Tuesday, September 27, 2011

CECILIA AWASHUKURU WATANZANIA


Meneja wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, Hamid Abdulkarim akiwa amemshika mkono Cesilia Edward (14) mwenye tatizo la moyo linalosababisha kuvimba tumbo akitoka Hospitali ya Regency jana tayari kwa safari ya New Delhi, India kwa matibabu.
Mtoto Cecilia Edward ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliopelekea kuvimba kwa tumbo amewashukuru kwa moyo mkunjufu watanzania waliojitokeza katika kumsaidia kwa hali na mali mpaka kufanikiwa kupata hela tayari kwa matibabu anayotarajia kwenda kuyapata nchini India.
 Cecilia amesafiri kuelekea katika hospitali iitwayo Fortis inayopatikana New Delhi -India kwa matibabu, jumatatu ya tarehe 26 mwezi septemba mwaka huu.
 Aidha walezi wa Sesilia familia ya mzee Kambaliko inatoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa moyo kumsaidia binti yao kwa kutoa pesa, mavazi na hata waliowapa maneno ya faraja pamoja na wale wote wanaoikumbuka familia hiyo katika maombi.
 Kabla ya safari yake hiyo, hali ya kiafya ya sesilia ilikuwa ikiendelea vizuri, kwani alikuwa anaweza kupumua na kukaa, tofauti na awali kutokana na kupunguzwa kwa kiasi cha maji katika tumbo lake hospitalini Regency alipolazwa kwa ajili ya matayarisho kabla ya kuanza safari yake kuelekea nchini India kwa matibabu zaidi.
 Mtoto huyu aliondoka hapa nchini jumatatu ya tarehe 26 na ndege ya shirika la Quatar Airways akifuatana na daktari mmoja kutoka hospitali ya regency, pamoja na mlezi mmoja mpaka nchini India alipotarajia kupokelewa na madaktari tayari kwa uchunguzi wa kina na kisha kuanza matibabu yake.
 Kipindi cha Mimi na Tanzania kinapenda kuwashukuru Watanzania wote pamoja na makampuni mbalimbali yaliyojitolea katika kumsaidia Sesilia kwa ajili ya matibabu. Shukrani za pekee ziifikie hospitali ya regency hasa daktari Kanabar kwa uvumilivu na huduma nzuri kwa Sesilia. Pia kwa mchango wao wa kulipia nauli ya kwenda nchini India kwa Sesilia, mzazi na daktari ikiwa ni pamoja na matibabu ya awali anayoyapata hivi sasa.
Watanzania, pamoja tumeweza tena. Sesilia ni mmoja tu kati ya watoto milioni moja wanaosumbuliwa na tatizo hili, hebu tujitolee kuwasaidia watoto hawa bila ya kuchoka, pia tusimsahau binti huyu kwa maombi ili upasuaji anaotarajia kufanyiwa umalizike salama na kwa mapenzi yake Mungu mtoto huyu arudie katika hali ya kawaida kama watoto wengine.

Mungu mbariki Sesilia.Amen!

Saturday, September 24, 2011

ANGALIZO ALILOLITOA WAZIRI MKUU MSTAAFU CLEOPA D. MSUYA KUHUSU HALI YA UMEME NCHINI LIZINGATIWE.

Mh. Cleopa David Msuya.
Athari ambazo zinaweza kutokea kutokana na Taifa kuendelea kuwa kizani, wananchi wanaotegemea nishati hii kama nyenzo yao ya kujipatia kipato na uhitaji wa Nishati hiyo Mahospitalini, inaweza kutupeleka Watanzania tukaingia kwenye vugu vugu la wananchi kutaka kuitoa Serikali iliyo madarakani kwa njia maarufu inayoitwa 'NGUVU YA UMMA' kama mataifa mengi ya Kiislam yalivyotokea; mfano hai ni Misri.

Hayo yalisemwa na Mh. Msuya wakati alipokua kwenye mjadala wa kitaifa kuhusu miundombinu, nishati na madini katika Wiki ya Maonyesho ya Miaka 50 ya Uhuru yaliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF).
Upi ? Msimamo wa viongozi wa nchi Afrika kuhusu Libya?
Je ? wanamtambua kiongozi halali wa Libya?
Vipi ? kiongozi wa waasi Mustafa Abdel-Jalil anatambulika na Viongozi wetu?
 

Wakati viongozi wa nchi mbali mbali wamekutanika mjini New York, kwa ajili ya mkutano wa umoja wa mataifa UN, katika mkusanyiko huo wamo pia viongozi wetu kutoka nchi za kiafrika ambao pia ni wanachama wa umoja wa Afrika AU, ambayo Libya pia ni mwanachama wa AU,lakini utata unakuja nani kiongozi halali wa nchi hiyo Libya? Kanal Gaddaf au Mstafa Abdel-Jalil ambaye nae yupo huko New York.
 
Swali lingine kubwa ambalo wengi wetu tunajiuliza je ?viongozi wa nchi za  Afrika wanautambua uhalali wa Mstafa Abdel- Jalil ?kama hawautambui je? watakubali kuwepo ukumbini na kumsikiliza otuba ya kiongozi huyo aleyeingia  madarakani kwa njia ya bunduki tena kwa kusaidiwa na NATO? au watakuwepo
ukumbini kwa mithali za kiswahili kila moja na lwake? yaani ya Ngoswe muachie Ngoswe! je? fadhila za Kanal Gaddaf na mchango wake katika bara la Afrika  ndio zitakua zimesauliwa.
 
Mengi tunajiuliza lakini siye wafrika tunategea sikio uko UN kusikiliza msimamo wa viongozi wetu juu ya kauli ya pamoja kuhusu maslahi ya bara la Afrika.

Friday, September 23, 2011

To All Tanzanians and Friends,
On behalf of the family of Mr. Biseko Magesa Berrien Spring Michigan, I would like to update you on the collection mechanism of contributions towards the Dr. Israel Magesa Memorial Fund.
Dr. Israel Magesa will be laid to rest on Monday September 26 in Berrien Springs Michigan.
A new checking account has been established at Bank Of America. The Israel Magesa Memorial Fund account details are as follows:
Account Name: Biseko Magesa
Bank Name: Bank of America
Bank Address: 1803 S. M-139, Benton Harbor MI 49022
Bank Routing No: 072000805
Bank Account No: 375009262891
Or for people who live around Michiana Area you may deposit in any Federal Credit Union near you in account of:-
Name of Credit Union: UNITED FEDERAL CREDIT UNION
Account Name: Biseko Magesa
Account #: 0193011
Routing or Transit #: 272484894
You can contribute to the account using of the following options:
1) (i) Account to account transfer if you have a Bank Of America
2(ii) Deposit into the account at a local Bank Of America if you happen to have a Bank of America branch near you.
3) (iii) Wire transfer from your bank account from anywhere in the world.
(iv) Mail a check or money order payable to Biseko Magesa to the following address:
Biseko Magesa
6543 Deans Hill Rd.,
Berrien Center, MI 49102
For more information or updates, please contact any of the following:
1. Stephen Mndalila 574-344-0134 smndalila@hotmail.com
2. Mendrad Mchopa 269-240-0812 bobmchopa@yahoo.com
You can reach the Magesa's family to comfort them after such a big loss of their loved one by email at magesa@yahoo.com or by phone at (269) 313-4102 or simply pay them a visit at:
Biseko Magesa Family Address:
6543 Deans Hill Rd.,
Berrien Center, MI 49102
MEMORIAL PROGRAM IS AS FOLLOW
Viewing: Sunday september 25, 2011
Time: 2pm - 5pm
Location:
Allred Funeral Home:
212 South Main Street
Berrien Springs, Michigan 49103
Phone: (269) 471-3729
Service will take place on : Monday, September 26, 2011
Time: 11:00Am ( viewing) service starts 12:00pm
 Church address:
Michiana Fil-Am SDA Church
8454 Kephart Lane
Berrien Springs, MI 49103

May God bless you all.

