Wednesday, July 31, 2013

"WAPIGWE TU" YA MIZENGO PINDA ITAMFIKISHA KORTINI

KAULI ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ya kubariki vyombo vya dola kuendeleza kipigo kwa raia wanaokaidi amri imechukua sura mpya baada ya Kituo cha Sheria na Haki za Bindamu (LHRC) kutangaza kumburuza mahakamani wiki hii kutokana na kushindwa kufuta kauli yake.
Juni 20, mwaka huu, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo bungeni, Waziri Mkuu, Pinda, alivitaka vyombo vya dola kuendelea kuwapiga raia, akisema kuwa hakuna namna nyingine kwani serikali imechoka.
Kauli hiyo imekuwa ikipingwa na wananchi, mashirika ya kutetea haki za binadamu na wanasiasa wakimtaka Waziri Mkuu, Pinda, kuifuta kwa kuomba radhi, wakidai kuwa inachochea uvunjifu wa sheria.
Akitangaza kusudio la kituo hicho kufungua kesi dhidi ya Pinda, Mkurugenzi wa maboresho na utetezi, Harold Sungusia, alisema hadi jana walikuwa tayari wameandaa kusudio la shtaka lao.
Alisema kuwa kisheria kilichowafanya kufikia uamuzi huo ni kutokana na waziri mkuu huyo kukiuka Katiba ya nchi inayozungumzia usawa mbele ya sheria.
“Kitendo alichofanya waziri mkuu cha kuwaruhusu polisi kupiga wananchi hakikubaliki hata kidogo na walitegemea kwamba angeomba radhi kutokana na kauli yake hiyo tangu alivyoshinikizwa kufanya hivyo na makundi mbalimbali.
“Badala yake ameendelea kuwa kimya licha ya mkubwa wake, Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni kukiri kwamba mtendaji wake huyo aliteleza,” alisema.
Sungusia aliongeza kuwa Alhamisi wiki hii wataweka bayana kwa waandishi wa habari ni wapi kesi hiyo itafunguliwa.
Pinda alitoa kauli hiyo tata ambayo imehojiwa na wengi wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) aliyehoji kama serikali iko tayari kutoa tamko kuhusu vurugu zilizotokea jijini Arusha, Mtwara na maeneo mengine pamoja na hatua ya vyombo vya dola kutumia nguvu.
Katika majibu yake Pinda alisema kuwa suala la amani linawagusa wote, kwamba jukumu ni kwa viongozi wa kisiasa. Alifafanua kuwa kama viongozi wa kisiasa hawatafika mahali wakakubaliana bila kujali vyama vyao nchi itafika pabaya.
Pinda alifafanua kuwa kwa upande wa serikali lazima wahakikishe kwamba wale wote wanaojaribu kuvunja amani kwa namna yoyote ile kazi waliyonayo ni kupambana kweli kweli kwa njia zozote zinazostahili.
“Mimi naomba sana Watanzania, maana kila juhudi zinazoonekana zinaelekea huko, tunapata watu wengine wanajitokeza kuwa mara unajua…unajua. Acheni serikali itimize wajibu wake, kwa sababu jambo hili ni la msingi na wote tulilinde kwa nguvu zetu zote.
“Mheshimiwa Mangungu umeanza vizuri lakini hapa unasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo unaambiwa usifanye hiki, ukaamua wewe kukaidi, utapigwa tu,” alisema.
Waziri mkuu aliongeza kuwa hakuna namna nyingine, maana lazima watu wakubaliane na serikali kwamba nchi hii wanaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki, unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ni jeuri zaidi, watakupiga tu, na mimi nasema wapigwe tu, maana hakuna namna nyingine, tumechoka,” alisema

Tanzania Daima

CHADEMA HAINA UBAVU WA KUMKATAA TENDWA

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakina ubavu wa kumkataa au kutomtambua John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Msajili wa Vyama vya Siasai, Rajab Baraka alipozungumza na MTANZANIA kuhusu kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa aliyedai chama hicho hakimtambui John Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa.

Katika madai yake Dk. Slaa alidai Tendwa anakipendelea CCM katika kutoa haki ya demokrasia na hatendi haki kama mlezi wa vyama vyote vya siasa nchini.

Dk. Slaa alisema hayo wiki iliyopita alipokuwa akizungumza na waandishi wa Habari na kusisitiza hata katika barua zao za mawasiliano kwenda kwa ofisi ya msajili chama hicho hakitumii jina la John Tendwa.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa, Chadema kinaitambua ofisi ya Msajili wa Vyama tu lakini hakimtambui Tendwa kuwa ndiye msajili wa vyama vya siasa nchini.

