Tuesday, July 31, 2012

TAMKO LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)KUHUSU KUFUNGIWA KWA GAZETI LA MWANAHALISI



 

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinalaani uamuzi wa Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulifungia kwa muda usiojulikana gazeti la MwanaHalisi kwa kutumia mwanya wa sheria mbovu ya magazeti inayokwenda kinyume na haki za binadamu na utawala bora.

CHADEMA kinaitaka Serikali kulifungulia gazeti hilo haraka iwekanavyo na kimewasiliana na Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA kuchukua hatua za kibunge kuisimamia Serikali  kurekebisha udhaifu huo ikiwa inaheshimu uhuru wa habari na inazingatia maslahi ya taifa.

CHADEMA kinatafsiri hatua hiyo ya Serikali ya kufungia gazeti la MwanaHalisi kuwa ni sawa na kufungia uhuru wa kusambaza habari, uhuru wa kupokea habari na uhuru wa kutoa maoni, hivyo tunatoa mwito kwa wananchi na wadau wote wa habari kuungana pamoja kupinga hatua hiyo, na CHADEMA kitaeleza hatua za ziada za kuchukuliwa iwapo Serikali haitasikiliza kauli za wadau wa habari juu ya suala hili.

CHADEMA kinatambua kuwa uamuzi wa Serikali kufungia gazeti hilo kwa mara nyingine tena ni kwenda kinyume na haki za binadamu, kinyume na utawala bora na ni kikwazo kwa demokrasia na maendeleo nchini.

CHADEMA kinapinga hatua ya Serikali ambayo viongozi na watendaji wake wakiwa wametajwa kama watuhumiwa katika habari zilizoandikwa na gazeti hilo imetumia mamlaka haramu ya Waziri mwenye dhamana ya sekta ya habari kugeuka mlalamikaji, mwendesha mashtaka na mfungaji huku ikipuuza taasisi za kusimamia uwajibikaji na haki.

MCHAKATO WA KUTOA MAONI YA KATIBA MPYA MKOA WA KUSINI PEMBA

Khamis Said Abdalla (47), mkazi wa Shehia ya Madungu, Wilaya ya Chakechake, Mkoa wa Kusini Pemba, ambae ni mlemavu, akitoa maoni yake kuhusu Katiba mpya katika mkutano wa kutoa maoni kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba mpya wakati wa mkutano huo uliofanyika katika Shehia hiyo hivi karibuni. Picha na Othman Maulid

SINGLE BUTTON VIBUNDUKI SHORTS....

 

WE NI MSICHANA WA KILEO NA MWENYE KUTAKA KUNG'AA WAKATI UKIWA MTAANI?? SIO LAZIMA JEANS.. KUNA KITU KINAITWA VIDUNDUKI... MARTIN KADINDA ANAKWAMBIA UTAKUWAJE SALAMA KAMA HUNA KIBUNDUKI KABATINI KWAKO??? 

PICHA NA MATUKIO KATIKA PITA PITA YA CAMERA YA FUNDI WA KOMBO

 Chicago down town inavyoonekana kwambali kupitia lake Michigan, unaweza kufikiria ni bahari him kumbe ni ziwa mambo ya Fundi wa Kombo hayo.

 Wakazi Wassira Kushoto na Dulla Solo wakipeana challenge ya mistari ya hip pop Wakazi ni mwanamuziki kizazi kipya and Dulla Solo ni Tanzania hip pop legend.

 Dulla Solo akiwa na Stanboi aka the Afican Child, Stanboi  mwanamuzik wa kizazi wa r&b na kwa sasa anatamba na kibao chake cha feel good akipata ukodak na legend wa hip pop

Stanboi na nembo ya Tshirt zake zinazo julikana kama the African child akiwa na watu walio walionunua kutoka kwake.

Ukodak wa Fundi wa Kombo watu wakishow love mwanzo kushoto mdau wa Chicago kati ni Stanboi kutoka    Wichita Ks na Dr Kally kutoka Detroit MI Dr Kally ni jina la kisanihi nae licha ya kufanya kazi za kuajiliwa pia ujiusisha na muzik wa hip pop pale anavyo pata muda.

Pita pita ya camera ya Fundi wa Kombo  ikakuta parking hii hipo full na vyombo vya majini katika lake Michigani Chicago..........kama unavyo jionea.

Dkt Migiro akutana na Jaji Warioba leo

 

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt.Asha-Rose Migiro (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko yaKatiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba wakati Dkt. Migiro alipotembelea ofisi zaTume jijini Dar es Salaam leo (Julai 31, 2012). (Picha na Ismail Ngayonga).

