Thursday, February 21, 2013

RAIS WA KENYA MWAI KIBAKI AKAMILISHA ZIARA YAKE NCHINI TANZANIA

Rais Mwai Kibaki wa Kenya akikata utepe, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda kuzindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa na iliyokuwa Old Bagamoyo .
. Rais Mwai Kibaki wa Kenya akifunua pazia, akishuhudiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli na Meya wa Kinondoni Mstahiki Yusuph Mwenda akizindua rasmi jina la Barabara ya Mwai Kibaki linalochukua nafasi ya jiba la barabara ya Old Bagamoyo leo kwenye makutano ya barabara ya Bagamoyo na Rashid Kawawa.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mwai Kibaki akiwasalimia wazee wa mkoa wa Dar es salaam mara baada ya kuwasili katia ukumbi wa mikutano wa PTA viwanja vya maonyesho ya sabasaba jijini Dar es salaam.
Rais wa Kenya Mwai Kibaki akizungumza na watanzania kupitia wazee wa mkoa wa Dar es salaam leo wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania.
Wazee wa mkoa wa Dar es salaam wakimsikiliza Rais Mwai Kibaki wakati alipokua akizungumza nao leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa wazee wa mkoa wa Dar es salaam Bw. Abdallah Tamba (kushoto) akitoa maelezo kwa rais wa Kenya Mwai Kibaki kuhusu zawadi za wazee alizokabidhiwa leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Kenya Mwai Kibaki akiingia ndani ya Kiwanda cha Magereza Ukonga kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo.
Kikundi cha burudani cha ngoma za asili cha Jeshi la Magereza kikitoa burudani wakati wa mapokezi ya Rais wa Kenya Mwai Kibaki katika gereza la Ukonga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe akitoa muhtasari kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kukamilika kwa wa ziara ya siku mbili ya Rais wa Jamhuri ya Kenya Mwai Kibaki katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati), makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal (kushoto),waziri Mkuu Mizengo Pinda (kulia) na viongozi wengine wa serikali wakimpungia mikono Rais wa Kenya Mwai Kibaki ishara ya kumuaga wakati akiondoka nchini Tanzania kurejea Kenya kufuatia kukamilika kwa ziara yake ya siku mbili. - Picha zote na Aron Msigwa - Maelezo.

No comments:

Post a Comment