na Danny Tweve wa Indaba Blog
Halmashauri ya wilaya ya MBOZI kupitia kitengo cha kudhibiti UKIMWI imeendesha warsha ya siku moja kwa wenyeviti wa kamati za kudhibiti UKIMWI za kata pamoja na mambo mengine kuzungumzia kampeni ya tohara kwa wanaume inayoendelea kutekelezwa kupitia hospitali ya wilaya ya Mbozi
Akizungumza kwenye warsha hiyo mratibu wa Kudhibiti UKIMWI wilaya Bwana Oscar Mgani alieleza kuwa katika kipindi kirefu wanachi wamekuwa wakihamasishwa kutoa mikono ya sweta, na sasa mwitikio umepanuka hadi kwa watoto wadogo
Katika hali ya kuonyesha watu wanakumbwa na aibu kwa kuendelea kuwa na mkono wa sweta baadhi ya wazee wenye umri mkubwa wamekuwa wakiongozana na watoto hadi hosipitalini wakidai wanawapeleka vijana wao kutahiri lakini wakishafika ndani kwenye eneo la upasuaji mdogo wao wenyewe ndiyo wanaanza kuvua suruali ili wapate huduma!
katika mijadala mbalimbali iliyoendeshwa katika warsha hiyo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni umuhimu wa kuhamamasisha wananchi wanaoishi na vvu kujiunga na vikundi vya waVIU vijijini ili waweze kunufaika na fulsa zinazotolewa na serikali za mitaa pamoja na program za UKIMWI wilayani.
No comments:
Post a Comment