Big Boss wa band ya Twanga pepeta kwa mara ya kwanza toka huu mwezi uanze leo ameongea kwa mara ya kwanza na AMPLIFAYA, huwa hapendi sana kuzungumza lakini ukimuona kafanya hivyo ujue kuna sababu nyuma yake.
Alichokifanya leo ni kufichua siri ambayo ameshindwa kuivumulia, ni kutokana na ishu ya kuchukuliwa wanamuziki wake toka na kupelekwa Mashujaa Musica.
Siri anayoamua kuitangaza leo ni kwamba baadhi ya wanamuziki wake waliochukuliwa na Mashuja Band wamefukuzwa mashujaa na sasa wameomba kurudisha makazi Twanga Pepeta.
Asha amesema jumla ya wanamuziki waliofukuzwa Mashujaa anasikia ni 11, waliotaka kurudi Twanga ni watano akiwemo repa Mirinda Nyeusi ambae aliletwa Tanzania na yeye Asha kutoka South Afrika na kafukuzwa Mashujaa kisa alikwenda kumsalimia Asha.
Kwenye sentensi nyingine Asha amesema “kikubwa zaidi ni kwamba naongezewa mzigo kama wanavyoniita mama wa wasanii wa muziki wa dance, wanamuziki wanachukuliwa kwangu kwa kurubuniwa kwa pesa nyingi lakini sio kwamba wamependa na kwa sababu umri wao ni mdogo huwa wanadanganyika wanapotanguliziwa pesa mbele..
Kuhusu kuwapa nafasi tena baada ya kuomba kurudi, Asha amesema “ndio tunataka tuwajadili kwa sababu leo bahati mbaya ni siku ya kazi sijakaa na kebineti ya Twanga kwa hiyo sijajua lakini baadhi ya wanamuziki wako pale ofisini na sasa hivi nimewaacha pale wanaomba msaada, hebu fikiria wameachishwa kazi ghafla, wameachishwa kazi jana hebu fikiria watakwenda wapi?
No comments:
Post a Comment