Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akishuhudia mlundikano wa magodoro na hali ya sehemu wanayolala wavulana wa shule ya Mount Zion kwenye moja ya vyumba vya darasa vilivyotengwa kwa ajili ya kujisitiri. |
ZIARA ya kushitukiza iliyofanywa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza akiambatana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya ukaguzi katika shule ya sekondari ya Mount Zion iliyoko ilemela jijini Mwanza imebaini wanafunzi kuishi katika mazingira hatarishi huku uongozi wa shule hiyo ukiwaficha vichakani zaidi ya wanafunzi 50 wa bweni kukwepa ukaguzi.
Hatua hiyo inafuatia kuwepo taarifa zilizotolewa kwa mkuu huyo na baadhi ya wasamaria wema hali iliyomlazimu mkuu wa wilaya na ujumbe wake kufika shuleni hapo ili kujionea endapo uongozi wa shule hiyo umeboresha kasoro na mapungufu yaliyoonekana baada ya ukaguzi wa awali kufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita baada ya kutakiwa kuyafanyia kazi mapungufu hayo na Idara ya Afya na Elimu ukaguzi.
Wanafunzi 50 waliobainika kufichwa waumbuliwa. |
Akizungumza huku machozi yakimbubujika kwa uchungu wa hali aliyoishuhudia shuleni hapo Mkuu wa wilaya ya Ilemela Bi. Amina Masenza ameeleza kusikitishwa kwa kitendo hicho na kukilaani vikali akiagiza hatua madhubuti za kisheria kuchukuliwa dhidi ya Mkurugenzi wa shule hiyo….
Hii ndiyo hali halisi ya ukaaji ndani ya darasa hili jeh kwa mpango huu kuna usalama wa kufanya vyema kazi za darasani na hatimaye kufaulu kwenye mitiani kihalali? Kwa Picha Zaidi |
No comments:
Post a Comment