Monday, January 5, 2009

SAMAHANI!! SAMAHANI!! SAMAHANI!!
Ningependa kutoa samahani zangu za dhati kwa wasomaji wote wa blogu hii pamoja na ye yote aliyeguswa na posting inayosema "MAAJABU 7 YA WAKRISTU". Nia yangu haikuwa kukashifu dini au Wakristu kwa namna yoyote ile. Mimi naheshimu sana imani ya kuabudu ya kila mwanadamu na kuziheshimu dini zote. Mimi si mdini na sijalelewa hivyo, na labda tu ningeongezea kwa kutaarifu kwamba mama yangu pamoja na upande mzima wa ndugu wa mama ni Wakristu. Mke wangu pia ni mkristu.
Nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na uchapishaji wa utani huo, ambao ulitoka kwa ndugu yangu ambaye ni Mkristu sana, na sikutegemea kabisa kama ingeleta kutokueleweka kulikotokea. Nimeamua kuyaondoa mara moja maandishi hayo katika blogu hii na kutoa ahadi ya kuwa mwangalifu sana siku za mbeleni. Madhumuni na nia ya kuanzisha blogu hii si kukashifu, kutukanana au kuvunjiana heshima bali ni kuchangia matukio na kuelimishana ili kuendeleza jamii.
FUNDI K.R.

14 comments:

  1. Hello Mr. Fundi Kombo.... Faith is very personal thing and sensitive issue, mimi kama Mkristu niliisoma hiyo na sikuona ubaya (understand as a joke), but for those who reacted nadhani ni sababu ya imani zao, na wengine wengi bado wanachukulia kila kitu literal.... pole bwana..... that is all about faith

    ReplyDelete
  2. Akhsante sana kwa kulielewa hilo.

    ReplyDelete
  3. Well done umefanya vizuri kwa heshima yako bora umefanya hivyo.

    ReplyDelete
  4. umesomeka roja keep on posting

    ReplyDelete
  5. Mr Fundi Hayo ni vijimambo tu. Mbona mengi yatasemwa. Mie ni Mkristu kabisa lakini sikuona kama kuna ubaya wowote bali kwanza nilichukulia kama ni challenge kwetu wakristu kwa sababu wengi wetu sio wakritu, sio waislamu tumepotoka sana hivyo mambo hayo ni chaallenge. Nafikiri aliyeguswa na hilo kaguzwa na ukweli uliopo kwenye ujumbe huo. Hata hivyo watu tu wengi wa tabia na vionjo mbalimbali,uangalifu ni muhimu.Pole sana

    ReplyDelete
  6. FUNDI WA KOMBO POLE KAKA KWA YALIYOKUKUTA,MIMI PIA NILIPOSOMA NILIELEWA KUWA NI JOKE KUMBE KILA MTU ANAMTAZAMO WAKE,LAKINI NDIO VIZURI TUNAELIMISHANA INABIDI TUWE WAANGALIFU SANA NA HIZI BLOG ZETU.

    ANYWAY TUACHANE NA HAYO HONGERA SANA NIMEPENDA BLOG YAKO NI NZURI SANA.

    ReplyDelete
  7. Pole sana kaka fundi kuna wahenga walisema mwanzo huwa mgumu,pia kula na kipofu angalia mkono wake, na yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

    Hongera Blog yako ni nzuri pia.

    ReplyDelete
  8. Umevamiwa na siasa kali? Unatakiwa kuwa stable hasa wakati ukiwa hujakosea.

    Usitaraji coments ambazo ni positive tuu bali mchanganyiko.

    ReplyDelete
  9. Unajua wewe ni wa imani tofauti na utani ulio weka hivyo haikua busara kuleta hiyo habari hata kama ni kutoka kwa mkeo aliye mkristo utani wa biblia ni kwa msoma biblia na muamini biblia na si vinginevyo.

