Tuesday, June 5, 2012

MKURUGENZI ATCL AFUKUZWA KAZI DAR ES SALAAM, Tanzania WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametengua nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi kutokana na uteuzi wake kuwa kinyume na sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma . Aidha Waziri Mwakyembe pia amewasimamisha kazi maofisa wanne wa Kampuni hiyo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL. Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Omary Chambo, kutenguliwa kwa nafasi hiyo kuanzia Juni tano. “Chizi Paul aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege (ATCL) Agosti 6 mwaka 2011, hata hivyo utaratibu wa uteuzi wake haukufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma”ilisema taarifa hiyo.


MKURUGENZI ATCL AFUKUZWA KAZI


DAR ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametengua nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi kutokana na uteuzi wake kuwa kinyume na sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma .
 Aidha Waziri Mwakyembe pia amewasimamisha kazi maofisa wanne wa Kampuni hiyo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL.
 Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Omary Chambo, kutenguliwa kwa nafasi hiyo kuanzia  Juni tano.
“Chizi Paul aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege (ATCL) Agosti  6 mwaka 2011, hata hivyo utaratibu wa uteuzi wake haukufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma”ilisema taarifa hiyo.

GRADUATION PARTY YA KUWA PONGEZA JOYCE, FETTY, NA GASTON ILIVYOFANYIKA ROOSEVELT ISLAND NY


 Hapa Joyce  Kati alie kula dondo ya Bachelor Of Business Administration In International Business And Bachelor Of Arts In Economics akiwa na marafiki zake Chris kulia kwake na Lily kushoto kwake wakipata ukodak kama kumbu kumbu katika party hiyo.
 Gaston nae aliegraduate na kujibebesha nondo ya Bachelor Of Business Administration in Computer Information System. Akipata picha ya kumbu kumbu na rafikia yake katika party hiyo.
 Fetty na smile ya haja mwana kwetu wewee kwa raha zako....
 Joyce na Chris kushoto kwa Joyce ni Monica aka Lulu Ukodak Moment....
 Mama na watoto wakiwa na marafiki Ukodak Moment kama kawaida
 Maafisa wa Ubalozi Wa Tanzania  Hapa New York Wakipata Picha Ya Pamoja
Maafisa Wa Ubalozi Wa Tanzania Hapa NYC Wakiwa na Nyuso Na Smile Changamfu Kabisa Kuashiria Akuna Matata ......


Historia inaonyesha kwamba wanamuziki wengi hupitia vikwazo vingi mpaka kufikia mafanikio. Ni hali halisi ambayo bila shaka inaeleweka ukizingatia utitiri wa vijana wenye vipaji vya kuimba na hata kutunga au kuandika nyimbo. Wapo wengi.Katika sanaa ya muziki kuna kukataliwa, kuna kuambiwa huwezi, hujui kitu na huwezi kufika mbali.
Pamoja na ukweli huo, kuamua kuendelea au kukubaliana na “maoni” ya wadau na kuachana na muziki, kunategemea mambo kadhaa ikiwemo imani binafsi kama unaweza au huwezi. Ukiambiwa huwezi na wewe ukakubaliana na hoja hiyo,bila shaka utakuwa umefikia mwisho wa ndoto.Unaamka.
Lameck Ditto ni miongoni mwa wanamuziki ambao wamepitia vikwazo vingi mpaka kufikia hapo alipo hivi leo. Bila shaka tunakubaliana kwamba Ditto ni miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya wenye vipaji, nidhamu na juhudi za hali ya juu katika sanaa ya muziki.
Kufikia hapo alipo, alipitia mengi. Alistahimili mengi. Aliwahi kuambiwa hawezi. Aliwahi kutembea kwa mguu masafa marefu ili kwenda studio kwa sababu mfukoni hakuwa na nauli hata ya daladala. Kukaja masuala binafsi ya kufiwa na Mama yake mzazi akiwa bado kijana mdogo tu. Kwa muda mrefu hakumjua baba yake. Akaishi kwa kubahatisha kama vile mtoto wa mtaani. Pamoja na yote hayo,akaendelea kuamini kwamba anaweza na sanaa ndio itakayomtoa. Kama alivyoimba katika wimbo wake “Tushukuru Kwa Yote”, Ditto akaendelea kushukuru na sasa anaanza kuonja mafanikio ya uvumilivu;
Nini kinamfanya kamwe asikate tamaa? Baada ya kufikia mafanikio ambayo anayo hivi sasa,ana mipango gani? Ilikuwaje akaamua kwamba sanaa ya muziki ndio uwanja wake wa kujidai? Fuatana nami katika mahojiano yangu na Lameck Ditto, akielezea kule alikotoka,alipo na anapotaraji kufika na mengine mengi;

BC: Hello Ditto,karibu sana ndani ya BC.Tunafurahi kuwa nawe hivi leo.Labda kwa haraka na kwa faida ya msomaji ambaye hakufahamu, unajielezeaje? Ditto ni nani.Ni mtu wa aina gani?