“Hatumpelekei hata barua huyu hatunzi sheria siyo mtu wa kulea vyama ni mlezi wa chama kimoja, hayuko serious na hatushirikiani naye mpaka aondoke madarakani.

“Tukiandika barua hatuweki jina lake lakini tunaitambua ofisi yake, hata yeye mwenyewe analijua hilo na akijibu barua zetu haweki jina lake,” alidai Dk. Slaa.

Akijibu hoja hizo, Naibu Msajili alisema Chadema hawana ubavu wa kutomtambua Tendwa kwa sababu amewekwa kisheria na ofisi yake ipo kisheria.

Alisisitiza Tendwa ataendelea kuwa mlezi wa vyama vyote na siyo chama kimoja kama inavyodaiwa na kuvitaka vyama vyote kuheshimu sheria iliyomuweka madarakani msajili huyo.

Mtanzania.

BODI YA MIKOPO YAKANUSHA UVUMI KUWA WALIOOMBA MKOPO WA ELIMU WANAPASWA KUJIANDIKISHA UPYA


Kumekuwa na uvumi kwamba mtandao wa uombaji mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (OLAS) ulikuwa na hitilafu ya kiufundi na hivyo Wanafunzi wanaondelea na masomo ambao walikuwa tayari wameshahakiki taarifa zao wanapaswa kurejea kujaza upya ama kuhakiki iwapo taarifa zao zipo mtandaoni.

Bodi inatumia fursa hii kuwajulisha Wanafunzi husika, Vyuo vya Elimu ya Juu na Umma kwa ujumla kuwa taarifa za Wanafunzi hao zilizopokelewa ziko salama na hawapaswi kujaza tena na hivyo taarifa hizo za uvumi zipuuzwe.

Aidha Bodi inasisitiza kwamba kesho tarehe 31 Julai, 2013 ni

mwisho wa kupokea maombi ya mikopo ya waombaji wote wanaotarajia kujiunga na Vyuo vya Elimu ya Juu kwa mwaka wa masomo 2013/2014 na wale wanaoendelea na masomo na kwamba hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya tarehe hiyo kupita.

Bodi inawapa nafasi ya mwisho waombaji wapya na wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao hawajaomba mikopo kwa njia ya mtandao, kuhakikisha wanatumia muda uliobaki kukamilisha taratibu zote za maombi kupitia anuani ifuatayo: http://olas.heslb.go.tz au kupitia tovuti: www.heslb.go.tz

Tangazo hili limetolewa na:

Mkurugenzi Mtendaji

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU.

PICHA ZA UCHI ZANASWA KATIKA UKUMBI WA KANISA JIJINI DAR

Kiongozi wa Kanisa la Greek Orthodox duniani, Papa Theodor’s II ameamuru kufungwa kwa ukumbi uliopo ndani ya eneo la kanisa hilo lililopo Kiwanja Namba 7509 katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jijini Dar es Salaam kufuatia kuwepo kwa picha za utupu za wanawake ukutani..
Papa huyo alifikia uamuzi huo Februari 19, mwaka huu baada ya kutua nchini ambapo alifanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete.
Mbali na mazungumzo na JK, alipata nafasi ya kutembelea ukumbi huo ulio kwenye eneo la kanisa hilo ndipo ‘alikutana’ na picha za wanawake wa Kiafrika na Kizungu zikiwa zimetundikwa ukutani wakiwa kama walivyozaliwa.



Mbali na picha hizo za utupu, pia kulikuwa na picha ya mwanamitindo maarufu Bongo, Mariam Julius Odemba. Picha yake ilimwonesha akiwa amevaa nguo ya heshima na maandishi juu ya picha yakiwa yameandikwa; ‘Thanks British Legion for all your support. Miriam Odemba, 1st Oct 1999’. 

Imeelezwa kuwa baada ya kutua nchini, papa huyo alilala katika nyumba iliyo karibu na kanisa na klabu hiyo na usiku wakati akisali alishangaa kuwaona wanaume, tena wenye mwonekano mzuri wakiingia katika eneo hilo la kanisa akasitisha sala.

