Thursday, April 25, 2013

WANAWAKE WAUNGANA KUSUSIA BIDHAA NA MAONYESHO YA MWANAMUZIKI DIAMOND




Kwa Kumdhalilisha Bi.Wema Sepetu kwa kumrekodi katika simu na kusambaza mazungumzo nyeti !

Kitendo cha Mwanamuziki wa kizazi kipya Nasibu Abdul Juma maarufu kama Diamond,cha kurekodi mazungumzo yake na star wa Bongo Move Bi.Wema Sepetu,
na kuyatuma mazungumzo yao ya mapenzi katika mitandao ni kitendo cha"Udhalilishaji wa Mwanamke" . kwa kuwa wanamuziki na wasanii wote wanatakiwa wawe ni mfamo na kioo cha jamii katika kuielekeza jamii kuishi 
kwa kufuata na kuheshimu maadili ,lakini mwanamuziki Diamond ameonekana kuwa ni kiongozi wa "Udhalilishaji wa Mwanamke" kufuatia kitendo chake cha
kurekodi na kusambaza mazungumzo yao ya simu ya kimapaenzi kati yake na
Bi.Wema Sepetu na mpenzi wake wa sasa Bi.Penny,kitendo hiki ni cha "kuwadhalilisha wanawake wa kitanzania" Tunaowaomba akinamama
na kinadada na wanawake wote kwa ujumla kususia kununua video,vcd,cd
pia kugomea kuhudhuria onyesho lolote lile litakalofanywa na mwamuziki
Nasibu Abdul Juma aka Diamond hadi pale atakapo waomba radhi wanawake wote
wa kitanzania popote pale walipo.
Wanawake wote wanatakiwa kugomea maonyesho ya mwanamuziki huyo na
na kutonunua bidhaa za mwanamuziki huyo Diamond ili kukomesha kabisa tabia hizi chafu za "Udhalilishaji wa Mwanamke" 
Wanawake wote ambao wamempa like au ad katika mitandao kama facebook kujiondoa mara moja na kogemea kununua
jarida au gazeti lolote lile litakalo mpamba mwanamuziki huyo.

MAGIGE FOUNDATION YATOA MSAADA DODOMA


Mama Tunu Pinda akihutubia

Asasi ya Kijamii ya Catherine Foundation jana imetembelea kituo cha kulelea wa watoto cha Matumaini Village kilichopo mkoani Dodoma ambapo walikwenda kutoa misaada mbalimbali wakiongozwa na Mkurugenzi wa Asasi hiyo, Catherine Magige. 
Katika Hafla hiyo Mgeni Rasmi alikuwa Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda ambapo asasi hiyo ilitoa vitu mbalimbali vikiwemo, Madaftari, Mafuta, Sabuni, Juice, miswaki na dawa zake, mchele, sukari, nguo za watoto, kanga za wakinadada wanaowalea watoto hao na vingine vingi.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akihutubia katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akihutubia katika hafla hiyo
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada 
Mhe Catherine Magige akicheza na mmoja wa watoto wa kituo hicho
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige akiwa na mtoto mchanga anaye lelewa katika Kituo cha Matumaini Village mjini Dodoma jana.
Mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Mhe Catherine Magige wakizungumza na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Mama Tunu Pinda na Mhe Catherine Magige wakiwa na watoto hao
Mama Tunu Pinda akikabidhi zawadi mbalimbali zilizotolewa na asasi hiyo 
Misaada mbalimbali ikitolewa
Mkurugenzi wa Catherine Foundation, Catherine Magige akizungumza na watoto wanaolelewa kwenye Kito cha Matumaini Village kilichopo Dodoma alipokwenda kutoa msaada