LD: Asante sana Jeff.Nami nafurahi sana kuwa nawe ndani ya BC. By the way unafanya kazi nzuri sana.
Kwa kifupi tu Ditto ni mwimbaji na mwandishi wa nyimbo. Ni kijana ambaye anajitahidi kujituma katika shughuli zake yeye binafsi na pia kutoa msaada katika shughuli za wenzake kila anapohitajika na kila inapowezekana. Ni kijana mwenye imani katika kufanikiwa bila kujali chochote kinachohusiana na ugumu wa kufanikisha jambo.Ni mpole,mcheshi,msikivu na anayependa kujiendeleza.Huyo ndio Ditto.

BC: Mara nyingi wasanii huanza kupenda aina fulani ya muziki kutokana na waimbaji au wanamuziki walioanza kuwasikiliza tangu wakiwa watoto.Kwa upande wako unakumbuka ulipenda kusikiliza miziki ya kina nani au bendi gani? Unadhani miziki hiyo ilichangia katika uamuzi wako wa kufanya aina ya muziki unaofanya hivi leo?


LD: Kama kijana mwingine yeyote, nilipenda kusikiliza muziki. Na hata nisingependa wakati nazaliwa televisheni zilikuwa bado sio maarufu kwa hiyo nyumbani ukiingia utakachosikia ni redio na mara nyingi redio na muziki na mtu na nduguye. Kwa hiyo niliwasikiliza wanamuziki wengi.
Lakini ambao naweza kusema walinivutia zaidi ni wanamuziki kama vile Hayati Marijani Rajabu kwa upande wa wanamuziki wa kizazi cha awali na watu kama Banana Zorro,Lady jaydee Na Prof J kwa upande wa wale wa kizazi kipya..

BC: Katika tovuti yako,historia inaonyesha kwamba wewe ni pacha.Pacha wako(Kulwa kama sikosei) naye anafanya muziki? Una ndugu mwingine yeyote anayefuata nyayo zako katika muziki?

LD: Ni kweli mimi ni Dotto na nina mwenzangu ambaye ni Kulwa kama ulivyobainisha. Kwa bahati nzuri au mbaya, Kulwa yeye hana mapenzi makubwa na kuimba japokuwa ana kipaji kikubwa sana. Huwa nikimsikia anapoimba baadhi ya mashairi ya nyimbo zangu, kwa mfano, huwa najiona mimi nasubiri kabisa kwake. Hakuna ndugu yangu mwingine anayeimba.Kama yupo basi hatufahamiani.Unajua tena dunia uwanja mpana sana huu.


BC: Mbali na muziki, umewahi kufanya kazi nyingine yeyote kwa minajili ya kujipatia kipato au riziki?

LD: Hapo kabla nilijaribu kuwa fundi makenika. Muziki ukanitoa huko. Pia nimewahi kujishughulisha na biashara ndogo ndogo kitu ambacho nimekiendeleza mpaka leo.Na hivi karibuni kuna kampuni yangu binafsi itaanza kazi…itafanya nini? Vumilieni kidogo.Wote mtajua.

BC: Kwa muda mrefu ulikua bila kuwa na mahusiano na baba yako mzazi. Historia yako inaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza mlikutana katika msiba wa Mama yako(Mwenyezi Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani). Mahusiano yako na baba yako yakoje hivi sasa? Maisha yalikuwaje kukua katika malezi ya mzazi mmoja? Na una ushauri gani kwa wengine ambao, kwa sababu moja au nyingine,hawapo karibu na wazazi wao?

LD: Ni kweli kabisa Jeff kwamba mara ya kwanza kuonana na baba yangu mzazi ilikuwa katika msiba wa mama. Baada ya hapo tumeendelea kuwa na mahusiano ya baba na mwana.
Malezi ya Baba na Mama ni jambo la msingi sana kwa mtoto. Kukua katika mkono wa mzazi mmoja kuna changamoto kubwa sana hususani katika kujenga msingi wa maisha ya mtoto. Lakini namshukuru sana Mama yangu alijitahidi sana. Amenifanya naishi katika msingi alionitengenezea. Kwangu mimi, yeye ni shujaa. Kila siku najisikia imara nikimkumbuka.
Ushauri kwa vijana wenzangu, tuwalee watoto wetu ili tujenge kizazi imara.

