Wednesday, February 20, 2013

Ningekuwa Kawambwa, au Mulugo Ningejiuzulu

Na Bryceson Mathias

KWA matokeo Bomu ya kidato cha nne ya Mwaka 2012, ni wakati muafaka sasa, Serikali inatakiwa ijihoji na kujisikia aibu inatengeneza taifa Bomu la aina gani kupitia sekta ya Elimu? Hii ni kwamba kama ningekuwa Shukuru Kawambwa (pichani kulia) au Philipo Mulugo, ningejiuzulu nipishe wengine nao wajaribu.

Kwa matokeo mabaya na ya kusikitisha ya Kidato cha nne yaliyotangazwa kwa mwaka 2012, ni budi Serikali iepuke usanii na ikubali kukosolewa na wachambuzi wa Elimu na ijihoji na kujitathini na kuona, huko mbele inatengeneza na kuzalisha Taifa Bomu la aina gani nchini? .

Usanii ninaousema ni pamoja na madudu yaliyobainika kuandikwa na wanafunzi kwenye majibu hali inayotuoonesha kwamba, alivyo mfalme ndivyo walivyo wafuasi wake, kwamba maana ya kuwa yalivyo matokeo ya wanafunzi wetu nchini yanatuonesha namna ya viongozi na watalaam wa elimu tulionao.

Ninasema hivyo kwa sababu wadadisi wa mambo wanasema, likiwepo Taifa Bomu, huzaa Viongozi Bomu, na Viongozi Bomu hutoa mazao Bomu, ambapo Mazao hayo Bonu nayo hutoa utendaji Bomu, na kama utendedaji utakuwa Bomu, basi hakuna maendeleo na ustawi wa Taifa na wananchi wake.

Hivi karibuni kupitia kwa Mbunge wa Kuteuliwa James Mbatia NCCR-Mageuzi alilalamikia Udhaifu wa Sekta ya Elimu nchini, lakini kuna watu ambao watoto wao hawasomi kwenye shule za kata labda nje au kwenye Shule St. zinazofanya vizuri kutokana na uwezo wao waliipuuza wakisema serikali inafanya mapitio.

Mambo ya muhimu yakizuiwa kwa madai ya kufanya mapitio, maana yake ni kwamba hayastahili kushughulikiwa kwa dharura hali inayokinzana na Hoja ya Mbatia akitaka liwe jambo la Dharura na Muhimu linalopaswa kupewa kupaumbele lifanywe Haraka.

Kinachoonesha kama tunao watalaam wa elinu kwenye sekta hiyo basi wakati wakiwafunisha watalaam wetu hao wakati wa kufundisha ubaoni, labda walipokuwa wakiandika na Chaki zao ubaoni, Chaki hizo ziliznguka chini hivyo walishindwa kuandika wakati wa kuwafundisha watoto wetu.

Kama chaki za watalaam na viongozi hao zilianguka, ni dhahiri kuwa na hata baadhi ya walimu wetu kwenye Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Chaki zao inaonesha zimeanguka kiasi cha kutupatia matokeo duni yanayowapendelea vigogo wenye uwezo wa kuwapeleka watoto wao shule za St.

Matokeo haya ni dhahiri yamewaumbua walioifuja hoja hii na licha ya kuwapatia aibu kwa nyakati fulani nilimshangaa Waziri wa Elimu Shukuru kawambwa alikuwa anacheka badala ya kusikitika au kulia kabisa.

Nakasirishwa na baadhi ya viongozi ambao wakishauliwa juu ya elimu wanajifanya wanajua wakati hawaju huku mambo kwa watoto wetu yakienda mrama na ya watoto wao yakienda vizuri raha mustarehe!!.

Kama serikali kwa macho yake imeshuhudia wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu wakifaulu Mtihani wa Darasa la Saba, na wazazi wao kukataa kuwaruhusu watoto wao kuendelea na kidato cha kwanza Mfano Bahi Dodoma mzazi alikataa mwanae aisome kwa na Mbeya ambako Mbunge aliliambia Bunge. Je kwa msingi huo tuna sababu ya kuwa na Kawabwa na Mulugo wizarani?

Aidha ni ushauri wangu Wizara ya Elimu na Ufundi tangu Makao Makuu ya Elimu wizani hadi wilayani ifumuliwe na kuwekwa nyuso mpya zisizo za usanii wa sekta hiyo, maana sasa ndiyo tunabaini malalamiko ya walimu.

No comments:

Post a Comment