UNIC Dar yawahamasisha wanafunzi kujijengea utamaduni wa kusoma vitabu

Katika maadhimisho ya siku ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (katika ngazi ya Kimataifa) UNIC Bi. Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali waliohudhuria semina fupi iliyoandaliwa na UNIC na kuwafafanulia umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali ambapo wanaweza kujifunza mambo tofauti ikiwemo kujua takwimu za ugonjwa hatari wa Malaria hapa nchini ambao umekuwa ukiongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wenye umri chiniya miaka 5, hivyo kwa usomaji vitabu wanaweza kujua namna ya kujikinga na wanapogundua dalili kuweza kuwahi kupata matibabu.
Wanafunzi wa darasa la Saba shule ya msingi Oysterbay wakimsikiliza kwa makini Afisa Habari wa UNIC (katika ngazi ya Kimataifa) Bi. Stella Vuzo (hayupo pichani) wakati akielezea kazi zinazofanywa na Shirika la Afya Duniani WHO lililochini ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Ugonjwa wa Malaria unatokomezwa duniani katika nchini za kusini mwa Jangwa la Sahara. Ikiwa zimebaki siku mbili kuadhimisha siku ya Malaria duniani inayodhimishwa kila mwaka Aprili 25 wakati wa siku ya kuadhimisha siku ya uandishi wa vitabu na hati miliki duniani.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akiendesha chemsha bongo kwa wanafunzi walioshiriki semina hiyo kupima uelewa wao kuhusiana na Ugonjwa wa Malaria.
Picha juu na chini ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Usomaji na Maendeleo Bi. Demere Kitunga ambaye ni mmiliki wa Book Cafe iliyopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na nia na dhamira ya kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu vya nyanja mbali mbali ikiwemo vya Kiada, Ziada na vya maarifa ambapo amewapa changamoto kujianzisha Maktaba binafsi na vikundi ambapo wanaweza kuchangishana fedha kidogo kwa uwezo wao ili kuweza kujinunulia kitabu ambacho wanaweza kushirikiana kusoma ambavyo vitawapa uwezo wa kujitambua, kuwa na maamuzi, kupata uelewa wa vitu tofauti vinavyoweza kuwajengea kujiamini na kuwawezesha kubadilisha mfumo wa maisha katika makuzi yao.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania (UNCTN) Bernadetha Mshana akionyesha moja ya kitabu kilichomsaidia kuweza kupata uelewa wa kuongea Kingereza kwa urahisi zaidi ikiwa ni ushuhuda wake kwa vijana wenzake kuwa usomaji vitabu hupanua uelewa wa mtu na kujua mambo mengi.

KIFO CHA MWANAFUNZI UHASIBU NJIRO CHAZUA TAFRANI MABOMU YARINDIMA,,,,LEMA ASAKWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUCHOCHEA VURUGU

Umati mkubwa wa wanafunzi wa chuo cha uhasibu njiro jijini Arusha wakiwa wanamsikiliza kwa makini Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema mara baada ya kuandamana kutokana na mwenzao kuuwawa kikatili na watu wasiofahamika usiku wa juzi
Mkuu wa mkoa Magessa Mulongo pamoja na timu yake wakiingia katika eneo la shule ambapo aliambulia zomea zomea ,kurushiwa mawe,lugha za kejeli kutoka kwa wanafunzi hao kwa kile wanachodai kuwa serikali imekuwa siyo sikivu kutatua matatizo yao ya mara kwa mara ikiwepo kuibiwa vitu mbalimbali
Askari wakiwa tayari kukabiliana na wanafunzi hao waliosababisha vurugu huku Mbunge Lema akisakwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuchochea vurugu hizo
MWANAFUNZI wa mwaka wa pili katika chuo cha uhasibu kilichopo Njiro jijini Arusha,Henry Koga anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (25 hadi 30) ameuawa kinyama kwa kuchinjwa na kisu shingoni na kundi la watu wasiofahamika wakati wakitoka kwenye kumbi za starehe na wenzake.
Kufuatia tukio hilo ,kundi la wanafunzi walileta vurugu kubwa na kukataa kutii amri ya mkuu wa mkoa wa Arusha,Magesa Mulongo ya kuwataka warudi darasani wakati hatua zaidi za kisheria zikichukuliwa huku wakimzomea,hali iliyosababisha polisi kuingiliaka kali na kuwafyatulia mabomu zaidi ya 50 na baadhi yao kujeruhiwa.
Tukio la kuuawa kwa mwanafunzi huyo limetokea majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo ambapo marehemu huyo akiwa na wenzake walivamiwa na kundi la wahuni wapatao wanne katika eneo la CDA ,umbali mchache kutoka eneo la chuo hicho na kumchoma kisu shingoni .
Hata hivyo jitihada za wenzake kutaka kuokoa maisha yake kwa kumkimbiza hospitalini, zilishindikana kwani alifariki dunia muda mfupi baada ya tukio hilo kutokana na kuvuja damu nyingi.
Aidha wanafunzi hao walijikusanya asubuhi yake na kuanza kuandamana kushinikiza uongozi wa chuo hicho kutoa tamko juu ya vitendo vya uhalifu vinavyojirudia mara kwa mara katika chuo hicho bila kuchukuliwa hatua zozote na kufanya maisha ya wanachuo hao kuwa hatarini.
Wanafunzi hao walisikika wakilalamikia hali ya ukimya wa viongozi kushindwa kudhibiti matukio ya uhalifu kwani mwishoni mwa mwaka jana mwanafunzi mwingine aliuawa na vibaka kwa kuchomwa na kisu pia wanafunzi hao waliwahi kuvamiwa chuoni wakiwa wamelala na kuporwa vitu mbalimbali ikiwemo laptop simu na fedha.
Wakati vurugu za wanafunzi zikiendelea alifika mkuu wa mkoa wa Arusha ,Magesa Mulongo na kuwasihi waache vurugu na wakubali kumsikiliza hata hivyo wanafunzi hao zaidi ya 500 walianza kumzomea huku baadhi yao wakionekana kurushia mawe
Mkuu wa mkoa alilazimika kuondoka eneo hilo ,hatua iliyowalazimu askari wa kutuliza ghasia kufyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya na kujikuta baadhi yao wakijeruhiwa vibaya .
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ,Ibrahimu Kilongo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa wanafunzi zaidi ya 7 wanashikiliwa katika vurugu hizo huku uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea .

Wednesday, April 24, 2013

KATIBU MKUU DR WILBROD SLAA,MBUNGE WA UBUNGO JOHN MNYIKA,MBUNGE WA MBEYA JOSEPH MBILINYI AKA SUGU, MBUNGE WA IRINGA MJINI MCHUNGAJI PETER MSIGWA,MBUNGE WA ILEMELA EZEKIEL WENJE WAUNG'URUMA



 Mbunge wa iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa(juu ya gari kulia)na mbunge wa ilemelaEzekiel Wenje wakiwasili iringa kwa ajili ya mkutano mkubwa wa hadhara jana
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa(juu ya gari Kulia na Mbunge wa Chadema Ubungo John Mnyika wakiwa kwenye msafara wa kuelekea kwenye mkutano mkubwa wa hadhara iringa mjini Jana
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa. 
 Mbunge wa Mbeya mjini- Joseph mbilinyi aka Sugu akiunguruma kwenye mkutano mkubwa  wa hadhara wa chadema kwenye viwanja vya  Uwanja wa Mwembetogwa iringa jana
Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Akiunguruma mbele ya mamia ya wafuasi wa chadema kwenye mkutano mkubwa wa hadhara kwenye viwanja vya Uwanja wa Mwembetogwa iringa jana
 Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa Kushoto akipitia katiba kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliyofanyika iringa jana kulia kwake ni mbunge wa jimbo la ubungo Mh John Mnyika
 Sehemu ya mamia ya wafuasi wa chadema wakisiliza hotuba mbalimbali kutoka kwa viongozi mbalimbali wa chama hicho viwanja vya Uwanja wa Mwembetogwa iringa jana. Picha Zote na Chadema na Said Ng’amilo
--
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa amemlipua kigogo mmoja wa juu wa CCM (jina tunalihifadhi kwa kuwa hakupatikana kujibu tuhuma hizo), kuwa ndiye kinara wa biashara haramu ya pembe za ndovu na utoroshaji wa wanyama nchi za nje.

Akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa jana, Mchungaji Msigwa alisema anashangaa Serikali ya CCM kushindwa kumchukulia hatua.
 
Mchungaji Msigwa alidai kuwa tembo wapatao 75 wamekuwa wana

NDANI YA BONGO MAISHA TAMBARALE



Hizi ni nyongeza nyingine muhimu katika sura ya Jiji la Dar es Salaam. Jengo lenye column ya blue ni la Utumishi, na ile nguzo kule mbele ni Nguzo ya kuongozea meli wakati zinaingia au kutoka bandarini 
Ni ile iliyokaribu na mnara wa askari
Mnara wa askari, 
Wamaasai na mila zao Jiji la Dar.Kwa taswira zaidi ya jiji la Dar.....bofya Read more Home sweet home...

Tuesday, April 23, 2013

PICHA HII KUTOKA FACEBOOK KAMA IMEKUTOKEA WEWE HII UNACHUKUA UHAMUZI GANI?


ALIYEKUWA MKUU WA UPELELEZI MKOA WA DAR ES SALAAM ABDALLAH ZOMBE AKITOKA MAHAKAMA YA RUFAA JIJINI DAR ES SALAAM BAADA YA NOTISI YA RUFAA DHIDI YAKE KUGUNDULIKA INA MAPUNGUFU



Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam Abdallah Zombe akitoka Mahakama ya Rufaa jijini Dar es Salaam jana,mara baada ya notisi ya rufaa dhidi yake kugundulika ina mapungufu,kulia ni Wakili wake Richard Rweyongeza.Picha na Michael Jamson 

ZIARA YA MAKLAMO MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) Dk.ALI MOHAMED SHEIN ZANZIBAR


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Mpendae,alipowasili katika Tawi la CCM Meya,kutoa kadi za Chama kwa wanachama wapya wa chama hicho,akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Wilaya ya Amani Mkoa wa Mjini Unguja leo.
 Kikundi cha sarakasi cha Jimbo la Mpendae ,wakionesha umahiri wa sarakasi katika viwanja vya Tawi la CCM Meya Wilaya ya Amani,wakati wa Mkutano wa wa wananchi wa Jimbo hilo uliohutubiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

 Wanachama wa CCM Tawi wa Jimbo la Mpendae,wakiwa katika Mkutano wa kuwakabidhi kadi Wanachama wapya wa CCM, pamoja na Jumuiya za chama hicho,katika viwanja vya tawi la CCM Meya,Mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akimkabidhi Kadi Mwanachama Mpya wa UWT Subira khamis,huko Tawi la CCM Meya  akiwa katika ziara ya kuimarisha Chama katika Mkoa wa Mjini Unguja  pamoja na kutembela miradi mbali mbali ya Chama leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Vijana wa Kikundi cha UB40 cha Mpendae,wakiongozwa na Mohamed Salum Mohamed,baada ya kutoa burudani yao wakati wa Mkutano. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu ZNZ

Boston bombing victim whose leg was saved by student, 23, describes how terrifying ordeal has turned them into life-long friends

Firm friends: Ron Brassard, 51, and 23-year-old Rob Wheeler bonded after the student helped staunch the bleeding in his seriously wounded leg following the Boston bombing

Hour of need: Mr Brassard has a tourniquet applied to his leg by Mr Wheeler in one of the many scenes of bravery that emerged during the terrorist attack last Monday

Mr Wheeler, a Framingham State College student who is originally from Marshfield, had just finished the 26-mile race and was near the finish line on Boylston Street during the massive explosion.

Mr Brassard was nearby with his wife and daughter cheering on a friend who was running the race.
The student, who had stepped in last minute to run the race for a friend, rushed to the 51-year-old's side after he heard Mr Brassard's daughter crying out for someone to help her father. 

Mr Wheeler said that he relied on what he remembered from first-aid training and his interest in sports medicine to staunch the bleeding in Mr Brassard's leg, caused by severe shrapnel wounds. 
The 23-year-old plans to join the Marines after he graduates next month. 
Agony: Mr Brassard, pictured on a stretcher, was one of more than 180 people injured in the attack on Boston
Fate: The 23-year-old student was not even supposed to be running the race but stepped in for a friend

Mr Brassard told NBC: 'At that moment I absolutely needed someone to help me. And that someone was Rob.'

Mr Brassard's wife and daughter also suffered shrapnel wounds. However they had recovered enough to attend the Boston Red Sox game on Sunday after the team gave them free tickets. 


Ron had not recovered well enough to attend the game so asked his 23-year-old new friend to accompany his wife and daughter instead. 


The Brassard family also plan to attend Rob's graduation on May 19. Mr Brassard added: 'We're part of each other's life now.'