Friday, July 5, 2013

VIONGOZI MBALIMBALI WATEMBELEA KATIKA BANDA LA VETA NA KUJIONEA SHUGHULI MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA NA CHUO HICHO.


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi wakati alipotembelea katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa VETA Idrisa Mshoro (katikati)akipewa maelezo na Alfan Ngowo juu ya Teknolojia za ukusanyaji wa taarifa za ardhi na mazingira wakati alipotembelea katika banda la VETA lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.kulia niMkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi na Makamu Mwenyekiti wa Maonesho wa VETA Abduri Mollel.

Baadhi ya wanafunzi waliofika katika banda la VETA wakipata maelezo kutoka kwa Theopista Michael ambaye ni mwanafunzi wa chuo VETA cha Njiro Arusha kinachotoa mafunzo ya Diploma ya mambo ya hoteli na utalii.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipewa maelezo na Mwalimu wa VETA Tabora Diana Mlengeki juu ya mashine ya useketaji wa nguo aina mbalimbali zitokanazo na nyunzi wakati alipofika katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali zinazotplewa na Chuo hicho katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa VETA Idrisa Mshoro (katikati)akimsikiliza Mkufunzi wa madereva Anthony Gaspar wakati alipokuwa akimuelezea njinsi ya madereva wanavyoweza kuzuia ajari baada ya kupewa mafunzo wakati alipotembelea katika banda la VETA lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.kulia niMkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Moshi na Makamu Mwenyekiti wa Maonesho wa VETA Abduri Mollel
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Eric Shitindi akimsikiliza Linda Njenje ambaye ni mwanafunzi mwenye mahitaji maalumu anayesoma katika chuo cha VETA kwa walemavu kirichopo Usariva Arusha,akitoa maelezo juu ya mafunzo wanaoyoyapata katika chuo hicho wakati alipotembelea katika banda lao lililopo kwenye maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira Eric Shitindi akimsikiliza mwalimu wa VETA Tabora Diana Mlengeki juu ya mashine ya useketaji wa nguo aina mbalimbali zitokanazo na nyunzi wakati alipofika katika banda la VETA kujionea shughuli mbalimbali,zinazoonyeshwa kwenye maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
aji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania Mh.Fakih Jundu (katikati)akimsikiliza mwalimu wa VETA Morogoro Sophia Tuka wakati alipokuwa akimuelezea juu yautengenezaji wa alama za barabarani ,zilizotengenezwa na wanafunzi wa VETA,Kulia niniMkurugenzi Mkuu wa VETA mhandisi Zebadiah Mosh na Kushoto niMsajili wa Mahaka Kuu Benedict Mwingwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa VETA Idrisa Mshoro (Kushoto)akimsikiliza mwalimu wa VETA Marthine Choma akimuelezea mafunzo ya nayotolewa na chuo hicho wakati alipotembelea katika banda la VETA lililopo katika maonesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment