Tuesday, August 14, 2012

MJI HUU WANAUME NI MARUFUKU


Kwa mara ya kwanza duniani, mji ambao wanaume hawataruhusiwa kuishi unajengwa nchini Saudi Arabia ambapo ni wanawake pekee watakuwa wakiruhusiwa kuishi na kufanya kazi kwenye mji huo mpya utakaojengwa kisasa katika nchi hiyo ya kislam.
Mji mpya kwaajili ya wanawake pekee ukiwa na viwanda mbalimbali unajengwa nchini Saudia Arabia ambapo katika mji mzima wanawake wataishi wenyewe na wakifanya kazi bila ya kuwepo ya hata mwanaume mmoja.
Katika kuwapa nafasi wanawake kufanya kazi kwa uhuru kama wanawake wa sehemu zingine duniani, Saudi Arabia inatarajia kujenga mji wa kisasa kwa ajili ya wanawake pekee.
Mji huo utakaogharimu dola za Marekani milioni 133 utaanza kujengwa mwakani karibu na mji wa mashariki mwa Saudi Arabia wa Hafuf.
Mji huo utakuwa na viwanda vya nguo, madawa na vyakula na inakadiriwa kuwa jumla ya wanawake 5,000 watapata ajira.
Hatua hii ya kuanzishwa kwa mji wa wanawake pekee inakuja ili kuwapa nafasi wanawake kuendana na wakati na kufanya kazi na pia kuwapa mazingira ya kazi yatakayoenda sambamba na sharia za kiislamu.
Mamlaka ya viwanda ya Saudia, Modon imesema kuwa ina mpango wa kuanzisha mji wa pili wa wanawake pekee mbali na mji wa Hafuf.

No comments:

Post a Comment