BC: Ipo imani kwamba ili msanii atambulike ipasavyo na apate mafanikio,basi mahali pazuri ni Dar-es-salaam. Wewe ni mfano wa wasanii ambao kwanza mlikuwa mkoani(Morogoro) na kisha mkahamia Dar na kama tunavyokuona,una mafanikio mazuri.Unazungumziaje suala au imani hiyo?Ni kweli?Kwanini?

LD: Imani hiyo ipo na inaweza kuwa na ukweli. Kwa mfano, ni ukweli kwamba studio nyingi zipo Dar-es-salaam.Vituo vingi vya radio vinavyotamba nchini vipo Dar-es-salaam. Vituo vya televisheni pia na hata wadau wa muziki kwa ujumla. Lakini hiyo sio kusema kwamba hakuna vipaji ambavyo vinaweza vikapikwa mikoani na kutamba. Mifano ipo ya wasanii ambao wanafanya vizuri mikoani japo nao kwa njia moja au nyingine hufikia mahali ikabidi wajihusishe na Dar-es-salaam!

BC: Mbali ya kuimba,wewe pia ni mtunzi na mwandishi mzuri wa nyimbo.Umeshaandika nyimbo kama Darubini Kali uliyoshiriki ukiwa na Afande Sele na nyimbo kama Kariakoo ya Mataluma. Niambie kidogo kuhusu mlolongo wako mzima wa kuandika wimbo.Nini huwa kinaanza na kipi kinafuata mpaka wimbo unapokamilika?

LD: Asante kwa sifa hizo. Lakini wimbo Darubini sikuandika mimi japokuwa nimeishiriki kwa kiasi kikubwa. Katika utunzi kinachoanza ni wazo la wimbo. Kisha kinafuata mtindo wa kuandika kutegemea na aina ya muziki wa huyo unayetaka kumuandikia. Kisha baada ya hapo mabadiliko hutokea au huenda sambamba na jinsi matayarisho yanavyoanza mpaka kufikia mwisho..

BC: Wimbo wako wa Tushukuru Kwa Yote, ulipamba moto wakati Tanzania ilikuwa inasheherekea miaka 50 ya Uhuru. Kukawa na maneno na mitizamo tofauti.Wengine wakasema tushukuru kwa kipi? Wengine wakasema tushukuru kwa amani na vitu kama hivyo.Ulivyokuwa unauandika nini hasa kilikuwa kichwani kwako?Unajisikiaje kuona kwamba kile ulichokiandika kinaleta gumzo la hapa na pale?

LD: ah aha aha kama msanii, kitu kama hicho kinapotokea huwa naona ni nimefanya kazi yangu vizuri maana yake nimetimiza wajibu wangu.Mimi niliutunga kichwani nilikuwa napata picha ya kitu au watu ambao wanatakiwa kuwa pamoja bila kujali magumu wanayopitia.Sikuutunga kwa ajili ya sherehe za uhuru .Isipokuwa kwa sababu ulitoka kipindi kile watu wakaona waaunganishe na uhuru. Bahati nzuri ni kwamba hadi sasa umekuwa kila linapotokea tukio ni Tushukuru kwa Yote.

BC: Mambo mengi sana yamesemwa kuhusu T.H.T. Mengine mazuri na mengine mabaya.Bila shaka umeshasikia.Tukichagua kuongelea yale mazuri, unadhani T.H.T imekusaidiaje wewe binafsi kama msanii.Ni mambo gani ambayo unadhani usingepata nafasi ya kuwepo pale T.H.T pengine usingejifunza au usingekaa ukayajua?Kivipi?

LD: Ni kweli kwamba mengi huwa yanasemwa kuhusu T.H.T…sasa bila kuingia katika hayo malumbano, ninachoweza kufanya hapa ni kukueleza yale ambayo, kama ulivyoshauri katika swali lako, nimefaidika nayo tangu niende T.H.T. Leo hii mimi kama msanii naweza kusimama popote ndani na nje na nikaimba na watu wakanielewa. Naongelea kuimba katika Live Band.Nimekaa katika misingi ya uimbaji. Nimeweza kuutambulisha muziki wangu tofauti na hata mimi nilivyotarajia. Leo hii nikiimba jukwaani naimba na watu neno hadi neno.Maisha pia yanaenda.Isitoshe nafurahia maisha yangu hapa na ninaamini kila nilichokuwa naota kinaenda kutimia.