Kilichomshangaza zaidi ni kuwaona wanaume hao wakiwa na wasichana wabichi na baada ya kufika klabuni walikuwa wakipiga kelele huku muziki ukisikika kwa sauti ya juu.
Kufuatia hali hiyo, aligundua kwamba watu hao walikuwa wakinywa pombe hadi usiku wa manane jambo ambalo ni kinyume na maadili ya imani hiyo. 
“Kesho yake Papa Theodor’s aliamua kutembelea ndani ya klabu hiyo ndipo aliposhuhudia picha hizo chafu nyingi zikiwa zimetundikwa ukutani na chupa tupu za vinywaji vikali.

“Kuona hivyo papa alimuagiza kiongozi wa Bodi ya Wadhamini wa Kanisa, Dimitri Kimon akutane na mapadri wote mwezi wa nne (uliopita) na kujadili hilo nia ikiwa ni kurejesha usafi na kuondoa uchafu huo kanisani hapo.

“Katika mkutano huo waliamua kufunga na kuomba kisha kumtafuta wakili ili aweze kuwatoa waliokuwa wakiendesha ukumbi huo,” kilisema chanzo.

Chanzo kiliongeza kuwa, Julai 8, mwaka huu viongozi hao waliamua kufunga geti la kanisa hilo na kuimarisha ulinzi kwa kutumia kampuni ya ulinzi ili kuzuia wanachama wa klabu hiyo kuingia eneo hilo isipokuwa waumini.
Kiongozi wa kanisa hilo.

Habari zinasema viongozi wa kanisa hilo waliwaambia waliokuwa wakiendesha ukumbi huo kwamba kiongozi wao mkuu hakupendezwa na picha chafu za ukutani na alihoji endapo dini nyingine zikigundua uchafu huo wataelewekaje kwa jamii? 

Kuna madai kwamba wengi waliokuwa wakiingia kwenye ukumbi huo ni vigogo katika ngazi ya mawaziri na wabunge ambapo waandishi wetu walibahatika kuona jina la mbunge mmoja likiwa limeorodheshwa katika kitabu cha waliokuwa wakiingia. 

Mwanachama mmoja wa klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa kwa madai kuwa si msemaji, alisema wanakusudia kufungua kesi mahakamani ili kupinga adhabu ya kufungwa ukumbi huo kwa kuwa wapo eneo hilo kwa muda mrefu.

“Sisi tupo katika eneo hili na tumefanya shughuli zetu siku zote hizo, tunashangaa leo kuona kanisa linatufungia geti. Ni lazima tutachukua hatua za kisheria,” alisema mwanachama huyo.

Mwandishi wetu alimpata wakili wa kanisa hilo ambaye pia ni Katibu Myeka, Edward Chuwa alipoulizwa kuhusu mgogoro huo alikiri kuwepo.

“Ni kweli kuna huo mgogoro kati ya kanisa na waendesha klabu hiyo lakini kwa kuwa mimi ni wakili naomba nisiseme chochote kwa sababu za kimaadili,” alisema Chuwa.

Naye wakili wa waendesha klabu hiyo, Evodi Mmanda alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu mgogoro huo naye alikiri kuwepo.

“Mgogoro huo naujua lakini kwa kuwa mimi ni wakili wao siwezi kusema chochote kutokana na maadili ya kazi yangu.” alisema Mmanda bila kusema ni lini kesi hiyo itasikilizwa. 

Credit : Uwazi via GPL

SEREKALI YATANGAZA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KWENDA UALIMU

Serikali imetangaza majina ya wanafunzi 18,754 waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu vilivyo chini yake ikiwa ni ongezeko la wanafunzi 1,659 ikilinganishwa na 17,095 waliochaguliwa mwaka jana.

Kati ya wanafunzi hao, 11,806 wamechaguliwa kusomea ngazi ya cheti (Grade A) na 6,948 watasoma katika ngazi ya stashahada.

Wanafunzi 363 wamechaguliwa kusoma elimu maalumu kwa ngazi ya cheti huku 57 wakisoma elimu hiyo kwa ngazi ya stashahada.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu alisema wanafunzi wanatakiwa kuripoti kwenye vyuo walivyopangiwa kuanzia Agosti 15, mwaka huu.

“Usajili utafungwa Agosti 25 saa 12:00 jioni, ‘Joining instructions’ (fomu ya maelekezo ya kujiunga) zitatumwa kwa wahusika kupitia anuani zao.... fomu hizi pia zinapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,” alisema.

Taarifa ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliyotolewa baadaye jana ilisema kuwa wanafunzi waliochaguliwa wanatakiwa kufika vyuoni wakiwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na cha sita vinavyotolewa na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) , ada ya muhula wa kwanza Sh100,000 au Sh200,000 kwa mwaka.

