Saturday, September 17, 2011

OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
 
TAARIFA KWA UMMA

NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.

Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA
WILAYA ZAKE
MKOA ZINAKOTOKA
MAKAO MAKUU
1.
Geita
Geita
Mwanza
Geita
Nyang’hwale(Mpya)
Mwanza
Chato
Kagera
Bukombe
Shinyanga
Mpya/Mbogwe
Shinyanga
2.
Simiyu
Bariadi
Shinyanga
Bariadi
Itilima (Mpya)
Shinyanga
Maswa
Shinyanga
Meatu
Shinyanga
Busega (Mpya)
Mwanza
3.
Njombe
Njombe
Iringa
Njombe
Wanging’ombe(Mpya)
Iringa
Ludewa
Iringa
Makete
Iringa
4.
Katavi
Mpanda
Rukwa
Mpanda
Mlele(Mpya)
Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA
WILAYA MAMA
MKOA
MAKAO MAKUU
1.
Buhigwe
Kasulu
Kigoma
Buhigwe
2.
Busega
Magu
Mwanza
Igalukilo
3.
Butiama
Musoma
Mara
Nyamisisi
4.
Chemba
Kondoa
Dodoma
Chemba
5.
Gairo
Kilosa
Morogoro
Gairo
6.
Ikungi
Singida
Singida
Ikungi
7.
Itilima
Bariadi
Shinyanga
Itilima
8.
Kakonko
Kibondo
Kigoma
Kakonko
9.
Kalambo
Sumbwanga
Rukwa
Kalambo
10.
Kaliua
Urambo
Tabora
Kalua
11.
Kyerwa
Karagwe
Kagera
Rubwera
12.
Mbogwe
Bukombe
Shinyanga
Mbogwe
13.
Mkalama
Iramba
Singida
Nduguti
14.
Mlele
Mpanda
Rukwa
Inyonga
15.
Momba
Mbozi
Mbeya
Ndalambo
16
Nyang’hwale
Geita
Mwanza
Nyang’hwale
17.
Nyasa
Mbinga
Ruvuma
Mbamba Bay
18.
Uvinza
Kigoma
Kigoma
Lugufu
19.
Wanging’ombe
Njombe
Iringa
Waging’ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

Fax- 026-2322116

 Imetolewa na: -

 Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


9 Septemba, 2011

Tuesday, September 13, 2011

TIMU ZA SIMBA NA YANGA ZIMEJIFUNZA NINI KUTOKA KWA AZAM FC!



Logo ya Timu ya Simba Sports Club al-maarufu kama wekundu wa Msimbazi.

Logo ya Timu ya Yanga Africans al-maarufu kama watoto wa Jangwani.

Logo ya Timu ya Azam FC

Napenda niwaulize wadau kama kweli ni haki kwa Timu za Simba na Yanga kuufanya uwanja wa Azam FC kuwa kama uwanja wao wa nyumbani!! La hasha, kwa mimi nitasema si haki, ni kitendo cha aibu sana kwa timu hizi mbili kubwa ambazo kama tunavyoona hapo kwenye Logo zao zinaonyesha ni jinsi gani zilivyo vilabu kongwe hapa nchini lakini havina viwanja vyao vya kuweza kucheza mechi zao za ligi za nyumbani na za kimataifa.

NDEGE YADONDOKA HUKO MBEYA LEO ASUBUHI

Hapa ndio mahali ndege hii ilipoangukia baada ya injini zake kuzima ghafla.
Ni Ndege ambayo ni mali ya kampuni ya Kapunga Rice huko Mbeya.
CHEKA UNENEPE . . .
 
Bill Gates organized an enormous session to recruit a new Chairman for Microsoft
Europe. 5000 candidates assembled in a large room. One candidate was Urio,
Tanzanian living in USA .

Bill Gates thanked all the candidates for coming and asking those who do not
know JAVA programming to leave. 2000 people left the room. Urio says to himself,
'I do not know JAVA but I have nothing to lose if I stay I'll give it a try.

Bill Gates asked the candidates who never had experience of managing more than
100 people to leave. 2000 people left the room. Urio says to himself ' I never
managed anybody by myself but I have nothing to lose if I stay. What can happen
to me?' So he stays.

Then Bill Gates asked candidates who do not have management diplomas to leave.
500 people left the room.Urio says to himself, 'I left school at 15 but what
have I got to lose?' So he stays in the room.