    ReplyDelete
  10. Kwanza kabisa niseme Karibu kwenye ulimwengu wa ku-blog. Nami ni rookie kwenye ulimwengu huu lakini naamini nimekutana na vikwazo kadhaa vilivyonijenga kiutendaji. Pili nasema japo kuna maoni na maneno mbalimbali, lakini wapaswa kutambua kuwa kila mtu ana namna aangaliavyo tatizo. Blog yangu yaitwa "the way you see the problem is the problem" na nahisi ndilo lililokukuta hapa. Mtazamo wa watu kulingana na tatizo. Basi kwa hilo nikupe pole. Na mwisho ni kukupa moyo katika kusonga baada ya hili lililotokea. Jaust kutambua hadhira yako yahitaji nini na kisha kuwawekea kwa nia ya kuwaelimisha, kuwaburudisha na kuwakomboa na hapo utakuwa umekamilisha nia yako ya uandishi. "House style" na contents za blog ni uamuzi wako na kwa kuwa huwezi kumfurahisha kila mtu, basi angalia kikufaacho na kiifaacho jamii utakayo kisha u-stick nacho.
    Karibu sana "changamotoni"

    ReplyDelete
  11. Bwana Kombo nadhani utani huo hakuwa mzuri kabisa, first wewe siyo Mkritu kumbe kwa kuweka ujumbe huo kwa vyovyote vile watu wange react. Napenda sana mdau wa juu alivyo ongea kuwa imani ni mtu binafsi, kumbe kama mkeo ni mkristu hilo halina maana yeyote, maybe ungeweka any joke linalohusu Uislam then I could understand, nadhani ulilujua hilo ndiyo sababu ukaweka hilo la Wakristu sababu kila mara wamezoea kuandambwa. Kumbe kula Sweden hule mchoro wa Mtu mambo yalikuwaje? Naipenda sana glob yako, kumbe ni vizuri tuwe makini kwenye dini, ingawa Nyerere alisema kuwa Tanzania siyo nchi ya dini, lakini mimi nasema kwa sasa we are, thanks

    ReplyDelete
  12. mimi binafsi nimekusamehe kwa sababu umejua kosa lako na umelikubali kosa vilevile umeahidi kuto rudia kosa, na nimeipenda sana blog yako kwani inavitu vingi sana anbavyo huwa navitafuta mfano ni hiyo exchange money, ambayo naweza kuipata kirahisi kutoka kwenye i blog, big up bro, na naomba usikate tamaa,

    ReplyDelete
  13. big up bro kombo! kuendeleza libeneke, du blog yako ni nzuri na inavutia kweli, kuna vitu vingi vizuri, usiwasikilize hao wasitaka kuelewa kwani hata mungu alisema samehe 7 mara 70, ije kuwa wewe na ukiwa umesha omba msamaha,

    ReplyDelete
  14. Unaomba msamaha wa nini mzee mbona unajibebesha makosa usoyafanya?!!
    Wanaomaindi ndo walioguswa na iyo post kwanza wakristo wengi ndo tulivyo.

    Mi sidhani kama mtu ni mkristo kweli akasirike kwa iyo post isitoshe wengine tumeguswa na tumeanza kufanya mabadiliko kidogokidogo ingawa ilikuwa ni katika hali ya utani but message sent.

    Tatizo wakristo wengi wababaishaji na wakiambiwa ukweli wanakuja juu,kama mtu unaimani na Mungu wako huwezi kukasirika na wala hakutajwa mtu wala kudharauliwa,mi nadhani ni kutokuwa wakamilifu ndo kunakotufanya baadhi yetu kuona ka tumedharauliwa ilihali si lengo la bwana Fundi,kama kuna nyingine mzee we zipost tu achana na hao wanaotaka kukuendesha kama vp wafungue blog zao.

    Kosa kubwa ulolifanya ni kuomba msamaha pasipo sababu na kuonekana huna msimamo katika libeneke kwa kuyumbishwa na watu wachache.Blog yako imetulia mzee na watu tuta-visit tu wala usijali kwani kizuri chajiuza...ati.
    Acha kubabaika,kuwa na msimamo mzee we piga kazi,those who want to talk,let them talk so long as it`s everyone`s right na ndo maana kuna sehemu "Post a comment"

    Ama kweli UKWELI UNAUMA.Usiibanie hii comment fundi ohoo!

    Potz.

    ReplyDelete