Wanatakiwa kuwa na “Sare ya chuo kulingana na maelekezo ya chuo husika, fedha za tahadhari chuoni na matumizi binafsi,” inasema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inaeleza pia kuwa wakuu wa vyuo wanatakiwa kuhakikisha wanafunzi wanaosajiliwa ni wale waliopo kwenye orodha iliyotolewa na wizara na si vinginevyo.

Wengi wa wanafunzi hawa ni wale waliohitimu kidato cha nne mwaka 2012 na kidato cha sita mwaka huu. Kwa upande wa wale wa kidato cha nne, matokeo yaliyotangazwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi yalionyesha kuwa watahiniwa 159,609 wa shule walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la nne.

Inaonyesha pia kuwa kwa upande wa Tanzania Bara, wanafunzi 34,599 walifaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu na kati yake waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi walikuwa ni 34,213.

Kwa upande wa matokeo ya kidato cha sita mwaka huu, watahiniwa waliofaulu mtihani huo walikuwa ni 44,366 kati yao 40,242 wakiwa ni wa shule. Matokeo hayo yanaonyesha pia kuwa, watahiniwa 35,880 ndiyo waliofaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu.

Kwa mujibu wa Kitabu cha Takwimu cha Wizara ya Elimu (Best), mwaka 2012 wanafunzi 17,095 walichaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali vya ualimu nchini.
Kutokana na takwimu hizo, kuna uwezekano mkubwa kwamba wanaokwenda kusoma ngazi ya cheti wanatoka kwenye kundi la wanafunzi waliopata daraja la nne.

Wanafunzi waliopata daraja la nne kwenye mtihani wa kidato cha nne mwaka jana ni 124,260.

Baada ya kutangaza majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano pamoja na vyuo vya ufundi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo aliliambia gazeti hili kuwa wanafunzi waliopata daraja la nne katika kiwango cha alama 27 watachaguliwa kujiunga na vyuo vya ualimu endapo wataomba.

“Vigezo vya kujiunga na kidato cha tano na vile vya vyuo vya ualimu ni tofauti. Kidato cha tano mwisho anatakiwa mtu mwenye alama 25 na masomo yake matatu yawe sawa, ualimu ni alama 27.

“Mwanzoni walikuwa wanakwenda wenye alama 28, lakini mwaka jana tukasema hapana, iwe alama 27 na tutachukua kuanzia waliomaliza shule mwaka 2008 kama wataomba, kwa sasa hivi watu wanaendelea na kazi ya kuwachagua,” alisema Mulugo.

Kwa muda mrefu, wadau wa elimu wamekuwa wakipiga kelele kuhusu wanafunzi wanaochaguliwa kusomea ualimu nchini wakitaka nafasi hiyo ichukuliwe na wale wanaofanya vizuri kwenye masomo yao.

Monday, July 29, 2013

LADIES:JE WAJUA WANAUME WANAWEZA KUWEKWA KIGANJANI BILA WAGANGA?

Mbinu chache za kuwaweka waume zenu kiganjani.
Mpe mumeo anachohitaji :
Wanawake wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au night dress ndani huna kitu. Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia zake. Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue tayari mwenzako alishafiria mbali zamani we huna habari.
Ni vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za mwanaume huyo mumeo kama inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya hivyo unamwathiri kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje waliowaweka waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia. Akiwa na ahadi na mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?
NB:

UKOO WATISHIWA KUTEKETEZWA KWA USHIRIKINA HUKO TABORA


Watu watatu wa ukoo mmoja wameuawa kwa kukatwa mapanga kutokana na imani za kishirikina katika Wilaya ya Nzega Tabora, huku ujumbe mkali wa kuuawa kwa watu wengine ukiachwa katika Kijiji cha Nsanga.


Tukio hilo lilitokea katika kijiji hicho kilichopo Kata ya Ikindwa Nzega, Julai 25 mwaka huu, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Nzega Bituni Msangi alisema sababu ya mauaji hayo ni kukithiri kwa imani za kishirikina kwa baadhi ya wananchi wa kijiji hicho.



Aliwataja waliouawa kuwa ni Catherin Shija (65), Fransnc Kaliki (69) pamoja na Maria Kulwa (52) wote wakiwa ni wa ukoo mmoja wakiishi katika kijiji hicho.



Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho alisema watu wanaofanya mauaji hayo wanaishi nao, huku usiri mkubwa wa kuwataja kwenye vyombo vya dola ukiwa umetawala.