Thursday, September 22, 2011

Leo tarehe 22 September ! Siku ya Kuzaliwa mwanamapinduzi
 Abdulrahman Mohamed Babu (RIP) 
Professor Abdulrahaman Mohamed Babu alikuwa mwanasiasa,mwanamapinduzi msomi,mwandishi,mchumi, na ujamaa kwake ulikuwa ni mfumo wa maisha yake.
Tunapowataja na kukumbuka wakongwe wa siasa na wapambanaji waliosimama kidete kuhakikisha kuwa wafrika tunajikomboa kutoka katika makucha ya ukoloni uwe mkongwe au ukoloni mambo leo,jina la marehem Abdulrahman Mohamed Babu (RIP)alitasahulika, ambaye kama angelikuwa hai leo tarehe 22 September ndio siku yake ya kuzaliwa.
Historia inatuelezea kuwa mwanamapinduzi marehem Prof. A.M.Babu alizaliwa 22 Sept 1924 huko kisiwani Unguja,Zanzibar, na alifariki dunia 05.08.1996, marehem Prof. A.M.Babu anakumbukwa kwa mengi pamoja na kuwa engineer wa mapinduzi ya visiwani 1964 yalimfanya sultani akimbie na kusahau kiremba kitandani.

Tuesday, September 20, 2011

KASI ZAIDI!! NGUVU ZAIDI!! NA HARI ZAIDI!! TULIAHIDI NA TUMETEKELEZA!! NA NYINGINE; TUMEWEZA! TUMETHUBUTU! TUNASONGA MBEEELEEE!! YA MWISHO NAYO; PIPOOO!!! PAWAAAA!!!

Hii ni moja ya Shule ya msingi Bukoba - Kagera

'HIZO ZOTE NDIO KAULI ZA WANASIASA'
Wanasiasa watatujia kwa kauli nyingi sana, lakini mwisho wa siku watoto wetu tunaishia kuwapa elimu kwenye mazingira kama haya! ebu muangalie huyo aliye karibu na Mfuko wa plastic, yupo darasani kweli!!! nini anachowaza! Mimi na wewe tutabaki tunahisi tu: Labda hajanywa chai! au anaumwa! La hasha! mazingira hayo yanampelekea kutomsikiliza mwalimu.
KAPINGAZ Blog inakwambia "TAFADHALI CHUKUA HATUA, TUWAWEZESHE WATOTO WETU WAPATE ELIMU BORA"

HAWA NDIO VIONGOZI WETU WA KISIASA!

Mh. Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Dr. Wilbrod Slaa, Katibu Mkuu wa CHADEMA. kumbukumbu zangu kama sijakosea wakiwa kwenye shughuli moja inayohusu CCBRT.
Mh Dr. Jakaya Kikwete akikumbatiana na Mh. Profesa Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha wananchi - CUF Tanzania

Watanzania wenzangu wanasiasa wetu wanapokua wanakuja kutuomba kura, wanakuja na mengi sana kutoka kwenye vinywa vyao, ni vema yale wanayoyasema tuyachukulie kama vile tunawaona wako pamoja wamekaa meza moja wakiwa wanatueleza hayo ya kwao. Hili litatusaidia sana kuwafanya wao wasiweze kutugombanisha sisi mpaka kutupelekea kutokea yale ambayo hatutaki yatokee.

KAPINGAZ Blog inakwambia Mtanzania kuwa makini na maneno yao; yatafakari kwanza kabla hujachukua hatua
"MJUE SENSEI RUMADHA FUNDI"

