Monday, May 6, 2013

PICHA 15 ZA HILI KANISA LA ARUSHA LILILOSHAMBULIWA KWA BOMU MAY 5

Taarifa zilizopo ni kwamba tukio limetokea kwenye saa tano asubuhi kwenye Kanisa Katoliki Olasiti Arusha ambapo lilikua linazinduliwa na mgeni rasmi ambae ni balozi wa Papa hapa Tanzania.

Inasemekana chanzo ni bomu la kurushwa na mtu ambae aliwasili kanisani hapo na kurusha hilo bomu muda mfupi tu baadae ambapo walioumia wamekimbizwa hospitali ya Mount Meru.

Hakuna taarifa zozote za kifo mpaka sasa na mgeni rasmi pia amenusurika.

TheTZA millardayo.com inaendelea kufatilia taarifa zaidi na zikipatikana za uhakika utazipata hapahapa na link zake zitaanza kwa kuwekwa kwenye facebook yetu ambayo ni 
Hii ni baada ya mlipuko
Baada ya mlipuko.
Hawa ni baadhi ya walionusurika.
Picha zote zimepigwa na thechoicetz.com
Polisi wakiendelea na uchunguzi
Hizi picha 2 za mwisho nimetumiwa na my Bro Gaure Mdee.

CHUO KIKUU CHA VARGNIA DMV


Baadhi ya wanafunzi Watanzania wanaosoma chuo hicho Kutoka kushoto ni Alex John Luketa(student recruitment and marketing assistant in Virginia international University ),anaefuata Veronica N Magacha ,Cathereen Virginia Minja, Rehema Waziri ,Winfrida Josephat na Jose Fabian
Bendera ya Tanzania inayowawakilisha wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma chuo hicho cha Virginia International University. ikipitishwa mbele na mwanafunzi wa Kitanzania Winfrida Josephat.
 Wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa chuo.
 Bendera za nchi mbalimbali zinazowawakilisha wanafunzi na nchi wanazotoka zikisimikwa.
 Juu na chini ni picha ya pamoja ya wanafunzi waliomaliza chuo
Hapa chini ni Video ya Alex John Luketa akielezea jinsi ya kujiunga na chuo hicho hasa kwa wanafunzi wa kutoka Tanzania hebu msikilize
Now we are recruiting student for summer II and Fall 2013, Virginia International University Now we are can process admission very fast, just find me in FACEBOOK; Alex john Luketa and skype; alex.john.luketa in my number +15712449300 in this number you can get me in whatsapp,Tango,viber and also in my email alex@viu.edu) for more information visitwww.viu.edu.

Sunday, May 5, 2013

MAZISHI YA THADEO LWAKAJENDE NEW YORK


 Funeral home watanzania walikutana kwa ajili ya kuaga mwili wa marehemu Thadeo kabla ya kwenda kuupumzisha katika nyumba ya milele.
 Hii ndiyo nyumba mpya ya milele ya ndugu yetu mpendwa Thadeo

 Mwili wa Thadeo ukisitiriwa kwa kuwekwa udongo juu yake mungu ametoa mungu ametwaa mapenzi yake yatimizwe. Picha zaidi bofya read more.

Saturday, May 4, 2013

Agness Masogange Atupia Tena Kwenye Internet Picha za Umbo lake la Nyuma



See what My mama Gave Me......Habari Ndio Hiyo Mtoto Kaumbika vilivyo Mwenye Wivu Najua Atakuwa Amenuna.

Friday, May 3, 2013

WATU WATANO WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI WAUWAWA NA POLISI MKOANI MBEYA


Baadhi ya wananchi wakitoka kutambua miili ya wanaodhaniwa kuwa ni majambazi
Tunaomba radhi kwa kuonyesha picha hizi kwani mpaka sasa maiti hizi hazijatambulika
Kamanda diwani akiwaonyesha moja ya jambazi lililokuwa limeshika siraha


Hii ndiyo Gari iliyotumiwa na majambazi hayo
Siraha walizokuwa wanatumia majambazi hayo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.

Kamanda Diwani akikagua gari ya majambazi yaliouwawa



MTANDAO wa Ujambazi nchini hususani Mkoani Mbeya umezidi kusambaratishwa baada ya watu watano wanaodahaniwa kuwa ni majambazi kuuawa katika majibizano na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya. 


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani amewaambia Wandishi wa Habari Ofisini kwake kuwa Tukio hilo limetokea leo majira ya Sita Mchana katika kijiji cha Garijembe Wilaya ya Mbeya katika Barabara ya Mbeya Tukuyu.


