Sunday, April 13, 2014

TAARIFA KAMILI YA AJALI YA HELKOPTA ILIYOMBEBA MAKAMU WA RAIS NA MAAFISA WENGINE WA SERIKALI

Helikopta waliyokua wakisafiria Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, waziri wa ujenzi John Magufuli, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick imepata ajali asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam. (kwa mujibu wa mashuhuda)
Taarifa zilizotoka muda mfupi baadae zimeeleza kupata majeruhi lakini hakuna yeyote aliepoteza maisha baada ya Helikopta hiyo kuanguka wakati ikianza safari kuwapeleka viongozi hao kutembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko.

Wote walitoka salama na majeraha madogomadogo ambapo pia kwenye taarifa nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea na ziara ya kutazama athari za maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo Pwani.

Ajali hii ya Helikopta imetokea siku moja baada ya ndege ya shirika la ndege la Kenya kubamiza chini na kuharibu upande wa kulia wa bawa kutokana na ukungu mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam wakati ikitua kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila waliojeruhiwa wakati wa kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.

Taarifa kutoka kwa mmoja wa Waliokuwemo kwenye Helikopta hii ya jeshi inasema wakati inapaa kwenye umbali wa kama futi tano hivi kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam, ilizidiwa na upepo ulioirudisha nyuma na kuangukia paa kabla ya kutua chini.
Kilichofanyika ni watu waliokuwemo kutoka nje harakaharaka kisha aliekua akiiendesha kufungua tenki la mafuta na kumwaga mafuta yote alafu baada ya muda mfupi vikosi vya zimamoto vikaanza kuipiga maji helikopta hiyo ili kuepusha mlipuko.

Unaambiwa kama ingekua ni majira ya moto, helikopta hii ambayo ilikua inawapeleka kutazama maafuriko yaliyookana na mvua Dar es salaam ingeweza kuwa kwenye hatari zaidi ya kulipuka.

No comments:

Post a Comment