Monday, August 20, 2012

SALAMU ZA EID MUBARAKA KUTOKA SPRINGFIELD MASS


 Ustadh Kibodya katikati akiwa na watanzania wenzake waishio Springfield, Mass wakitoka msikitini kusali swala ya Eid, Swala ya Eid hiyo ilifanyika katika msikiti wa Islamic center, west Springfield, Mass. Baada ya swala walielekea Forest Park kwa ajili ya chama choma na vinywaji laini, hiyo yote ni kusherekea Eid Mubaraka. Picha na matukio ya kama unavyoona kwenye picha hapa chini.


 Hapa kama unavyoona ni mishikaki na kuku ikiwekwa jikoni na Omary Kibodya wa huko Springfield  kila kitu  hapa ni Halal, Si unajua mambo ya waislam tena kwa kujipendelea.
 
 
 Akina mama wakijipatia chakula kabla ya akina baba, mambo ya Ladies first hayo
 
 
 Dada Hidaya kushoto akiwa na mama mwenye nyumba wa Ustadh Kibodya kulia wakiachia tabasamu mbele ya  ukodak wakisubiri kitoweo.
 
 

Akina mama wakiwa na familia zao katika picha ya pamoja kabla ya kuondoka sehem ya tukio hapo Forest park.picha kwa hisani ya Ustadh Kibodya!!!


No comments:

Post a Comment