MAPENZI MOTOMOTO;KUSHIKWA KWENYE MAPENZI SIYO LIMBWATA AU MAPENZI MOTOMOTO BALI NI MATOKEO YA HOMONI!

Wakati mwingine huwapigia simu wapenzi wao wa nje waziwazi
Tunajiuliza
siku zote ni kwa nini penzi linapoingia mahali huweza kuharibu kila
kitu? Tumekuwa na misemo yetu ya siku nyingi kama siyo ya asili, kama
vile ule wa ‘penzi ni ulevi’ au ‘penzi ni upofu’ na mingine yenye
kuonyesha kwamba penzi lisipoangaliwa kwa makini linaweza kuleta athari
mbaya na kubwa kwa binadamu.
Ni nani
ameshawahi kujiuliza ni kwa nini hali hiyo hutokea? Kuna yeyote ambaye
hata mara moja ameshawahi kujiuliza ni kwa nini penzi halina shujaa au
mnyonge pale linapoingia wote huwa kama waliopagawa? Bila shaka sio
wengi, kama wapo ambao wameshawahi kujiuliza swali hili. Kila mmoja
anadhani ndivyo ilivyo na hakuna awezaye kujua ni kwa nini.
Ukweli ni
kwamba penzi halina tofauti na ulevi sugu kama ule wa pombe au madawa
ya kulevya. Penzi linaelezwa kwamba ni sawa na ubobeaji wa mcheza
kamari. Ile starehe na pumbazo la akili ambalo mtumiaji wa madawa ya
kulevya au mlevi sugu analihisi, ndilo hilo hilo ambalo mtu aliye
katika mapenzi anahisi.
Penzi(Kwa
maana ya mtu kumpenda mwingine wa jinsia tofauti kwa penzi la kawaida
au hadi kwa kufanya mapenzi) na usugu wa madawa au pombe, vyote huwa
vinauchochea mwili wa anayehusika kutoa homoni inayofahamika kama dopamine.
Homoni hii ambayo ni kemikali katika ubongo huwa inaujaza mwili raha
na ni kemikali hii hii ndiyo ambayo inahusika katika kuupa mwili tabia
ya usugu katika mambo fulani kama ulevi.
Ni kitu gani kikubwa katika hili?
Ni kwamba
kama ni hivyo, ina maana kuwa mtu kuwa kwenye kiwango kikubwa au cha
juu cha kupenda, yaani kama tulivyozea kusema ‘kuwa hoi kwa penzi’, ni
sawa na wakati ule mlevi sugu wa madawa akiwa ameshavuta au kunywa.
Mbaya zaidi ni pale penzi linapofikia hatua ya kuwa penzi la kukutana kimwili. Ni mbaya kwa sababu katika hatua hii homoni ya depomine inayotolewa inaweza kuizinga akili milele.
Kinachotokea
ni kwamba kama homoni hiyo itajizinga kwenye akili, mhusika anakuwa
sawa kabisa na mlevi sugu wa pombe au madawa ya kulevya, inakuwa ni
vigumu sana kumtoa mtu kama huyo kwenye penzi na huyo fulani wake.
Bila shaka
umeshawahi kuona au kusikia juu ya watu ambao wanaishi kwenye uhusiano
mgumu sana na wapenzi wao, lakini bado wakawa wagumu wa kuondoka
kwenye uhusiano huo. Kwa mawazo yetu wengi huwa tunadhani kung’ang’ania
huku kunatokana na hali kama utegemezi, hasa kwa wanawake.
Baadhi
yetu huwa tunaamini kwamba hali hiyo inaweza kuwa inasababishwa na dawa
za asili au uchawi maarufu kama Limbwata, hasa pale mwanaume anapokuwa
ameshikwa kwenye mapenzi na mpenzi wake au mkewe. Hii sio kweli.
Kuna
wakati unakuta kwamba mwanamke ana uwezo wa kuendesha maisha yake na
pengine yeye ndiye anayemsaidia mwanaume katika maisha, lakini pamoja na
kuteswa au kuburuzwa na mwanaume huyo, bado atang’ang’ania kuishi
naye. Kuna wakati tunaona kabisa kwamba, mwanaume anajua kwamba
mwanamke anamfurusha kwenye uhusiano wao na anakiri, lakini bado
anang’ang’ania kwenye uhusano huo na mwanamke huyo.
Inaanzaje?
Watu
wawili hupendana. Kama nilivyosema, kupendana huku husababisha homoni
hii kuzalishwa ubongoni. Kuzalishwa kwa kemikali hii ndiko ambako
humfanya mtu aliyependa kuwa katika raha fulani isiyoelezeka. Kama
ilivyo kwa mlevi wa pombe au madawa ya kulevya, kuna wakati kiwango cha
nishai hushuka ambapo inabidi avute au kunywa tena. Kwa mtu aliyependa
naye, kuna wakati hali ya raha hii hushuka, kutegemea mazingira.