SALAMA JABIL MAHOJIANO NA AL HAJ ISMAIL RAGE NA MKASI TV

     Mkasi - SO3E11 with Rage  

     

HII KALI YA LEO

Hii Nayo Kali...!


KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

 

 Naibu Waziri wa Afya Dkt. Seif Rashid (kulia) akibadilishana mawazo na Wabunge wa viti maalum Zarina Madabida (kushoto) na Zainab Vullu (katikati) katika viwanja vya Bunge  mjini Dodoma leo. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO.


  Mbunge wa Simanjiro,  Christopher Ole Sendeka, (kushoto) akibadilishana mawazo na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, leo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

   Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI-ELIMU)  Majaliwa Kassim Majaliwa, akijibu  hoja zinazohusu wizara yake Bungeni, mjini Dodoma leo.


1    Mbunge wa Monduli, Edward Lowasa  (kushoto) na Mbunge wa Viti Maalum, Diana Chilolo, wakifuatilia taarifa za Bunge wakati wakiwa katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, leo.

HASIRA ZA MKIZI FURAHA KWA MVUVI' NGASA SASA KUUZWA M 80

 


KLABU ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam, imetangaza katika ukurasa wake wa Facebook kumuuza mshambuliaji mahiri wa timu hiyo aliyejiunganao kwa dau kubwa akitokea Klabu ya Yanga, Mrisho Ngasa kwa dau la Dola za Kimarekani 50,000, ambazo ni sawa na Sh. milioni 80  za kitanzania.


Uongozi wa Klabu hiyo umeweka wazi kuwa umekasirishwa na kitendo cha mkali huyo kuonyesha mapenzi ya wazi kwa kuibusu Jezi ya Klabu yake ya zamani Yanga baada ya kuifungia timu yake bao lililoiwezesha kuipeleka timu hiyo hatua ya Fainali za Kombe la Kagame dhidi ya timu hiyo na AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, wakati akishangili bao lake mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga.


Katika Mchezo huo Azam iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutinga hatua ya Fainali katika michuano hiyo, ambapo ilikutana na Yanga katika Fainali hizo mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo Ngasa, aliingia akitokea benchi katika dakika za mwisho za mchezo huo.


Azam imeonyesha kukasirishwa na kitendo hicho cha Ngasa na kukielezea kuwa hakikua sahihi, ambapo awali uongozi huo ulikaliliwa kuwa ulikichukulia kitendo hicho kama tukio la kimichezo zaidi kutokana na mchezaji huyo kuwa alifanya hivyo huku akiwa tayari ametimiza majukumu yake ya uwanjani na kuwafungia bao muhimu katika mashindano hayo, na kuongeza kuwa hawakuona vibaya kwa Ngasa kuonyesha furaha yake kwa kushangilia kwa staili yake aipendayo.


Lakini sasa Uongozi huo umekuwa na kauli tofauti kuhusu tukio hilo ambapo sasa kama walivyojieleza katika mtandao wao wa Facebook, kuwa wamekasirishwa na kitendo hicho kilichoonyeshwa na Ngasa.


Aidha Uongozi huo umesema kuwa upo tayari kupokea ofa yeyote kutoka kwa timu yeyote iwe ya ndani ya nchi au nje ya nchi kwa dau hilo walilolitaja. 


Uongozi huo ukionyesha hisia zake juu ya kukasirishwa huko, umeeleza kuwa mara kadhaa umemshuhudia Ngasa, akitinga katika Jengo la Klabu ya Yanga, kuwafuata rafiki zake Jerry Tegete, Hamis Kiiza na Niyonzima.


Mrisho Ngasa (kulia) akipozi kwa picha na Haruna Niyonzima, baada ya mchezo wa fainali za Kombe la Kagame uliozikutanisha timu zao jumamosi iliyopita, na Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kutwaa Kombe la Kagame 2012 kwa mara ya pili mfululizo.

MATUKIO YA MGOMO WA WALIMU LEO WANAFUNZI WAANDAMANA KUWAPINGA

 

   Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi za jijini Dar es Salaam, Morogoro na Singida, wakiandamana leo asubuhi kupinga hatua ya walimu kugoma kuingia madarasani kufundisha jambo ambalo wanafunzi hao wamelielezea kuwa ni kunyimwa haki zaoza msingi kuwakosesha masomo, ambapo nao wamepanga kutinga Mahakamani kuwafungulia kesi walimu wao kutokana na kwamba madai wanayoidai Serikali wao hayawahusu na hawahusiki kwa mamna yeyote ile, alisikika mmoja wa viongozi wa wanafunzi hao aliyejitambulisha kwa jinala Shaban Mudunda.