BC: Kwa mtu yeyote ambaye amepata nafasi ya kujua mawili matatu kuhusu historia yako, nina uhakika atatambua kwamba umepitia mambo mengi magumu na ingekuwa rahisi sana kukata tama. Ni kitu gani,kile cha ndani hasa,ambacho kimekuwezesha kuendelea na kutokata tamaa?

LD: Brother Jeff, mimi naamini kabisa moyoni na mwilini kwangu kwamba nimeumbwa na neno la kutoshindwa.

BC: Umeanza kuimba ukiwa na umri mdogo tu.Mbali na kuimba pia wewe ni mpenzi mkubwa wa mpira wa miguu(soka) na umewahi kusema kwamba usingekuwa mwimbaji ungependa kuwa mwanasoka ingawa unakiri kwamba kiwango chako katika soka ni kidogo sana.Unazipenda timu gani za soka hapa nchini na duniani kote? Na mbali ya muziki na soka(naamini at least unapenda kuangalia), unapendelea kufanya mambo gani mengine unapokuwa na muda?

LD: Kwa upande wa hapa nyumbani mimi Ni Shabiki Wa Simba na katika soka la kimataifa mimi ni shabiki wa Manchester United. Ninapopata muda wa ziada napenda kupumzika na marafiki nyumbani kwangu na kubadilishana mawazo.

BC: Kama ningekupa offer ya chakula cha jioni,ungependelea kula chakula gani? Na wakati wa chakula hicho ingewezekana ungependa kuwaalika watu gani watatu(hai au waliofariki)
LD: January Makamba,Zitto Kabwe Na Marehemu Amina Chifupa.


BC: Naamini kabisa kwamba unapenda sana kusikiliza muziki au nyimbo za watu wengine.Katika kusikiliza kwako,ni nyimbo gani au zipi ambazo huwa unatamani kwamba ungekuwa wewe ndio mwandishi wake?

LD: My Hope is In You ya Youssou Nd’our, Chuki Ya Wayre, Machoni Kama Watu ya AY na Nyimbo karibia zote za Lokua Kanza.

BC: Nini malengo yako katika miaka 5 ijayo? Na una ujumbe gani kwa mashabiki wako? Wajiandae na nini kipya kutoka kwako mwaka huu?

LD: Mashabiki wangu waendelee kutegemea muziki mzuri kutoka kwangu.Malengo yangu baada ya miaka mitano ni kuwa na nguvu kubwa kimuziki wa Africa na dunia nzima.

BC: Asante sana kwa muda wako Ditto. Shukrani

LD: Asante na wewe endelea kutangaza wanamuziki wa Tanzania na East africa Yetu.

Kwa habari zaidi kumhusu Lameck Ditto unaweza kutembelea tovuti yake kupitia www.lameckditto.com na pia unaweza kumfuata kupitia mtandao wa Twitter @Lameckditto


Read more: LAMECK DITTO: ALIPOTOKA,ALIPO NA ANAPOOTA KUFIKA(INTERVIEW) - BongoCelebrity

SHUKRANI KUTOKA KWA MCHUNGAJI JOHN KUPAZA WA KANISA LA BAPTIST TANGA.

Marehemu Mama Mchungaji John Kupaza
Familia ya Mchungaji John Kupaza wa Kanisa la Baptist Kisosora Tanga anapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wale wote waliojaribu kuokoa maisha ya Mke wake Mpendwa Marehemu Mama Mchungaji Kupaza na wale walioshiriki kwa dhati katika shughuli za mazishi.
Mchungaji J. Kupaza anapenda shukrani zake za dhati ziwafikie Baptist Convention of Tanzania, Mwenyekiti wa Jumuiya Kuu ya Wanawake wa Baptist Tanzania, Dr. Lugano Mtafya, Umoja wa Makanisa ya Baptist Dar es salaam, Baptist Kanda ya Kaskazini, Umoja wa Makanisa Tanga, Manesi na Wauguzi wa Hospitali ya Muhimbili, Hospitali ya Cancer ya Ocean Road, Hospitali ya Bombo Tanga, Madaktari na wauguzi wa Magomeni Baptist Center, Majirani wote wa Mchungaji Kupaza na watoto wa Marehemu Sarah, Samwel, Rosemary, Dr. Lawi, Potinna, David na Tumaini wote kwa pamoja wanawashukuru wote mlioshirikiana nao katika kipindi hiki kigumu. Mungu awabariki wote.
Marehemu Mama Mchungaji Kupaza alifariki Tar. 18/05/2012 Jijini Dar es slaam na kuzikwa Tarehe 21/05/2012 Jijini Tanga katika makaburi ya Bombo.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE
AMEN.