Lastly, Bill Gates asked the candidates who do not speak Russian to leave. 498
people left the room. Urio says to himself, ' I do not speak one word of Russian
but what do I have to lose?' So he stays and
finds himself with one other candidate.

Everyone else has gone. Bill Gates joined them and said 'Apparently you are the
only two candidates who have all the required qualifications & experience I am
looking for and speak Russian, so I'd now like to hear you have a conversation
together in that language.' and Calmly,

Urio turns to the other candidate and says `shimbony shafo bana!'

The other answers 'sicha kabsa mleu mbonyi saa kasi wana wai wecha kabsi nkwi
ukeri si ku si mleu

Urio, "nikunu ma mtoni ngikeri fo ngisengeta eleri mndu chu aicha wachaka nyi fo
ruwa"

The other candidate answers"lasma atumanye wachaka tukeri kila handu"

Bill Gates hired them immediately thinking that they were speaking Russian

DJOKOVIC BEAT NADAL TO WIN US OPEN 2011!!


 
MREMBO WETU DADA NELLY KAMWELU!




Ingawa dada yetu Nelly Kamwelu hakupata taji alilovishwa Miss Angola, lakini HONGERA nyingi sana kwa kutupeperushia bendera yetu na kuitangaza Tanzania. Kwetu wewe ni Miss Unirvese!
HUYU NDIYE MREMBO MPYA WA DUNIA
MISS ANGOLA - LEILA LOPEZ





Miss Angola Leila Lopes, left, is crowned Miss Universe 2011 by Miss Universe 2010 Ximena Navarrete, of Mexico, in Sao Paulo, Brazil, Monday Sept. 12, 2011

Sunday, September 11, 2011

SEPTEMBER 11 2001
SERENA, NADAL NA DJOKOVIC WAINGIA FAINALI ZA US OPEN!


 Serena Williams wa Marekani akiruka kwa kushangilia ushindi baada ya kumtoa Caroline Wozniacki wa Denmark.



Naye Novak Djokovic akijigamba kwamba bado yeye yuko juu baada ya kumfyeka Roger Federer.

Baada ya kumtoa Andy Murray wa Uingereza, Rafael Nadal wa Spain asema yuko tayari kutetea taji lake na Djokovic.
PICHA ZA MAAFA YA AJALI YA MELI ZANZIBAR




ENGINEER WILLIAM FOFO MTAALAM ALIEBOBEA KATIKA UTENGENEZAJI WA COMPUTER.

Engineer William Fofo
Fofo ni mtaalam aliye bobea katika utaalam wa kutengeneza Computer, Printers na pia kufanya Networking yoyote inayohusiana na teknolojia ya mawasiliano iwe Security System, Computer Networking, wireless na Cabling.
Kwa yeyote ambaye atahitaji kumpata anaweza akawasiliana na;
KAPINGAZ TECHNOLOGIES LTD au unaweza kumpigia simu kwa namba:
+255 655 113344
+255 713 254553
Vile vile kama una shida yoyote ya ushahuri wa kitaalam usisite kumpigia kwa namba hizo, atakushauri kulingana na tatizo lako bila gharama yoyote

Friday, September 9, 2011

FFU wa Ngoma Africa Band kuvamia Bremen City,Ujerumani
Ijumaa 16-09-2011

"Mzimu wa Bongo Dansi" unaendelea kufunika kimataifa !
 
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,
wanatarajiwa kutumbuiza katika onyesho kubwa la aina yake "AFRIKA MESSE"
mjini Bremen,nchini Ujerumani siku ya ijumaa 16-09-2011 majira ya alhasiri.
Bendi hiyo yenye tabia za kuwadatisha akili washabiki katika kila kona duniani na
mdundo wake "Bongo Dansi" made in Uswahilini.
 
Ngoma Africa band aka FFU imejikuta inapambanishwa tena uso kwa uso na washabiki wengine katika mji wa Bremen,huko ujerumani Ughaibuni !ambapo maelfu ya washabiki wamekaa mkao wa kula makombora ya mziki kutoka kwa bendi hiyo inayoongozwa na kamanda Ras Makunja,bendi hiyo yenye utajiri wa wanamziki wenye vipaji wakiwemo mwanadada Diva Bedi Beraca aka Princess Bedi Bella,pia yupo yule mcharaza solo  mahili Christian Bakotessa aka Chris-B,aka "Mshenzi wa Gitaa la solo" na wengineo.
 