Alisema Jeshi la Polisi kupata taarifa za Kinterejensia waliweka mitego mbali mbali na kufanikiwa kuwanasa watu hao wakiwa kwenye gari lenye namba za usajili T 911 BUG aina ya Toyota Spacio ambapo baada ya kusimamishwa katika eneo hilo wakitokea Kyela kuelekea Jijini Mbeya.


Alisema baada ya kusimamishwa ghafla walianza kurusha risasi ovyo ambapo Askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wote watano ambapo waliwafikisha katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Matibabu lakini Daktari alithibitisha kuwa tayari walikuwa wamekufa.






Aliongeza kuwa baada ya kufanyiwa upekuzi walikutwa na Silaha mbili ambazo ni bunduki aina ya SMG 848628 ambapo kwenye magazine zilibaki risasi 16 na bunduki nyingine aina ya Mark III yenye namba 94695J ikiwa na risasi mbili pamoja na Koa za Shaba.




Kamanda Diwani ameongeza kuwa taarifa za Kinterejensia zilieleza kuwa majambazi hayo yalijipanga kufanya uhalifu katika maeneo ya Ushirika, Tukuyu Mjini Wilayani Rungwe pamoja na Eneo la Uyole Jijini Mbeya.




Aidha alisema majina yao wala makazi yao hayakuweza kujulikana maramoja ambapo miiliehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na kutoa wito kwa wananchi kufika Hospitalini hapo kwa ajili ya kuwatambua ndugu zao ili wakabidhiwe kwa taratibu za mazishi.


Pia anatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zinazohusu uhalifu kuzitoa katika mamlaka zinazohusika kwa wakati ili zifanyiwe kazi.




Picha na Mbeya yetu 

Thursday, May 2, 2013

Lady Jay Dee "Siku Nikifa Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame"



Watu wanashtuka mtu akiongelea kifo, Utafikiri hawafahamu fika kuwa kila nafsi itakionja, Kwenye maisha yangu nimepitia mambo mengi, magumu na mepesi
Na bado naendelea ku experience mambo magumu zaidi kadri ninavyozidi kuwa mkubwa.
Siku za karibuni nimekuwa nikipigwa vita sana na watu wenye uwezo mkubwa kifedha , ki umri na hata wenye ukubwa wa connection katika hii industry ya muziki. Wanaomiliki chombo cha habari.
Nasimama na kusema kuwa sitokata tamaa, kwani lengo lao kubwa ni kuona na kuhakikisha nimeanguka kabisa na sipo katika ramani ya muziki.
Watu hao ambao vita yao ilikuwa baridi miaka kumi iliopita, sasa inazidi kuwa moto baada ya kutambua kuwa mimi ni mtu mwenye maamuzi yangu na misimamo yangu bila kuburuzwa.