Monday, June 4, 2012


Kuanzia leo, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake.Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.
The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi,Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).
Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu;

BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?

MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?

BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?

MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa

BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?

MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali.Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.

BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?

MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa

BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?

MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa.

Stage ya The Mboni Show
BC: Katika pitapita yangu ya mitandaoni nimesoma mahali kwamba Oprah ni miongoni mwa wanawake wanaokuvutia sana na yeye ni sababu mojawapo ya w ewe kuanzisha The Mboni Show ikiwa kama hatua mojawapo ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya. Kuna ukweli wowote katika hilo?

MM: Ni ukweli kabisa kwamba Oprah Winfrey ananivutia kupita kiasi. Pamoja na hayo show yangu haitokuwa ki-Oprah moja kwa moja. Sitaki na wala siwezi kumuiga kwa kila kitu. Ntakachofanya mimi ni kuchukua yale ambayo naweza kuyachukua na hususani kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania zaidi. The Mboni Show ni show ya kitanzania kwa ajili ya watanzania.

BC: Katika maelezo ya awali ya The Mboni Show umeeleza kwamba malengo ya show yako ni kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya watanzania. Mmejipanga vipi kufikia malengo hayo?

MM: Yaani Jeff you will be Suprised .Wewe subiri tu utajionea.Lakini ki-ukweli The Mboni Show imejipanga vilivyo. Nawaambia The Mboni Show ndio kimbilio la Watanzania na mwokozi wao ha ha ha ha

BC: Mlolongo wa kuanzisha TV show ni mrefu na bila shaka umepambana na vikwazo kadhaa mpaka kufikia hatua hii. Unaweza kunieleza kidogo kuhusu vikwazo ulivyopitia na kitu gani kilikuwa kinakupa msukumo kwamba endelea tu usikate tamaa?

MM: Jeff sio kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Mimi na timu yangu tumeanza production since April last year na imagine ndio kwanza tumemaliza juzi juzi.Ni wazi kwamba katika kutimiza lengo au azma hii nimepitia vikwazo vingi ambavyo kwa kweli nisingesimama imara ningeweza kabisa kukata tamaa. Lakini mwisho ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia mpaka kufika hapa.
Kwa upande wa kitu ambacho kilikuwa kinanipa msukumo naweza kusema ni asili yangu ya kuwa mvumilivu na mbishi sana ninapotaka la kwangu.Hizo ndizo silaha zangu; uvumilivu na ubishi wenye manufaa. Vikwazo vilikuwa vingi sana ingawa sitopenda kuvitaja.Kwa ufupi nawaambia sio kitu kirahisi hata kidogo, ni kukomaaa tu mpaka kieleweke.

BC: Tunaposikia mtu anaanzisha kipindi cha televisheni kuna maswali kadhaa yanakuja. Je kitakuwa ni kipindi cha kurekodiwa ndani ya studio maalumu au kitakuwa kipindi cha kurekodiwa nje ya studio kwa maana ya mtaani nk. Kwa upande wenu format ya production ya The Mboni Show imekaaje?

MM: Kwa upande wetu tuna sehemu maalum ya kurekodia kama hii session ya kwanza vipindi vyote tulirekodia pale Serena( zamani ilikuwa ikiitwa Movenpick). Nawashukuru sana Serena kwa mchango wao katika kufanikisha hili. Next session itakuwa the same japo huwa tunatoka kidogo na kurekodi nje. Kuna mtu ambaye tumerekodi naye nje na hivi karibuni tunapanga kuingia mtaani. The Mboni Show ni kwa ajili yenu watanzania. Popote tutawafuata.

BC: Upo ukweli kwamba Hosts wengi wa TV show huwa yawabidi wawe na tabia ya kujisomea sana ili kupata mawazo na mitazamo mipya kila mara na kwenda na wakati. Je, na wewe pia una hulka hiyo au umejipanga namna gani katika kuhakikisha kwamba sio tu unakwenda na wakati bali unapata ideas mpya mpya za show nk?

MM: Kama nilivyogusia hapo mwanzo, siri yangu kubwa ni kuangalia kwa makini show za wengine zinafanywaje. Namuangalia mtu kama Oprah,Tyra,Monique,Hellen etc ili kupata mtazamo tofauti na ili niweze kuboresha show yangu kila mara. Sidhani kama ni lazima sana kusoma sana vitabu kwa sababu inategemea na aina ya show uliyonayo au unayoifanya.