Ngoma Africa band kwa sasa wanatamba na nyimbo zao "Supu ya Mawe" na
"Bongo Tambarare" zisikilize at www.ngoma-africa.com

Upgrading of Colleges Into Universities Questioned

By Finnigan Wa Simbeye

7 September 2011

GOVERNMENT decision to upgrade the former Ardhi Institute, Mbeya Technical College and other similar colleges into universities has deprived the country of sources of well trained technicians, resulting into acute shortage of the skills in the local market.
According to retired Permanent Secretary, Engineer Nirei Msimbira, the move to change Ardhi Institute that used to train competent professional architects, surveyors and other technicians into a full-fledged university has badly affected the country as graduate engineers are not that competent.
"While serving as Permanent Secretary in the Ministry of Water there was a lot of pressure to transform Ardhi Institute into a university and later I witnessed similar pressure to upgrade the Tanzania School of Journalism into the university when with the Ministry of Information and Broadcasting," noted Engineer Msimbira.
He pointed out that the wind of change targeting to increase the number of universities and graduates later extended to other colleges, which used to train competent technicians who assisted engineers in practical implementation of projects.
He was commenting on a key note address delivered by Professor Awadh Mawenya who described the poor state of professional engineers in the country.
Prof Mawenya, a retired University of Dar es Salaam engineering lecturer, said 53 per cent of the country's engineers are not professionally registered. "I visited one site on the ongoing roads projects and did not find any local graduate engineer," Prof Mawenya, who is also Director of Design Partners of Dar es Salaam, said.
Responding to Eng Msimbira's observations, immediate retired University of Dar es Salaam Vice-Chancellor, Professor Mathew Luhanga said the decision to change Ardhi Institute to university and Tanzania School of Journalism (TSJ) into Institute of Journalism and Mass Communications was meant to address growing needs of the economy now.
"Engineers are problem savers and not makers , Ardhi Institute produces very few technicians to meet the country's needs and that's why we made the decision," argued Prof Luhanga, saying the Ardhi University has since its establishment more than doubled the number of graduates.
He also argued that the decision to transform TSJ into IJMC was meant to accommodate growing media needs to nourish democratic reforms. "We say no research, no right to speak, don't just condemn us without first finding out why we did that," charged Prof Luhanga.
Participants called on the government to revive in-house training of graduate engineers at parastatals such as Tanzania Electric Supply Company, Tanzania Railways Limited, Tanzania Ports Authority and others to groom them into full professional engineers
Evangelist Frank Mwakasisi, Ph.D.

Founder and President

Mighty Outreach International - "Helping Churches Reach More People for Christ"

PO Box 1655

Portage, MI 49081

USA




Phone: (269) 321-9900

HII NDIO HALI HALISI YA SHULE ZETU, TUTAFIKA KWELI!!!

Mwanafunzi akiingia Darasani katika moja ya Shule zetu.
Wanafunzi wakiwa Darasani wakimsikiliza Mwalimu.
Mwalimu akitoa Elimu kwa Wanafunzi wake.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nchini Rwanda.
Hii ndio hali halisi ya shule zetu nyingi vijijini na hata pia zile zilizo pepezoni mwa majiji yetu.
KWELI TUTAFIKAAA!!
Ona mwanafunzi wa Rwanda picha ya Mwisho haangaiki ni jinsi gani atakaa kwenye siti akifika Shule; yeye anachoangalia ni jinsi gani anaweza kuitumia Computer katika kuboresha elimu yake anayoipata Darasani.
Aibu kubwa kwa Taifa letu, Taifa la Rwanda limetoka kwenye Vita vya wenyewe kwa wenyewe lakini kwa leo nchi ya Rwanda inasonga mbele katika sekta ya Elimu.
KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika walitazame hili kwa mtazamo chanya.
"HAYA MAJIMBO ZILIKO SHULE HIZI KUNA WABUNGE KWELI"

JAMANI WAKANDARASI MPENI USHIRIKIANO KIONGOZI HUYU SHUPAVU!

