Friday, July 5, 2013

USIKU WA BI KIDUDE WAJA

bi kidude kuenziwa ziff,
usiku wa bikidude,
usiku wa wanawake ziff,
jukwaa la wanawake

Na Andrew Chale, Zanzibar

WANAMUZIKI Nguli nchini wakiongozwa na Sit bin Saad ambaye ni mjukuu wa marehemu Bi.Kidude,Synerg,Baby J wote hawa ni kutoka Zanzibar Linah na THT Band kutoka Dar es Salaam kesho watawasha moto ndani ya mabo klabu kwa ajili ya kumuenzi marehemu Bi.Kidude ambaye aliwahi kutumbuiza katika matamasha ya ZIFF yaliyowahi kufanyika.


Tamasha la filamu la nchi za Jahazi maarufu kama ZIFF linaendelea kupamba moto na kesho ni usiku maalumu wa wanawake katika kumuenzi marehemu Bi.Kidude katika tamasha hilo.

Tamasha hilo ambalo lina siku ya 5 tangu kuanza kwake limekuwa ni kivutio kikubwa kwa wakazi na wageni kutoka kila kona ya dunia kuwapa burudani kulingana na mahitaji.

Usiku wa wanawake unatarajia kufanyika jioni ya leo ndani ya Mambo klabu ampapo wasanii watakao tumbuiza katika tamasha hio watakuwa ni wanawake pekee ambapo mjukuu wa marehemu Bi.KIdude atafungua dimba kutoa burudani hiyo.

Wanawake wameombwa kuhudhuria kwa wingi kwakuwa tamasha la siku ya leo ni kwa ajili ya wanawake.

katika tamasha hilo la usiku wa wanawake wasanii hao wataweza kukonga nyoyo za mashabiki wake na kufanya kufana kwa tamasha hilo ambalo linamkumbuka Bi.kidude kwa mchango wake ambao alikuwa akiutoa katika kipindi chake chote cha uhai wake.

Hata hivyo burudani hiyo itaambatana na kuonyeshwa kwa filamu mbili tofauti ikiwemo ya The Last Fishing Boat kutoka Malawi na Lilet never Happened kutoka Netherland.

No comments:

Post a Comment