Wakati tunaelekea katika shangwe za miaka 50 ya Uhuru, tunawaletea makala maalumu ya matunda ya vijana walizozaliwa ndani ya miaka 50 ya uhuru,Tanzania pamoja na kuwa na watalaamu wa fani na taaluma mbali mbali lakini tunao wataalammabingwa wachache sana katika nyanza au fani ambazo ni adimu sana,watalaamu hao mojawapo ni mkufunzi bingwa wa michezo ya KARATE NA YOGA ,Mtanzania Sensei Rumadha Fundi,anayeishi kule Marekani aka nchi ya herufi tatu USA, Darubini yetu imemnasa na kama anavyoelezea: 
Muktasari wa Sensei Rumadha Fundi ”Romi”(Sandan)
Naitwa Rumadha Fundi, “Sensei Romi”Mvuto wangu katika sanaa ya Karate ulianza wakati nilikuwa mdogo mnamo miaka '70s pale Kariakoo,jiji Dar, lakini asili ya kwetu ni Tabora. Kwa bahati nzuri, jirani yetu pale mtaani(Aggrey/Congo) Dar-es-salaam ambako Sensei Bomani alikuwa anakuja kuwafuata baadhi ya wanafunzi wake enzi hizo. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wangu wa kujua hasa kuhusu Goju Ryu Karate.
Mwaka '78 mwishoni nilipata fursa ya kutembelea “Hekalu la Kujilinda” Zanaki Dojo Kan Shibu, nakuongea na Senpai Magoma Nyamuko Sarya. Kipindi hicho Sensei Bomani alikuwa amekuja toka Marekani na kuja kuwafanyia mitihani wa daraja la “Nidan”kina Senpai Magoma Nyamuko Sarya (Mwafunzi kiongozi), Senpai Tola Sodoinde Malunga, Sensei Gamanya nk. Ndipo nilipoanza shughuli za mafunzo kama”Teenager class”lilijulikana kama (Bomani Brigade)
Baada ya mtiani wa mkanda wa kahawia '81, kiongozi wetu (Senpai Magoma) aliondoka kwenda India na Phillippines kusomea sanaa mbalimbali na Yoga , ndipo na mimi nikajiunga nae huko India na baadae kwenda Sweden mnamo mwaka wa '85 katika shule ya Yoga”Internation school of Intution Practice” au katika lugha ya Sanskrit ambayo ndio inatumiwa na Yoga hujulikana kama “Prakshimata - Ananda Nilayam” huko, Gullringen, Vimmerby, Sweden.
Hapo ndipo lipohitimu ualimu wa Yoga baada ya kozi ya miaka miwili na kurudi tena Calcutta, India kwa Master mkuu wa Yoga duniani na hatimae kupata ngazi ya juu katika mafunzo ya Yoga mnamo mwaka wa '90 “Avadhuta”.
Vile vile nilipata fursa ya kwenda Houston, Texas mwaka '88 na kuendelea na mafunzo ya Karate mtindo wa “Okinawa Goju Ryu” chini ya uongozi wa Master Sensei Morio Higaona mwenye Dan 10, kiongozi mkuu wa “International Okinawan Goju Ryu Karate -Do Federation” na kupata fursa ya kupata daraja la kwanza '89 toka kwa Master Higaona huko Tampico, Mexico chini ya uongozi wa Sensei Mario Falcone wa Mexico na Sensei Ramon Veras wa Houston, Texas. Hawa ni moja ya walimu walio nisaidia kwa dhati katika sanaa ya Karate. Ninapenda kutowa shukran nyingi kwa walimu wote ambao waliweza kunifundisha sanaa hii sehemu zote zile nilizoweza kushiriki katika fani hii kama vile, Master Morio Higaona, Master Teruo Chinen, Sensei kiongozi wa Okinawa Goju Ryu, in Okinawa, Sensei Matsuda, na Sensei Muramatsu.Hao wote ni viongozi wa ngazi za juu sana duania katika sanaa ya mtindo wa Goju.
Kwa sasa hivi nina daraja la tatu “Sandan”mkanda mweusi kwa muda mrefu sasa. Kumbu kumbu yangu kubwa ni kuwa na ushirikiano mwema na wanafunzi wengi wa zamani pale “Hekalu la Kujilinda” ambao sasa hivi bado wapo mbele katika kusaidia vijana kama Sensei Maulid Pambwe, Rashid Almas, Mohamed Murudker, Wilfred Melkia, Geofrey Sawayael “Shoo”, Mbezi, Metthew huko Mwanza, Ndaukile,Edgar Kaliboti huko Sidney Australia, Salum Kitwana Khamisi huko UK. Hata wale wote ambao nimewasahau popote pale duniani.
Pia, natoa shukran nyingi sana kwa mtu muhimu sana katika maisha yangu ya kisaa ya Karate na Yoga ambaye ulikuwa ndio mashine ya mafanikio yangu ngazi zote hizo, Senpai Magoma Nyamuko Sarya(Mahadev/Mrnal) popote pale alipo nasema,”Shkran”.
Mipango ya uendelezaji sanaa hii kwa miaka ya mbele huko Tanzania ni muhimu sana. Moja ya hiyo mipango ni siku moja kufungua chuo cha sanaa ya kujilinda na kutumia nyezo za Karate”Kobudo” Kama vile “Sai, Tonfa, Nunchaku,Bo, Shuri, “Three section Nunchaku” nk. Kwa ajili ya kufundisha Tanzania. Ingawa sio leo wala kesho, bali ni moja ya mipango ya mbele huko katika maisha nitaporudi Tanzania, nakuwashirikisha walimu wengine wenye uzoefu mwingi katika kutumia nyenzo hizo.
Sensei Rumadha fundi pia at facebook Romi Fundi