BC: Mbali na hii venture mpya ya kuwa Host wa TV show, wewe ni mjasiriamali. Siku hizi, kama tunavyoona, wanawake wengi zaidi nao wanaingia kwenye ujasiriamali. Una ushauri gani kwa wanawake wenzio kuhusiana na ujasiriamali?

MM: Kwanza lazima ujue hiki kitu ” Fanya kitu ambacho unakipenda na unakiweza. Wanawake wengi tunakurupuka kwenye ujasiriamali na wakati hatuuwezi. Watu wanafanya kama fashion. Let’s say mimi napenda kuwa na Boutique kwa sababu napenda fashion na ninaimudu.Haya sasa nina talk show kwa sababu naipenda na ninaimudu. Kwa hiyo wanawake wenzangu, tujaribu kufanya kitu ambacho tunakipenda na kukimudu. Ni rahisi zaidi kufanikiwa ukiwa na hayo mambo mawili. Mapenzi kwa kitu unachokifanya au kutaka kukifanya na uwezo wa kukifanya.

BC: Mwisho una ujumbe gani mahususi kwa watanzania? Na pia kwanini mtu achague kuangalia The Mboni Show badala ya show zingine lukuki kwenye luninga?

MM: Ujumbe kwa watanzania wenzangu “Tupende vya kwetu, tuthamini vya kwetu, Tupendane na tushirikane. Kama unaona una connection na wewe huna uwezo nao ila kuna mwingine anaweza basi msaidie na sio kubaniana na kuoneana vijiba vya roho bila sababu za msingi.. Na pia tupende kusifiana. Mwenzako kafanya kizur basi mpe hongera zake na kama kakosea basi muelekeze( muongoze).
Ha ha ha ha Trust me The Mboni show iko kitofaut kabisa na zile tulizozizoea. Kwenye The Mboni show unapata kila kitu.Full package ha ha ha ha.


Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya The Mboni Show katika www.thembonishow.com.




Read more: UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA - BongoCelebrity

RAIS KIKWETE AKUNATA NA WABUNGE WA TANZANIKATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI MJINI ARUSHA

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao leo Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha. Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kesho ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.

UNYANYASAJI WAMPELEKA GEREZANI MKALI WA 'MAWE' BONDIA MAYWETHER


Mayweather, akisindikizwa na Mwanasheria wake, Karen Winckler  (katikati) na rafiki yake 50 Cent , wakati akiingia katika Mahakama ya Las Vegas kusomewa hukumu ya kesi yake.
 Mayweather akifungwa pingu tayari kuelekea katika gereza la  Clark County, Detention Center Nevada.
 Sare na Yeboyebo atakazotumia Mayweather kipindi atakachokuwa gerezani

OLIVIA CULPO NDIYE MISS USA 2012.



Suddenly band camp got a lot more glamorous! A 20-year-old Cranston, Rhode Island native – who talked about her love of the cello and spending her summers at band camp – was the winner of Sunday's 61st Annual Miss USA Pageant.


Olivia Culpo, a student at Boston College where she's a regular on the Dean's List, beat out 50 other hopefuls in the beauty contest, during which she worked the stage at the Planet Hollywood Resort & Casino in Las Vegas wearing a pink bikini and purple Grecian style evening gown. The brunette talked about the influence music has had in her life – she played the cello for 13 years, noting, "Band camp was my summer every summer." Other information given out about her during the pageant? She was "short and chubby" growing until she hit a growth spurt. She is also passionate about "quoting celebrities" and shared her favorite saying by Audrey Hepburn.

ILIVYOKUWA SHOW YA SUGU, VINEGA, JUMA NATURE, PROF JAY JANA DAR LIVE

ILIVYOKUWA SHOW YA SUGU, VINEGA, JUMA NATURE, PROF JAY JANA DAR LIVE


Sugu akiwarusha mashabiki waliofurika ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.


Sugu na Mkoloni wakizidi kuwadatisha mashabiki.

Profesa Jay akiwapa burudani mashabiki wa Dar Live.

Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari nae akitoa 'verse' kuupamba usiku wa Sugu ndani ya Dar Live.

Kundi la Naukala Ndima likifanya vitu vyake stejini.

Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan akiwasalimia mashabiki wa Dar Live.


Baadhi ya mashabiki wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Sugu.


Juma Nature na kundi lake la Wanaume Halisi likifanya makamuzi stejini.

Mapacha kutoka kundi la Vinega wakiiteka steji ya Dar Live.
Suma G nae alikuwepo kuupamba usiku huo.