 DAR:- Wananfunzi wa Shule ya Msingi Mbezi ya Jijini Dar es Salaam, nao hawakuwa nyuma katika kudai haki yao ambapo nao walifikisha ujumbe kwa njia hii ya Bango, wakiwa pembezoni mwa barabara Morogoro leo asubuhi.

 Nako Mkoani Singida wanafunzi walijitokeza kwa wingi katika mitaa ya mji huo huku wakiimba na wakiwa na baadhi ya Mabango yenye ujumbe kuhusu tukio hilo la kugoma kwa walimu.

 Hawa ni Wanafunzi wa shule za msingi za Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani ktk Manispaa Singida, wakiwa nje ya Ofisi za Mkuu wa mkoa huo leo asubuhi, ili kumfikishia ujumbe baada ya walimu wao kugoma.

Wakati walimu wakigoma kuingia madarasani leo asubuhi na wanafunzi wengine kushika mabango na kuandama ili kufikisha ujumbe wa kudai hazi zao, ilikuwa ni tofauti kwa wanafunzi hawa wa Shule ya Msingi Yeta, ambao wao waliamua kuwaonyesha walimu wao kuwa hata wao wanaweza ambao wanafunzi wa Darasa la Saba waliamua kujitolea na kutinga madarasa ya chini na kushusha Nondoz kwa wadogo zao. 

Na katika Shule ya Msingi Lugalo, leo baada ya walimu kugoma wanafunzi wa shule hiyo, walifundishwa na Ma MP pamoja na wanafunzi wa Darasa la saba walifanya kama ambavyo wamefanya wanafunzi wa Yeta amapo wao pia wamejitolea kuwafundisha wadogo zao wa madarasa ya chini.




Na: Elisante John Singida.
MGOMO Uliondaliwa Chama cha walimu CWT nchini, umeleta madhara katika Manispaa Singida, baada ya wanafunzi wa shule za msingi kuandamana hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa leo asubuhi.

Kwenye maandamano hayo, watoto wa shule za msingi Nyerere, Singidani, Ipembe na Unyankindi, waliamua kutembea umbali wa kilomita tatu hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa, wakiwa na mabango yenye ujumbe mbalimbali huku barabarani wakiimba '‘tunataka haki zetu, walimu wamegoma, tunataka haki zetu'’.

Baada ya askari polisi kubaini usalama wa watoto hao upo hatarini, waliingilia kati na kuongoza maandamano hayo hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa kwa amani.

HAKI SAWA KWA WOTE SI NDO KAMA HIVI, AU VIPI WADAU!!!!

 

Hapa hapa ile kaulimbu ya kina mama kudai haki sawa na kina baba si ndiyi sawa,? namna hii nadhani hata uchumi wa Taifa hili utapanda kwa kasi ya ajabu.

Saturday, July 28, 2012

RAIS KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO LA TATU LA JUKWAA LA UHUSIANO WA CHINA NA AFRICA KATIKA KUPUNGUZA UMASKINI



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam  Julai 28, 2012. Wa tatu toka kushoto ni Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian, wa pili kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya rais Mhe Steven Wassira, wa pili  kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Uchumi wa Sierra Leone Mhe Momodu Kargbo, kushoto ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango  Mipango Dkt Philip Mpango na kulia kabisa ni Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha na ujumbe toka China unaohudhruia  Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza  Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian (kushoto) na  Balozi wa China hapa nchini Mhe L.V. Youqing. baada ya  akifungua Kongamano la tatu la Jukwaa la Uhusiano wa China na Bara la Afrika katika kuondoa umaskini katika hoteli ya White Sands jijini Dar.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika mazungumzo rasmi na Waziri wa China anayeshughulikia Umaskini Mhe Fan Xiaojian. PICHA NA IKULU

THE OPENING CEREMONY OF THE LONDON 2012 OLYMPIC GAMES.


Tanzania

Jamaica

Brazil's flag bearer Rodrigo Pessoa holds the national flag as he leads the contingent in the athletes parade during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games

Flag bearer Mariel Zagunis of the U.S. holds the national flag as she leads the contingent in the athletes parade during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium

Members of Cameroon's contingent take part in the athletes parade during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games

Members of the Canadian Olympic team take part in the athletes parade during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games

Saudi Arabia's contingent takes part in the athletes parade during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games

The Olympic flag is carried during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium

Britain's David Beckham (C) drives a powerboat with the Olympic torch as fireworks are launched over Tower Bridge during the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games

 Basketball star LeBron James (L) takes pictures with his phone as he walks with the United States delegation in the athlete's parade in the opening ceremony of the London 2012 Olympic Games at the Olympic Stadium