Maamuzi ya kuyahamishia makao makuu kuwa Dodoma nadhani yalikuwa ni ya kimsingi kabisa ingawa utekelezaji wake haukuwa mzuri. Mpaka wa leo Watanzania tulio wengi bado hatuelewi tofauti kati ya Dar es Salaam na Dodoma hasa ukizingatia kwamba bado shughuli nyingi za kiserikali bado zinafanyikia Dar. Kwa wengine Dodoma inahusiswa na chama tawala (CCM), na si makao makuu ya serikali yetu. Hivi ndio kusema kwamba inabidi Ikulu ihamie Chamwino ndipo serikali yote itahamia Dodoma?
No comments:
Post a Comment