Alisema baada ya kuuawa vikongwe hao wa ukoo mmoja, waliotenda tukio hilo waliacha ujumbe mfupi wa barua katika kijiji hicho kuwa watu watatu wa kijiji hicho watauawa kwa kukatwakatwa mapanga muda wowote kuanzia sasa.



Ujumbe huo ulisema kuwa kutokana na watu hao kukaa mbali zoezi hilo limeshindikana kuuawa wote kwa pamoja na kuongeza kuwa ndani ya saa 24 watu hao watauawa.



Msangi akisoma ujumbe huo na kutaja majina yaliyokuwa yameandikwa kuwa ni Mwanamagazi, Mwanakizinga pamoja na mwanawe ambaye jina lake halikufahamika, wote wakiishi katika kijiji hicho wanatuhumiwa kwa ushirikina .



Aliwataka wananchi hao kutokuamini imani za kishirikina na macho mekundu kutokana na vikongwe wengi kufanya kazi za kijamii ikiwa ni pamoja na kutumia kuni za kupikia ambazo husababisha hali hiyo.


Alitaka doria za vitongoji kuimarishwa ikiwamo Sungusungu kulinda mazingira ya vijiji pamoja na kutambua watu wageni wanaoingia katika vijiji ili kuweza kupunguza mauaji hayo ya vikongwe.



Mkuu wa Polisi Wilaya, Yusuph Sarungi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa upelelezi mkali unaendelea wa kubaini wahalifu wa tukio hilo.

AGNESS MASOGANGE AFUTIWA DHAMANA YAKE NA KURUDISHWA RUMANDE

HUKU akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya

Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo,Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.

Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.


“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele. 






“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.



“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake. 


Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.

“Nyie si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo. 


Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.


Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande 

-GPL

WANAWAKE KUTEMBEA NUSU UCHI, KUMBE WANA LAO JAMBO

Kuna wakati wanaume hudhani kwamba, wanawake wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa wanaume. Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba, sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba pengo au udhaifu huo.

Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao. Hawa nao ni lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo. Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao, bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.

Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri. Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine kutongozwa.

MBUNGE WA CCM ANAYEDAIWA KUFADHILI MADAWA YA KULEVYA AJISALIMISHA POLISI

Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam kwa tiketi ya CCM, Iddi Azzan, aliyetajwa kwenye barua inayosadikiwa kuandikwa na wafungwa Wakitanzania waliopo Hong Kong “amejilisalimisha” kwenye ofisi za jeshi la polisi na kulitaka jeshi hilo lifanye uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizoelekezwa kwake, ili hatua nyingine na ikibidi sheria, vichukue mkondo wake.

Azzan amesema alienda mwenyewe kutoa taarifa katika Kituo Kikuu cha Polisi Kati, jijini Dar es Salaam.

"Nimeamua kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa ili ufanyike uchunguzi wa jambo hilo na ukweli ubainike na hatua za kisheria zifuate juu yangu," alisema Azzan kwa njia ya simu


"Mimi sipo juu ya sheria , itakapobainika najihusisha na tatizo hilo, nichukuliwe hatua mara moja, na nitajiuzulu ubunge wangu," alisisitiza Azzan na kuongeza:


 "Wapiga kura wangu wa Kinondoni pamoja na wananchi kwa ujumla inatakiwa waelewe kuwa barua hizo zina nia mbaya zenye lengo la kunichafua na kama kweli wana ushahidi wangetaja majina yao,"alinukuliwa Mbunge huyo.

CHANGUDOA APAWE KICHAPO NA WENZAKE KWA KUUZA MWILI WAKE KWA BEI YA CHINI

Kwa hali isiyo ya kawaida changudoa mmoja huko Naivasha Nairobi Alipewe kichapo cha mbwa mwizi Baada ya kugundulika na wenzake kuwa huwa anauza kwa bei ndogo na saa zingine huwa anatoa kwa mkopo..kitendo hicho kimelaaniwa na wenzake kwa vile kinapunguza bei yao na kuonekana kuwa si wa gharama...inafikia kipindi watu wanaokuja wanamtafuta yeye tu kwa vile ni wa bei ya chini .....
“Kwani unafikiria sisi tutakula wapi kama utaendelea kujiuza hii bei hasara" Alisikia Changudoa mmoja akisema huku akishusha kichapo...