Lakini
kama wapendanao wamekutana kimwili na kukutana huko kukawapa raha kubwa
sana, uwezekano wa kemikali hii kuizinga akili moja kwa moja ni mkubwa
sana. Akili inapozingwa na homoni hii, mpendaji kamwe hataacha tena
kumpenda huyo mtu wake.
Inakuwa
kama mlevi sugu anavyotegemea pombe au madawa kupata raha ya maisha,
huyu mpendaji naye atakuwa hajisikii raha bila kuwa na huyo mpenziwe,
bila kujali visa na vibweka anavyomfanyia. Hata kama hashiriki naye
tendo la ndoa, bado atakuwa anajisikia raha tu kuwa naye.
Msomi mmoja
wa chuo kikuu cha Guelph huko Canada, George Bubenik anakiri kuwepo
kwa hali hii na anasema ndio maana unaweza kukuta mtu akiishi kwenye
ndoa ya mashaka na vurugu huku huku wengine wakishangaa na kutoelewa
sababu. “Mtu ambaye anafurahia sana tendo la ndoa mwanzoni mwa uhusiano
na mwenzake anaweza kung’ang’ania kwenye ndoa hata kama imejaa vurugu”
Anasema
watu hawa wangetarajiwa kuondoka au kuzikimbia ndoa za aina hii lakini
huwa hawafanyi hivyo kwa sababu wamepata usugu wa kiakili kwa zile
hisia wanazozipata wakati waliposhiriki tendo la ndoa na wapenzi wao.
Kama mlevi sugu wa pombe asivyoweza kuacha pombe hata kama inakaribia
kumuuwa, ndivyo inavyokuwa kwa watu wa aina hii.
Haina maana
kwamba hao wapenzi wao ni watu wenye kujua sana mapenzi, hapana. Ni
kwamba siku ya kwanza walipokutana , ubongo ulizalisha homoni kwa wingi
na ikawa imeizinga akili. Kinachojirudia hapa ni zile hisia za awali.
Sawa kabisa na mlevi sugu, ambaye anaweza kuwa anakunywa pombe kali na
isiyo na utamu, kwa sababu anachohitaji siyo ladha ya pombe, bali zile
hisia wakati au baada ya kunywa. Hapa mwanamke au mwanaume aliye katika
hilo penzi anaendeshwa na hisia anazozipata wakati wa tendo la ndoa,
ambazo zimeganda akilini kupitia homoni hii ya dopamine.
Huwa
hakuna kulogwa wala limbwata au mapenzi motomoto, hapana., hapa kuna
tatizo la utegemezi. Mhusika ni mtu ambaye inabidi asaidiwe kama
anavyosaidiwa mlevi sugu. Wengi wetu huwalaumu watu hawa au wapenzi wao,
jambo ambalo bila shaka siyo haki.
Tumeshawahi
kusikia bila shaka watu wakisema, ‘wewe hujui ni kwa nini
anang’ang’ania uhusiano ule, anajua mwenyewe anachokipata’. Wengi
wanaposema hivyo wana maana ya kile mtu huyo king’ang’anizi
anachokipata hadi kutokuwa tayari kuvunja uhusiano na mpenzi anayemtesa
au kumdhalilisha. Mara nyingi wana maana ya mapenzi motomoto ya
kitandani. Huu siyo ukweli hata kidogo, kwani unaweza kukuta hata
mapenzi ya kitandani mtu huyo hapati. Anachokipata hapa ni ridhiko
linalotokana na dopamine iliyozinga ubongoni mwake.
Inakuwaje ikibidi uhusiano huo ufe:
Kuna
wakati kwa sababu ya mazingira fulani fulani inabidi uhusiano huu ufe,
hata kama mmoja ni king’ang’anizi vipi. Hilo linapotokea yule
king’ang’anizi hukabiliwa na athari za matokeo kama vile wasiwasi, aina
ya hamu ya mapenzi au kupendwa isiyoweza kuridhishwa, huzuni na hasira.
Hali hizi pia huwa zinapatikana kwa mlevi au mvutaji sugu ambaye
anajaribu kuacha kuvuta au kunywa.
Kuthibitisha
hii Bubenik aliwafanyia utafiti panya wadogo wa porini na kugundua
kwamba wanyama hawa wakizuiwa wasitoe homoni iktwayo oxytocin ( sawa na homoni ya dopamine kwa binadamu) wakati wakipandana huwa hawadumu pamoja. Lakini pale wanapoachiwa watoe hiyo homoni huwa hawaachani hadi kufa.
Tunaweza kusema mtu kushikwa au kunaswa kwenye mapenzi ni suala ambalo hakuna mtu anayeweza kudai
kwamba anaweza kulizuia. Kulizuia kunawezekana kama mtu ataamua
kuachana na tabia ya uzinzi tu, kwani hatafikia mahali ambapo akili
yake itazingwa na homoni hii.
No comments:
Post a Comment