Mh. John P. Maghufuli Waziri wa Ujenzi.
Mh. J. Maghufuli akifunga kongamano la kuadhimisha miaka 50 ya uhuru, kwa kuwaomba wakandarasi wafanye kazi kulingana na tataratibu, maadili na sheria za Ukandarasi.
Watanzania tumpe ushirikiano Mh. J. Maghufuli ili afanye kazi yake kwa ufasaha ili wote tuweze kufaidi na utendaji wake. Napenda kuwaomba Viongozi wa Jiji la Dar es salaam jitahidini kumpa ushirikiano ili wakazi wa Jiji waweze kuepukana na huu msongamano wa magari barabarani.
KAPINGAZ Blog inampongeza sana kwa jitihada zake za kutuletea maendeleo Watanzania.

TANGAZO LA KIFO

Familia ya Rowland Mwakibete wa Chicago, Illinois, USA, na Dar es Salaam, Tanzania, inasikitika kutangaza kifo cha mama yao, Bi Mary J. Mushi, kilichotokea Dar es Salaam, Tanzania Jumatano, September 7, 2011. Marehemu ameacha:
· Watoto wanne; Rowland. Roderick, Robert and Raymond
· Mjukuu mmoja; Brian
Mazishi yatafanyika Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Bi Mary mahali pema, peponi.
Kwa wale wote wanaotaka kutoa rambirambi na mchango tunaomba utumwe kwa:
Rowland Mwakibete
1633 Monroe St, Apt # 1
Evanston, IL 60202.
Mawasiliano ni:
Simu: +1 773 312 2124 (Rowland)


DEATH ANNOUNCEMENT

The family of Mr. Rowland Mwakibete of Chicago, Illinois, USA, and Dar es Salaam, Tanzania regrets to announce the death of Bi Mary J. Mushi, Rowland’s beloved mother. She passed away on Wednesday, September 7, 2011, in Dar es Salaam, Tanzania. She is survived by:
· Four sons; Rowland. Roderick, Robert and Raymond
· One grandchild; Brian
The burial will be in Dar es Salaam, Tanzania. May the Almighty God rest Bi Mary’s soul in eternal peace.
The family is accepting and appreciates contributions. If you would like to send one please address it to,
Rowland Mwakibete
1633 Monroe St Apt # 1
Evanston, IL 60202.
Contacts:
Phone: +1 773 312 2124 (Rowland)

Wednesday, September 7, 2011

WATANZANIA TUTEGEMEE NINI KUTOKA KWA MWANAFUNZI ANAYEMALIZA ELIMU YAKE YA MSINGI KWA KUFANYA MTIHANI WAKE WA MWISHO KATIKA MAZINGIRA HAYA!

Saba wakifanya Mtihani wao wa kumaliza Elimu ya msingi leo.
Wanafunzi wa Darasa la

Watanzania Elimu yetu ipo wapi na inakwenda wapi! hili ni swali ambalo lazima wengi wetu tutakua tunajiuliza.
Hali kama hii kwa wanafunzi kufanya Mtihani wa mwisho wakiwa wamekaa chini itaisha lini! ni jambo la kusikitisha sana hali kama hii inavyoendelea na naona kama inazidi kuota mizizi, wahusika wako wapi; Wizara ya TAMISEMI wapo wapi? Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi wapo wapi?

Hizi Wizara zinataka Mtanzania wa kesho awe na Elimu ipi ambayo inaweza kumkwamua katika haya maisha ya leo na mbeleni ambayo mwenye elimu ndio atakayetambulika

KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika wote ambao wanahusika katika kuboresha Elimu za watoto wetu waliangalie hili katika mtazamo mpana zaidi, sidhani kama tutaweza kuwapata wanasayansi wazuri kwa kuwafanyisha Mitihani katika hali hii.

Karne tulionayo ni ya kumpa Mwanafunzi "ELIMU BORA SIO BORA ELIMU


Kumbukumbu ya Septemba 11





Mdau wa Blogu ya Fundi Wa Kombo Ateta

 Kumbukumbu ya Septemba 11
Septemba 11 imekuwa ni tarehe yenye kumbukumbu nyingi na kubwa baada ya mashambulizi ya kigaidi kutokea. Siku hiyo ilibadilisha hali ya maisha sio tu kwa Marekani bali kwa ulimwengu mzima. Zimesalia siku chache tu kuadhimisha miaka kumi tangu tukio hilo la kigaidi kutokea nchini Marekani na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 3,000.