Wanapita kila mahali kuhakikisha kila mrija unaoniingizia chochote unakatika, na hiyo ni kutaka kuuthibitishia umma wa Tanzania kuwa hakuna msanii anaeweza ku survive bila wao.
Mimi ni msanii tofauti na hao mnaofikiria.Nadhani mnafahamu tangu niachane na Tuzo zenu mnazo influence nani apate nani asipate, na tangu niachane na Fiesta nilipolipwa laki 8 mara ya mwisho na kuamua kuunda Band ili nijiajiri na kupata shows zangu mwenyewe, ikafanikiwa sana jambo ambalo limewauma na kuamua kufanya kitu cha kuiangusha Band yangu.
Nita survive kwa njia zozote MUNGU alizonipangia.Wakati bado wote tunapumua na kwakuwa watu hao hawanipendi kabisa, Naamini fika hawataweza kunipenda hata siku nitakapokuwa nimekufa.
Na huu ndio wosia wangu kwa watu hao.
Natambua wanaweza kutumia redio yao kutangaza sana kifo changu na kusema marehemu alikuwa mtu mzuri na pengine kupiga nyimbo zangu kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Ila naomba nitamke hivi, siku nikifa CLOUDS FM isipige nyimbo zangu, wala isiongelee lolote kuhusiana na kifo changu.
Ruge Mutahaba na Joseph Kusaga wasihudhurie msiba wangu, na mkiwaona muwapige wame. Enyi mtakaokuwa hai baada yangu.
Kama wamenifitini, na hawajanipenda nikiwa hai. Hakuna haja ya kujifanya kunipenda nikiwa marehemu.
Sina haja wanipende pia kwakuwa mimi sio ndugu yao, Ila ubaya wanaoundeleza mioyoni mwao wanaujua na nina hakika nafsi zao zinawasuta pia.
Niliamua kujiepusha nao miaka mingi na kufanya biashara zangu, nimekaa kimya watu wanafikiri nabebwa lakini sijabebwa chochote sikutaka ugomvi haya mambo yalianza baada ya Album yangu ya pili ya Binti mwaka 2003 nilipojitoa Smooth Vibes chini ya Ruge.
Nilivumilia fitna nikiamini ipo siku yatakwisha lakini naona moto ndio unazidi kuwaka.
Na hii ni kwasababu wanaogopa msanii akiwa mkubwa watashindwa kumuamrisha, Hamuwezi kumiliki dunia..
Kama mnasema mlinibeba mbona hamkuwabeba dada zenu wa tumbo moja waimbe ili hela irudi nyumbani??. kama kweli wewe Kusaga unajua kubeba basi beba jiwe liimbe liwe star..
Kwa roho zenu mbaya mnaweza kumbeba mpita njia nyie??.Talent haibebwi, hujibeba kama mnabisha si mna watoto wabebeni basi wawe kama kina Diamond ndio nitaamini kweli nyie mnaweza kubeba watu.
Mnawatishia wasanii kuwa yoyote atakaefanya nyimbo na mimi hazitapigwa, vikao vinne mmeshakaa kunijadili.
Mnadhani je! nitapungukiwa nini endapo wasanii wengine wakiacha kufanya kazi na mimi?? nyimbo hazitakuwa nzuri.
Basi sawa ngoja tuone MUNGU ni nani, Binadamu nani?? Kwahiyo mtaamrisha watu pia wasikae na mimi??
Ilikuwa niseme majina matatu huyo mmoja nimemsamehe baada ya kugundua sio hiyari yake ila yuko under influence ya hawa jamaa wawili.
Kila siku mnamsingizia Ruge peke yake Kusaga ni mfitini kuliko hata huyo Ruge, watu hamjui tu.
Mtu hela zote hizo bado shillingi mbili ya Jide inakuuma?? Roho gani hiyo??
Naishia hapo na sitabatilisha kauli yangu
JIDE

MAZOEZI YA REDD'S MISS KIBAHA YAPAMBA MOTO


Mkufunzi wa Warembo wa Redd's Miss Kibaha Rehema Uzuwiya akizungumza na warembo hawo wakati wa mazoezi yao yanayo endelea katika ukumbi wa Vijana Kinondoni.
Warembo wa Redd's miss kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao
Warembo watakao wania taji la Redd's Miss Kibaha wakiwa katika pozi wakati wa mazoezi yao yanayoendelea katika ukumbi wa vijana Kinondoni Dar es salaam picha na www.burudan.blogspot.com

WAFANYAKAZI BORA WAFURAHIA ZAWADI WALIZOPEWA

JANETH EZEKIEL AKIKABIDHIWA HUNDI SH MILION 2 NA RAISI JAKAYA KIKWETE KWA KUWA MFANYAKAZI BORA WA SHIRIKA LA PPF 
HAKIKA ILIKUWA NI FURAHA KUBWA KWA JANETI KWA KUCHAGULIWA KUWA MFANYAKAZI BORA

Wednesday, May 1, 2013

SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAMA


SHEREHE ZA MEI MOSI JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara mbalimbali za Serikali na Taasisi Binafsi wakiwa katika foleni wakijiandaa kuanza maandamano kuelekea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa ajili ya kushiriki maadhimisho ya Sherehe za Mei Mosi, ambapo katika Sherehe hizo mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Saidick, huku sherehe hizo kitaifa zikifanyika Kitaifa Mkoani Mbeya, na Mgeni Rasmi huko ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akiwa meza kuu na baadhi ya viongozi wengine wakati wakisimama kupokea maandamano hayo.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF, wakipita mbele ya jukwaa kuu na maandamano na mbwembwe za kucheza Kiduku, wakati wa sherehe hizo.
 Wafanyakazi wa TALGWU, wakipita mbele ya jukwaa kuu na Bango lenye ujumbe.
 Twiga Cement wao walikuwa wakipromoti bidhaa yao tu bila hata bango lenye ujumbe kuhusiana na sherehe hizo.
 Maandamano yakiendelea kupita mbele ya jukwaa kuu.
 Maandamano yakipita mbele ya jukwaa kuu........
 'Watenda Haki' wakipita na bango lao mbele ya jukwaa kuu