HUKU akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo,Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.
“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyie si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande
-GPL
No comments:
Post a Comment