Katika mjadala huu washiriki walikuwa ni:
1. Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Dar es salaam- Azaveri   Lwaitama


2. Peter Langwisa- mkazi wa Marekani aliyeko New York, alishuhudia shambulio hilo na kusaidia   majeruhi.


3.Sheikh Faruk Machanja- Afisa kutoka Taasisi ya Waislam ya kutetea haki za binadamu.


4. Fundi Ramadhani- pia mkazi wa Marekani New York.
Mjadala huu umeendeshwa na Zawadi Machibya

Tuesday, September 6, 2011

LUGHA GONGANA UWANJA WA NDEGE WA KIGOMA; HICHO NDICHO KISWANGLISH PURE.

Hapo ndio mlango wa kuingia katika uwanja wa Ndege wa Kigoma ukisoma hayo maandishi utajua kinachoendelea ni nini!
Wazungu wenyewe hawana tabu washakielewa kilichoandikwa wana furaha tele wakijiandaa kuingia.
KAPINGAZ Blog inawaomba wahusika wa Uwanja huu warekebishe hayo maneno hapo wanajiaibisha na pia wanauaibisha uwanja huo.

PONGEZI KWA BABA NA MAMA MZIRAY

Mr and Mrs K. Mziray

Hapa Mzee Mziray na Mama wakiwa katika moja ya Sherehe ambazo wanahudhuria katika kuweza kujumuika na jamii mbali mbali.

Pongezi nyingi ziwafikie Baba na Mama kwa kudumisha upendo wenu, na sisi kama watoto tutajitahidi kuiga mfano wenu.

Mungu awape maisha marefu na yenye Baraka

Sunday, September 4, 2011

MWAKILISHI MKAAZI WA UNOPS NDG. OMARY MJENGA AZIDI KUDUMISHA USHIRIKIANO WETU HATA KATIKA NYANJA ZA MICHEZO



Ndugu Omary Mjenga, Mwakilishi Mkaazi wa UNOPS nchini Sierra Leone Picha ya juu akiwa na Mkuu wa Itifaki wa Rais wa Sierra Leone, Ndg. Sulay Manah Mkpukumu, ambaye walifanya kazi pamoja Umoja wa Mataifa New Yorkkatika Balozi za Nchi zao. Hapa wapo uwanjani wakati wa mapumziko katika mechi kati ya timu ya taifa ya SL na Misri, na Picha ya Chini yake baada ya kuanza kipindi cha pili Ndg. Omary Mjenga akifuatilia kwa umakini Mtanange huo.

Huo ndio uwanja ambao mpambano huo ulifanyika kati ya Timu ya Taifa ya Siera Leone na Timu ya Taifa ya Misri, ambapo Timu ya Taifa ya Siera Leone iliibuka Kidedea na ushindi wa Bao 2 kwa 1.

MTANZANIA HALISI AKIWA KATIKA VEKESHENI MOJA YA KUUENDELEZA UJASIRIAMALI


Mkurugenzi wa KAPINGAZ PUB, KAPINGAZ TECHNOLOGIES LTD na Mwakilishi Mkaazi wa KAPINGAZ BLOG Ndg. Henry Kapinga akiwa ndani ya viunga vya Sea Cliff Hotel akitafakari jambo baada ya kumaliza kusign Mikataba ya Ujasiriamali

Saturday, September 3, 2011

MTANZANIA ANAYE IPEPERUSHA VEMA PENDERA YA TANZANIA KATIKA ANGA ZA KIMATAIFA

Omary Mjenga wa kati kati.
Hapa akiwa katika moja ya mikutano ya kimataifa akiiwakilisha Tanzania pamoja na Viongozi wenzake kutoka UN.

Hapa akimnong'oneza jambo Msaidizi wa Rais Mstaafu Mh. Benjamin W. Mkapa.

Hapa akipewa Nishani ya Utumishi uliotukuka na Mkuu wake wa kazi UN baada ya kupangiwa kwenda kufanya kazi za UN Nchini Siera leone.

Hapa Ndg. Omary Mjenga akiwa na Mh. Anna Makinda, walipomkaribisha Siera Leone.
Kwa sasa Ndg. Omary Mjenga ni Mwakilishi Mkaazi wa UNOPS Nchini Siera Leone.