




Hali hiyo ilijitokeza baada ya madiwani kupitia kamati zao kuanza kulalamika hatua iliyofikiwa ya kuzuiwa kwenda kukagua miradi wakiwa kwenye kamati zao na badala yake kupewa maelezo kuwa kuna waraka unaozuia kamati hizo kutokana na kukosekana ufanisi!
Ndipo miongozo mwenyekiti, azimio na maneno mengine ilipoanza kusikika, lakini mwishowe ikawa ngumu kurudisha wwaraka huo TAMISEMI na badala yake madiwani kukubaliana nao kwa shingo upande
Hatua hiyo ilifikiwa\ baada ya ufafanuzi kutolewa kuwa kimsingi serikali za mitaa pamoja na kuwa ni muhimili muhimu katika kuunganisha wananchi na kuleta maendeleo haimaanishi kuwa serikali kuu haina nguvu ya kuelekeza jambo mbele ya serikali za mitaa.
Na kwamba kwa kutambua hilo ndiyo sababu halmashauri kwa sehemu kubwa kama siyo asilimia 95% hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu, hivyo pale inapoagizwa baadhi ya mabadiliko ngazi za chini hakuna lugha ya kuyapamba maelekezo hayo bali kuyatekeleza
Ndipo diwani mmoja akasimama na kuomba mwongozo kisha akachomekea na azimio! hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo akatoa ufafanuzi kuwa serikali haiwezi kuazimiwa kwakuwa baraza hilo limeundwa pia kutokana na maelekezo na miongozo kutoka juu hivyo waheshimiwa wawe wapole kwanza!
katika hatua nyingine suala la uanzishwaji wa benki ya wananchi ya Mbozi leo limeendelea kupigwa dana dana ya kukubaliana kuto kubaliana! baada ya madiwani kuunga mkono kuanzishwa kwa benki hilo lakini wakitaka wananchi waleweshwe pole pole na pia wapate ziara ya kwenda kujifunza mikoa mingine namna ya benki hizo zinavyofanya kazi
Katika hali inayoonyesha kuwa wimbi hilo lilishawekwa mapema, kila aliyenyanyuka alikuwa akiongezea misumali ya kuzuia kuharakishwa kuchangisha shilingi 200 kwa kilo ya kahawa kwaajili ya uanzishaji wa benki hiyo ambapo baada ya maelezo ya ufafanuzi ya mkurugenzi mtendaji wilaya ya MBOZI, bado suala hilo liliamuliwa kwa kutakiwa kwanza wapewe ziara na baadaye wananchi waelimishwe namna bora ya kushiriki uanzishaji wa benki hiyo.
indabaafrica blog
No comments:
Post a Comment