Saturday, March 16, 2013

Nyaya za Transfoma za TANESCO zenye thamani ya Tsh.20 mil zakamatwa Dodoma



Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma David A. Misime-ACP
Na John Banda, Dodoma


POLISI Mkoani Dodoma inawashikilia watu watatu baada ya kuwakuta wakiwa na nyaya za Transfoma za jumla ya 20 milion mali ya Tanesco.


Nyaya hizo aina ya kopa zenye uzito wa kilo 76 na nusu zilikutwa kwa watu hao baada ya msako wa polisi wakishirikiana na Shirika la umeme Tanzania Tanesco


Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema nyaya hizo za matumizi ya Transfoma hutumika kwa kufanyia Winding na nyingine ni kwa ajili ya kuzuia Radi [earthing] na kwamba imebainika ziliibiwa maeneo ya kizota na Ihumwa baada ya transfoma zake kuangushwa.


Misime aliwataja waliokamatwa kuwa ni Abdul Bakari 17 mkazi wa Chang'ombe, Stanel Shayo 26 muuza vyuma chakavu Nkuhungu na Peter Kessy 50 mkazi wa Area E manispaa ya Dodoma.


Aliongeza kuwa jeshi hilo linamsaka Jamal Said Sondo wa Chang'mbe Juu aliyekimbia ya mfanyakazi wake Abdul Bakari kukamatwa


No comments:

Post a Comment