MBUNGE WA BAHI OMARY BADWEL, AFIKISHWA KIZIMBANI LEO KWA KESI YA KUDAI RUSHWA Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili. Mbunge huyo alikamatwa jana kwa kile kilichodaiwa kudai na kutaka kupokea Rushwa baada ya kukamilika kwa mitego ya Wana TAKUKURU katika Hoteli ya Peacock iliyopo maeneo ya Mnazi Mmoja jana. Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wakati akitoka Mahakamani huku baada ya kusomewa mashitaka mawili ya rushwa ya sh. milioni 1, aliyokuwa akiitaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana. Wakili wa Mbunge wa Bahi, Omary Ahmed Badwel, Mpare Mpoki (kushoto) akitoka Mahakamani. Na Mwandishi Wetu, Jijini MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel (43) leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kosa la rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana. Wakili wa Takukuru, Janeth Machullia na Ben Lincoln, walidai mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba, kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa. Wakili Machullia, alidai kuwa kosa la kwanza ni la rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam , Badwel, akiwa ni Mbunge wa Bahi na Mjumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na wakati huo akiwa ni ofisa wa serikali kwa maana ya sheria ya Takukuru, alitenda kosa la kushawishi ili apewe rushwa ya jumla ya Shilingi milioni nane kutoka kwa, Sipora Liana, ili kiasi hicho cha fedha aweze kuwapelekea wajumbe wenzake wa Kamati hiyo ya Bunge ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya mwaka 2011/2012 ya Halmashauri hiyo. Wakili Machullia, alidai shitaka la pili ni kwamba kati ya Juni 2 mwaka huu, katika Hoteli ya Peacock, mshitakiwa akiwa na nyadhifa zake zote hizo alipokea rushwa ya Milioni moja kutoka kwa Liana ili aweze kwenda kuwashawishi wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya Halmashauri ya Mkuranga huku akijua kufanya hivyo ni kosa. Hata hivyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki, alikanusha mashitaka yote na wakili wa Machullia, alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika. Kwa upande wake Hakimu Mkazi Kahamba, alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni nne na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani, sharti ambalo lilitimizwa na mshitakiwa huyo na akapata dhamana. Hakimu Kahamba, ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo.




Monday, June 4, 2012


MBUNGE WA BAHI OMARY BADWEL, AFIKISHWA KIZIMBANI LEO KWA KESI YA KUDAI RUSHWA

 Mbunge wa  Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kusikiliza kesi inayomkabili. Mbunge huyo alikamatwa jana kwa kile kilichodaiwa kudai na kutaka kupokea Rushwa baada ya kukamilika kwa mitego ya Wana TAKUKURU katika Hoteli ya Peacock iliyopo maeneo ya Mnazi Mmoja jana


 


 Mbunge wa Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel, akiwa chini ya ulinzi wa Polisi wakati akitoka Mahakamani huku baada ya kusomewa mashitaka mawili ya rushwa ya sh. milioni 1, aliyokuwa akiitaka kutoka kwa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana.

Wakili wa Mbunge wa Bahi, Omary Ahmed Badwel, Mpare Mpoki (kushoto) akitoka Mahakamani.


Na Mwandishi Wetu, Jijini
MBUNGE wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Ahmed Badwel (43) leo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa kosa la rushwa ya shilingi Milioni moja toka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Jonathan Liana.
Wakili wa Takukuru, Janeth Machullia na Ben Lincoln, walidai mbele ya Hakimu Mkazi Faisal Kahamba, kuwa mshtakiwa huyo anakabiliwa na makosa mawili ya rushwa. 
Wakili Machullia, alidai kuwa kosa la kwanza ni la rushwa kinyume na kifungu cha 15(1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007, kuwa kati ya Mei 30 na Juni 2 mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam , Badwel, akiwa ni Mbunge wa Bahi na Mjumbe Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na wakati huo akiwa ni ofisa wa serikali kwa maana ya sheria ya Takukuru, alitenda kosa la kushawishi ili apewe rushwa ya jumla ya Shilingi milioni nane kutoka kwa, Sipora Liana, ili kiasi hicho cha fedha aweze kuwapelekea wajumbe wenzake wa Kamati hiyo ya Bunge ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya mwaka 2011/2012 ya Halmashauri hiyo.
 Wakili Machullia, alidai shitaka la pili ni kwamba kati ya Juni 2 mwaka huu, katika Hoteli ya Peacock, mshitakiwa akiwa na nyadhifa zake zote hizo alipokea rushwa ya Milioni moja kutoka kwa Liana ili aweze kwenda kuwashawishi wajumbe wa Kamati hiyo ili waweze kuipitisha ripoti ya fedha ya Halmashauri ya Mkuranga huku akijua kufanya hivyo ni kosa.
 Hata hivyo mshitakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea Mpare Mpoki, alikanusha mashitaka yote na wakili wa Machullia, alidai kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Kahamba, alisema ili mshitakiwa apate dhamana ni lazima awe na wadhamini wawili wa kuaminika ambao kila mmoja atasaini bondi ya shilingi milioni nne na kusalimisha hati zao za kusafiria mahakamani, sharti ambalo lilitimizwa na mshitakiwa huyo na akapata dhamana. 
Hakimu Kahamba, ameahirisha kesi hiyo hadi Juni 18 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kutajwa na kupangiwa tarehe ya kuja kumsomea maelezo ya awali mshitakiwa huyo.