Watu mbali mbali waliingilia kati na kuanza kumuokoa katika kichapo hicho...
Mteja mmoja alisikika akisema: 
“Unajua huyu mama huwa ananipatia kwa credit on a bad day so siwezi muacha auliwe na hawa wenzake (she offers me services on credit when I’m broke so I can’t let them kill her),”

CULTURE WARS MOVIE LAST SCENE

Bob and Monica 
Director Deo akitoa maelezo kwa backstage juu ya nini cha kufanya
Loctaion watunwajipanga....
Director Deo akitoa maelezonya mwisho kabla ya mambo kuanza kwa taswra zaidi za picha za location read more

Sunday, July 28, 2013

Mh. Dodest J. Mero akipata ukodak wa pamoja na familia yake

Mh. Dodest J. Mero akipata ukodak wa pamoja na familia yake. Mh. Mero alikuwa anafanya kazi Tanzania Mission New York katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo: 
Minister plenipotentiary at United Nations
Minister Plenipotentiary at Government of Tanzania
Partner at PM Consulting Group, na sasa amekuwa promoted na Mh. Rais kuwa 
Ambassador and Permanent Representative at Permanent Mission of United Republic of Tanzania to UN - Geneva. Kwahiyo viongozi wa jumuia ya watanzanani New York pamoja na Mh. Balozi Tuvako Manongi na wafanyakazi aliokuwa anafanya nao Office za Tanzania UN Mission New York walimwandalia BBQ ya Kumuaga na kumpa zawadi kama kumbukumbu na heshima kutokana na jinsi walivyo kuwa bega kwa bega katika utendaji wa kazi za kioffice na za kijamii kipindi yupo NYC.
H. E. Mr. Ken Kanda
Ambassador & Permanent Representative of
The Republic of Ghana to The United Nations
akipata ukodak na Mh. Mero na kushoto kwa Mh. Mero ni mke wake, anaefuatia ni mke wa Mh. Tuvako N. Manongi
Permanent Representative of the United Republic of Tanzania. Viongozi hao walipata ukodak kumbukumbu mbele ya Camera ya Vijimambo.
Mh. Balozi Manongi akimsomea maneno yaliyoandikwa kwenye zawadi kabla ya kumkadhi Mh. Mero
Makamu katibu wa New York Tanzania Community Mariam Abu akimkabidhi zawadi Mh. Mero kwa niaba ya Community.
Zawadi ziliendelea kama unavyoona
Mh. Balozi Manongi akiongea kabla ya kukabiz zawadi hiyo, Hafla hiyo ilifanyika nyumbani kwa Mh. Balozi Manongi Dobbs Ferry New York.
Ni zawadi picha kubwa ya ukutani yenye picha ya mama wa kiafrica.
Mh. Mero akiongoa na kutoa shukrani kwa watu waliojitokeza na pia kusema kuwa atawamiss sana wafanyakazi wenzie hasa kitu atakacho miss ni happy hour, Happy hour ni muda wa kukutana wafanyakazi wote kwa soft drink baada ya kazi za siku nzima.
Mwenyekiti wa New York Tanzania Community Mr Shaban Mseba akiongea machache kwa niaba ya Community. Kwa picha zaidi bofya read more

Saturday, July 27, 2013

TAKE ONE 2013 SEASON E14 C CLOUDSTV

MAMA SALMA KIKWETE AFUTURISHA VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI MKOANI LINDI

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa dini mbalimbali wa Lindi baada ya kuwaandalia futari nyumbani kwake hapo mjini Lindi jana.
Baadhi ya viongozi wa dini mbalimbali na serikali wa Lindi wakishiriki katika futari rasmi ilyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika makazi yake mjini Lindi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongea na viongozi wa dini mbalimbali wa Lindi baada ya kuwaandalia futari nyumbani kwake hapo mjini Lindi tarehe 25.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na baadhi ya akina mama walioshiriki futari aliyowaandalia nyumbani kwake mjini Lindi tarehe 25.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na baadhi ya akina mama walioshiriki futari aliyowaandalia nyumbani kwake mjini Lindi tarehe 25.7.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiaagana na baadhi ya akina mama walioshiriki futari aliyowaandalia nyumbani kwake mjini Lindi tarehe 25.7.2013.

Friday, July 26, 2013

Eti staa huyu wa Nollywood kasema hajakutana na mwanaume kimwili kwa miaka 10 sasa.


Kwenye zile stori za umbea kwa sasa huko Nigeria hii ni moja kati ya kubwa zake…

Mastaa wa kiwanda cha burudani mahali popote pale iwe ni Marekani au hapa nyumbani bongo wamekuwa na kawaida ya kujaribu kuhakikisha wanatafuta njia mbalimbali za ku-make headlines ambazo zitawafanya waweze kuendelea kuwa maarufu au kujipa promo kwa lengo flani.

