Wednesday, February 20, 2013

Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba abiria wa kawaida kwa waombaji wapya wenye magari yenye uwezo wa kubeba abiria wasio zidi 14



Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Athumani Diwani 
Mamlaka ya Uthibiti wa Usafiri wa Nchi kavu na majini( Sumatra) Mkoani Mbeya imesitisha utoaji wa leseni ya kubeba abiria wa kawaida kwa waombaji wapya wenye magari yenye uwezo wa kubeba abiria wasio zidi 14.
Aidha Mamlaka hiyo imesema kuwa endapo wamiliki hao wa magari hayo watahitaji kutoa huduma kwa jamii mamlaka hiyo itatoa leseni kwa ajili ya kubeba watalii tu .

auli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Ndugu Diwani Athumani wakati akizungumza na madereva wa mabasi madogo yaendayo Mji mdogo wa Tunduma Wilayani kufuatia kuwepo kwa mgomo uliodumu kwa miezi 3 sasa ambao umefanywa na madereva hao kwa kuto safirisa abiria waendao Tunduma.
Mgomo huo wa madereva hao umesababishwa na baadhi ya wamiliki wa magari madogo aina ya( Noah) ambayo yamekuwa yakifanya shughuli ya kubeba abiria toka Mbeya hadi Tunduma hali iliyo zua mgogoro mkubwa baina ya wamiliki wa gari hizo Ndogo pamoja na madereva wa Costa ambao ndio wenye leseni za kusafirisha abiria Toka Mbeya hadi Tunduma.
wali wakati akizungumzana madereva hao Kamanda Diwani amewataka mara moja watu wanaofanya biashara hiyo kuacha mara moja kwani sheria itachukua mkondo wake.
Amesema sababu kubwa ya kusitisa huduma inayo tolewa na magari hayo madogo ni kuzuia majanga ambayo yanaweza kutokea kwani gari hizo hazina madirisha makubwa pamoja na milango yake kuwa midogo ambayo na haina milango ya dharura endapo kunaweza kutokea tatizo lolote.
Kufuatia hali hiyo Kamanda Diwani amewataka madereva costa ambao wamekuwa wakitoa huduma hiyo kwa muda mrefu kuachana na mgomo huo badala yake waendelee kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyo kuwa awali.

No comments:

Post a Comment