Sunday, June 3, 2012

MAZOEZI NI AFYA


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano wakePICHA NA 

Saturday, June 2, 2012

ANNA MWALAGHO INVITES YOU FOR HER PERFORMANCES

Hello Friend,

I hope this message finds you well. To my new found friend,
I welcome you. Thank you for your support and acceptance to receive my
newsletter informing you of my performances.

The month of May has been very busy for me and busy is good.
I have met new friends and acquaintances through many of my events during this
month. I do not take for granted your support in any way. Thank you for letting
my self and also my band entertain you and also for buying my CDS and T-
shirts.

On June 16th my band and I will be at the Columbia
festival. Come get entertained and enjoy the summer, other bands will also be performing
and more details are given below. Come listen to our band that will make you
groove, enjoy spoken word and a bit of comedy at some of my events.

Do not forget to buy my new CD if you still have not
purchased a copy. The CD is called HAKI, a word in Kiswahili meaning justice.

Check it out and buy yourself a copy at or www.cdbaby.com/artist/annamwalagho
my CD is also sold on itunes.
http://itunes.apple.com/us/album/haki-justice/id450786720
http://fb.me/19H2VTgM7


June 16, 2012
ColumbiaFestival
Anna Mwalagho & Afrofloetry Band
Performance @ 2:45 – 3:45
p.m.

Venue:LakeStage,
ColumbiaTown
Center

Address:Columbia,MD
Free Admission

June 15, 2012
In Honor of Father’s Day
Hosted By: Ex-Saker Students Association
Venue:St.Andrews Hall
Address:15100 New Hampshire Ave
Silver Spring,MD
Time:8:00pm

June 9, 2012
Afrikan Goddess Awards
In Honor of Ms. Betty Makoni
Venue: O’Connor Auditorium at Trinity
University

Washington,DC.
Time:6:30pm-9:30pm
For More Information Visit
http://www.afrikangoddess.com

A POEM For You
Show Me Heaven
Lost in a haze
Thoughts begin to race
So much in my head
Feels like an explosion
Yet I can’t control
What thoughts are in my brain
The hardest part of all
Is I can’t explain

I can’t explain the hurt and the pain
The child in the streets
Begging in nakedness

I can’t explain
The slaughter of the weak
Through bombs and ammunition
In the name of liberation

I can’t explain the evil in the world
The rape and the killings
In the name of minerals

I can’t explain
The hunger and the famine
While the rich are getting richer
And the poor are getting poorer

I can’t explain the happiness in his face
The sadness in your face
Why she is sick and you are well
Each night and day

I can’t explain life and death
Why we are here then we are gone
In this place we call world

That’s why am in a haze
So torn each day
Not knowing which way
To go or to stay
So am hoping for a better place
Some heaven sweet paradise
Where justice is upheld
And the good are rewarded
And the evil burn in hell

by Anna Mwalagho


Upendo Girl Child
Foundation

I support a foundation in my country Kenya
through the sell of my Merchandise (CDS and T-shirts) The foundation runs a
school in the slums of Mathare in a community that is financially poor and lack
basic necessities. Most of the students are taught for free since there parents
are not able to afford, other children are orphaned and others from single
parent homes. . Even though the children do not sleep at the school they depend
on the foundation to help them with school supplies, food, and teachers pay. We
therefore are kindly requesting for your donations financially or in kind to
help the foundation and the needy of the community as Kenya is in the brink of another famine disaster.

"Doing nothing for others is the undoing of ourselves"- Horace Mann

God Bless you

Mwalagho productions LLC
www.annamwalagho.com


<><><><><><> <><><><><><><><><><><><> <><><><><><> <><><><><><> <><><><><><>