Mashushushu wanawake wanne raia wa Rwanda wanaoaminika kutumwa na Rais Paul Kagame wamekamatwa mjini Dodoma. Wamekamatwa wakiwa wameshajenga uhusiano wa karibu na baadhi ya viongozi waandamizi pamoja na wajumbe wa Bunge la Katiba.
Pamoja nao Rwanda inadaiwa kuingiza makachero wengine wengi ili waungane na wakimbizi wa Kitutsi walioingia hapa nchini katika miaka ya 1958/1959 na mwaka 1994. Habari kutoka vyanzo vya uhakika zinasema wapelelezi wengi wamekuwa wakiingia nchini kupitia Karagwe mkoa wa Kagera, ambako kumeanza kuonekana kama sehemu ya Jamhuri ya Rwanda.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ya Tanzania imethibitisha kukamatwa kwa makachero wanawaeke wanne raia wa Rwanda, wakijifanya ni makahaba, lakini baada ya uchunguzi imebainika pasi na shaka kwamba ni makachero toka Rwanda. Ukahaba unatumika kama moja ya nyezo adhimu katiak shughuli za ukachero.
Duru za uchunguzi zimebaini kuwa wanawake hao ni sehemu ya makachero waliotumwa kuichunguza Tanzania, kwa lengo la kulinda maslahi ya Rwanda. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mathias Chikawe, amethibitisha kukamatwa kwa wanawake hao, lakini amekataa kuingia ktika undani wa suala hilo.
Habari ipo kwa kirefu gazeti la Jamhuri.
No comments:
Post a Comment