Tuesday, August 14, 2012

VURUGU ZA WACHIMBA KOKOTO ZAFUNGA BARABARA KIGAMBONI


Wanausalama wakizima moto uliosababishwa na mataili yaliyochomwa na wachimba kokoto.…
Polisi wakijihami wakati wa mapambano na wachimba kokoto hao.


Baadhi ya vijana waliotiwa nguvuni na polisi katika vurugu hizo.

...Vijana hao wakiwa kwenye Difenda tayari kuelekea kituo cha polisi.

Eneo linalochimbwa kokoto lililosababisha vurugu hizo.

WACHIMBA kokoto eneo la Kigamboni Maweni, leo wamezua vurugu baada ya kufunga barabara na kuchoma mataili kutokana na kuzuiliwa kuendelea kuchimba kokoto eneo hilo wakati wananchi wenye asili ya Kihindi wakiruhusiwa kuchimba. Polisi walilazimika kuingilia kati huku wakitumia mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia hizo.

No comments:

Post a Comment