Star wa Movie za Naija, Genevieve Nnaji ametoa kauli ambayo inaweza ikawa kali ya mwaka baada ya kuanika wazi kabisa siri zake za ndani za ishu za mapenzi yani.

Anakwambia hajawahi kufanya mapenzi kwa muda wa miaka kumi sasa hivi, amekuwa single kwa muda mrefu na kuna kipindi aliamua kuwekeza mawazo yake kwenye career au kazi yake ambayo ni kutengeneza filamu na ndio maana amekaa muda wote huo bila kufanya mapenzi.
Watu wengi watashangazwa na kauli hii kwa kuwa miaka si mingi staa huyu alikuwa akidaiwa ku-date na mwimbaji D’Banj ambapo anasema wakati anaingia kwenye uhusiano na mwimbaji huyo, D alisisitiza kuwa uhusiano huo sio wa muda mrefu na ndio maana wameachana.

Genevieve amewachanganya mashabiki wake kwa kauli nyingine yenye utata akizungumzia uhusiano wake na D’Banj ambapo alisema kuwa msanii huyo ana ‘uume’ mdogo, aliuona vipi wakati anadai hajafanya mapenzi kwa miaka kumi? swali gumu hilo…

Kutana na picha 10 za pozi tofauti za Mkenya Huddah wa BBA 2013!


Moja ya majina ya maceleb wa nchini Kenya ambayo yanatajwa sana na pia yanaonyesha kuongoza kwa kuwa Clicked na ku-trend kwenye google , Blogs na mitandao ya kijamii ya Twitter,Instagram na Facebook ni jina Huddah Monroe.

Huyu ni mkenya ambaye amejijengea jina kwa urembo wake lakini pia amehusishwa na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa C.M.B Prezzo japo amekuwa akikanusha, alishiriki pia shindano la Big Brother The Chase 2013 lakini alitolewa mapema baada ya kukaa wiki moja ndani ya mjengo.
Huddah akiwa ameweka pozi.

KIKWETE"ATAKAYE SUBUTU KUIGUSA TANZANIA ATAKAKIONA CHA MOTO"

Rais Jakaya Kikwete ametuma ujumbe kwa wale wanaoitishia Tanzania. Amewaambia wakithubutu watakiona cha mtemakuni kama ilivyokuwa kwa Idd Amin wa Uganda. 


Alisema mamlaka za ulinzi na usalama zilimdhibiti Amin alipofanya uvamizi katika ardhi ya Tanzania mwaka 1978 na kwamba hazitashindwa kufanya hivyo kwa mtu mwingine yeyote atakayechezea usalama wa nchi.
Wakati Rais akisema hayo, Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amewahakikishia wananchi kuwa wakati wote jeshi liko imara na kuwataka wasiogope lolote.
Viongozi hao walisema hayo jana katika maadhimisho ya Siku ya Mashujaa iliyofanyika katika Kambi ya Jeshi ya Kaboya iliyopo Muleba, Kagera.
“Sihitaji kusema tena, mmeshamsikia Mkuu wa Majeshi, atakayejaribu atakiona cha mtemakuni, laleni usingizi na msiwe na wasiwasi, msisikilize maneno ya mitaani,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Wakati wowote, saa yoyote tuko tayari kulinda nchi yetu. Hatuko tayari kuona amani inaharibika nchini, hatuwezi kuruhusu mtu yeyote kuimega au kuichezea nchi yetu kama alivyofanya Idd Amin.”
Katika siku za karibuni kumekuwa na kauli kadhaa kutoka kwa baadhi ya viongozi wa nchi jirani ambazo zinatafsiriwa na wananchi kwamba ni za kuitisha Tanzania.
Jenerali Mwamunyange alisema jeshi wakati wote liko imara kuwalinda wananchi na nchi kwa jumla hivyo wasiogope...“Endeleeni na shughuli zenu na msiogope mtu yeyote, fanyeni kazi zenu bila wasiwasi.”
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria maadhimisho hayo, Jenerali Mwamnyanye alisema yeyote atakayethubutu kuchezea usalama wa nchi atakiona cha mtema kuni.
Akizungumzia Siku ya Mashujaa, Rais Kikwete alisema ni siku ya kuwakumbuka mashujaa waliojitolea maisha yao wakati wa Vita ya Kagera kuilinda nchi yao ili iwe salama na yenye amani.
“Kuhakikisha usalama wa nchi kuna gharama yake kwani kuna wengine walikufa na wengine wakabaki na vilema kwa ajili ya hilo. Wale ambao wamebaki na wana matatizo lazima tuwaangalie vizuri na vile ambavyo havijafanyika tutavishughulikia kwani kutetea taifa ni kazi ngumu.”
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwamo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal, Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein, Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande na Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu ambao wote walipewa nafasi ya kuwasalimia wananchi waliohudhuria maadhimisho hayo.

