Friday, July 12, 2013

DIVA WA CLOUDS FM AJIPIGA TATOO YA KICHINA KIUNONI...

Katika kile kinachotafsriwa kuwa ni harakati za kulimwagilia maji na marashi penzi lake kwa prezzo, Diva wa clouds fm sasa ameamua kujipiga TATOO YA KICHINA kiunoni ili kumchanganya mwanakaka wa Kenya anayegombaniwa na warembo kibao...

Diva amejikuta katika ugomvi mkubwa na warembo wa Kenya ambao wanadai kunyang'anywa mpenzi wao.Miongoni mwa warembo hao ni Hudahh aliyekuwa mshiriki wa Big Brother mwaka huu akiiwakilisha Kenya...

Kabla ya kujipiga tatoo ya kichina kiunoni, Diva aliwahi kujianika akiwa nusu uchi huku shanga zake zikiwa hadharani.
Uamuzi huo aliufanya ili kulipiza kisasi kwa mke mwenza Huddah ambaye naye alijianika mtupu na kumtaka Diva afanye hivyo pia kama ana mapenzi ya dhati kwa Prezzo

1 comment:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete