Sunday, December 14, 2008




Rais mteule Barack Hussein Obama na familia yake, wakiwa wameelekeza macho na masikikio kwenye luninga usiku wa tarehe 4 Novemba. Mamillioni ya watu duniani kote walikuwa kama kina Obama katika siku hiyo ya kihistoria. Zimebakia siku chache kwa jamaa na familia yake kuingia Jumba Jeupe na matumaini ya walio wengi ni kumuona bwana Obama akiliongoza Taifa hili kurudia kwenye neema na maendeleo kwa watu wake pamoja na kulirudishia heshima duniani.
Kwa maoni ya walio wengi, Rais anayemaliza muda wake(bwana Kichaka), ametuyumbisha sana kwa kutuingiza kwenye mengi ya matatizo tunayokumbana nayo kwa sasa. Historia pekee ndiyo itakayo muhukumu bwana Kichaka kwa damu nyingi aliyoimwaga Iraq na mengi mengineyo.


No comments:

Post a Comment