Awali, viongozi wa dini, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Bukoba Methodius Kilaini, Shehe wa Mkoa, Haruna Kichwabuta na Mwakilishi wa Jumuiya ya Makanisa ya Kikristo, Askofu Elisa Buberwa walitoa wito kwa Watanzania kuthamini amani iliyopo na umuhimu wa kuwa na mshikamano katika kuilinda na kuhakikisha kwamba haivurugwi kwa misingi ya imani, itikadi au ukabila.
Matatizo Muleba
Awali, Rais Kikwete aliwahakikishia wananchi wa Muleba kuwa matatizo ambayo wabunge wao wameyawasilisha kwake mbele yao atayashughulikia.
“Nimesikia yale waliyoyasema hapa ; suala la mpaka kati ya eneo la wananchi na jeshi, Waziri wa Ardhi yupo hapa, kaeni na jeshi na vijiji ili tatizo liishe ni jambo ambalo linawezekana hivyo litatuliwe,” alisema Rais Kikwete.
Alisema suala la umeme na madaraja litashughulikiwa na viongozi wa mkoa wakishirikiana na wabunge na watakapokwama wafikishe kwake... “Mimi ndiye ninayetoa fedha za maendeleo hivyo hayo masuala yakikwama waniambie nitayashughulikia.”
Imeandikwa na Boniface Meena Dar na Joas Kaijage, Muleba

UBALOZI WA MAREKANI WAIPONGEZA TTCL KWA KUTOA HUDUMA BORA ZA MAWASILIAN​O WAKATI WA UJIO NA UWEPO WA RAIS BARACK OBAMA



Afisa Mtendaji mkuu wa TTCL Dtk. Kamugisha Kazaura akibadilishana mawazo na Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader akitoa shukrani zake kwa uongozi na wafanyakazi wa TTCL alipotembelea makao makuu ya Kampuni hiyo.

Afisa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa TTCL Bw. Peter Ngota akiwashukuru wawakilishi kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini kwa kutambua mchango wa TTCL katika kufanikisha ziara ya Rais wa Marekani alipotembelea Nchini Tanzania.
Uongozi wa TTCL pamoja na wawakilishi wa Ubalozi wa Marekani hapa nchini katika picha ya pamoja.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL dkt. Kamugisha Kazaura akipokea cheti cha shukrani kutoka kwa Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader.
*******
Kampuni ya simu Tanzania (TTCL) imepongezwa na Ubalozi wa Marekani kwa huduma bora iliyotoa wakati wa ujio wa Rais wa Marekani hapa nchini.

Akitoa shukrani hizo Kiongozi wa ujumbe kutoka ubalozi wa Marekani hapa nchini Bw. Jeff Shrader amesema, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umejipatia sifa kubwa kwa huduma bora na za uhakika kutoka TTCL wakati wote wa ujio na uwepo wa Rais wa Marekeni hapa nchini.
Ameongeza kuwa huduma walizozipata zimethibitishwa na taarifa kutoka ofisi inayoratibu safari za Rais wa Marekani kuwa katika nchi walizopita Afrika huduma ya mawasiliano ialiyoipata Tanzania ilikuwa ni ya kiwango cha juu na aliipongeza TTCL na kusema hii ni sifa kubwa kwa Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa Marekani hapa nchini.

Akipokea salam hizo za shukrani kutoka kwa ujumbe huo wa Marekani, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura amesema, TTCL ilifanya kazi yake kwa uhakika na ina uwezo wa kuhimili mahitaji ya watanzania na Kimataifa pia.

Ameongeza kuwa TTCL inaendelea na juhudi za kujikita zaidi katika huduma ya data/ intanet na kuendelea kuboresha gharama ili kila mtanzania apate fursa ya kunufaika na mawasiliano ya simu pamoja na data.

Katika Shukurani zake Bw. Jeff Shrader alioa pia zawadi kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Dkt. Kamugisha Kazaura na kwa baadhi ya wawakilishi kutoa fani mbalimbali za Ufundi na Biashara kwa niaba ya wafanyakazi wote wa TTCL kama ishara yao ya shukurani kwa TTCL na Taifa kwa ujumla.