !
No comments:
Post a Comment