Wednesday, February 20, 2013

BARABARA YA MOMBASA - MAZIZINI SASA TAMBARARE


Mkeka wa Barabara hiyo unavyoonekana kwa sasa. Madereva wamelalamika pia barabara hiyo kubana sana na kukosekana kwa njia za watembea kwa miguu.
Mashine za kushindilia lami za Kampuni ya Ujenzi ya Del Monte ya Jijini Dar es Salaam zikiwa kazini wakati wa kushindilia kipande cha barabara ya Mombasa hadi Zahanati ya Ebeneza iliyopo jirani na Ukonga Mazizini jijini Dar es Salaam. Ujenzi huo wa kiwango cha lami katika barabara hiyo iliyopo chini ya wakala wa barabara TANROADS unafanywa na Manipaa ya Ilala. 
Aidha wananchi wamepongeza hatua hiyo ya ujenzi katika kipande hicho korofi cha barabara na kuiomba Manipaa Hiyo kuongeza fungu na kuendelea na barabara hiyo hadi Mazizini na baadae ufike eneo la Moshi Bar na Kwa Mkolemba.

No comments:

Post a Comment