Mtoto Ombeni Mbeula ambae ameungua kwa moto vibaya kama anavyoonekana anahitaji msaada wako (TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI WADAU)
Mama wa mtosto Kilaudia Kigailaakiwa na mwanae huyo.
HUJAFA hujaumbika bado mtoto Ombeni Mbeula amenusurika kifo baada ya nyumba aliyokuwa akiishi kuteketea kwa moto wakati mtoto huyo akiwa ndani baada ya mama wa mtoto huyo kuwaacha watoto hao na kwenda shamba eneo Chitemo wilaya ya mpwapwa mkoani Dodoma.
Imedaiwa kuwa moto huo ulitokea wakati mvua inanyesha ghafla nyumba ilibomoka na wakati huohuo walikuwa watoto wawili walikuwa jikoni ndani ya hiyo nyumba na ndipo kijana huyo alipotetekea kwa moto
Baada ya tukio hilo kutokea ikafanyika uokoaji kwenye nyumba hiyo maeneo ya Chitemo na kufanikisha kuokoa watoto wote wawili kati ya mmoja aliumia kwa kuangukiwa na udongo wa nyumba hiyo na huyu Ombeni Mbeula aliangukia kwenye moto mpaka kuungua hivi unavyoona kwenye picha lakin hali zao ni salama kwa wote.
Baada ya uokoaji waliamua kumpeleka mtoto huyo kwenye hospitali ya Mima iliyoko Mpwapwa ikashindikana madaktari wakamuagiza aende hospitali ya Mpwapwa hapo hospitalini wakakaa siku mbili katika hospitali ya mpwapwa na siku ya tatu wakaambiwa waende hospitali ya rufaa iliyoko Dodoma Mjini ambayo ni inajulikana General kwa matibabu zaidi.
Walipofika katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakaanza matibabu lakini uwezo wa kipato cha wazazi wake sio kizuri inahitajika msaada kwa matibabu maana hata dawa hajapatiwa na pesa kwa ajili ya matibabu haikuweza kupatikana paka sasa
Kama umeguswa kutoa ni moyo sio utajiri muokoe mtoto huyu maana hata kula anashindwa mpaka kuona anaona kwa mbali sana.
Mama yake hana simu lakini anatumia simu ya ndugu yake Ekiria Paskali
Kwa yeyote atakayependa kumchangia mtoto huyo atume chochote kwenye namba hii au atumie M- pesa kwenye namba hii 0757 498336
No comments:
Post a Comment