Monday, September 19, 2011

Happy Birthday Kakamanda ketu ! Ras Makunja wa FFU ! 19.September
Leo tarehe 19.September ni siku ya kuzaliwa mwanamuziki,Ebrahim Makunja aka
Kamanda Ras Makunja ,mtunzi,mwimbaji na kiongozi wa bendi maarufu "Ngoma Africa band" aka FFU,yenye makao yake nchini Ujerumani.
Kamanda Ras Makunja alizaliwa Katikati ya jiji la Dar-es-salaama 19.Septemeber/
mtoto wa kiume wa Bw.Jumanne Saleh Makunja(RIP) na Bi.Moza Hassan Mpili.
www.ngoma-africa.com

Saturday, September 17, 2011

VITENDO HIVI VYA KIKATILI VYA WATU KUPIGWA NONDO VITAISHA LINI MBEYA?

Bwana Elia Daudi Mwalonde mkazi wa Uyole akiwa hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya wodi namba 1 baada ya kupigwa nondo hivi karibuni.

Bwana Zefania Mwangwale mwenye umri wa miaka 31 mkazi wa Uyole akiwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya baada ya kupigwa nondo pia.

Vitendo vya watu kupigwa nondo kwa Jiji la Mbeya vimekua kama ni vitendo vya kawaida, ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu kila mwaka lazima hivi vitendo vitokee na kupelekea watu wengi wa jiji la Mbeya kuishi katika maisha ya wasi wasi sana.
OFISI YA WAZIRI MKUU TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
 
TAARIFA KWA UMMA

NOTISI YA KUANZISHA MIKOA NA WILAYA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge.

Katika kutekeleza Mamlaka hayo, Rais ametoa notisi ya kusudio la kuanzisha Mikoa minne (4) na Wilaya kumi na tisa (19). Notisi hizo ambazo zimetolewa chini ya kifungu cha 4 cha Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002 ni Tangazo la Serikali Na. 285 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Mikoa na Tangazo la Serikali Na. 287 la tarehe 9 Septemba, 2011 kwa ajili ya uanzishaji wa Wilaya.

Madhumuni ya Notisi hizi ni kuzialika Taasisi na mtu mwingine yeyote ambaye ataathirika na uanzishaji huo kutoa maoni, mapendekezo au pingamizi iwapo yatakuwepo katika kipindi cha siku 21 kwa Mikoa mipya na siku 30 kwa Wilaya mpya kuanzia tarehe ya Notisi hizi.

Baada ya muda uliowekwa kupita, Rais atachambua maoni, mapendekezo na pingamizi zilizotolewa na kuzitolea uamuzi kabla ya kuanzisha rasmi Mikoa na Wilaya hizo kwa kadri atakavyoona inafaa.

Mikoa mipya inayoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

MKOA
WILAYA ZAKE
MKOA ZINAKOTOKA
MAKAO MAKUU
1.
Geita
Geita
Mwanza
Geita
Nyang’hwale(Mpya)
Mwanza
Chato
Kagera
Bukombe
Shinyanga
Mpya/Mbogwe
Shinyanga
2.
Simiyu
Bariadi
Shinyanga
Bariadi
Itilima (Mpya)
Shinyanga
Maswa
Shinyanga
Meatu
Shinyanga
Busega (Mpya)
Mwanza
3.
Njombe
Njombe
Iringa
Njombe
Wanging’ombe(Mpya)
Iringa
Ludewa
Iringa
Makete
Iringa
4.
Katavi
Mpanda
Rukwa
Mpanda
Mlele(Mpya)
Rukwa

Wilaya mpya zinazoanzishwa na Makao Makuu yake ni kama ifuatavyo: -

WILAYA MPYA
WILAYA MAMA
MKOA
MAKAO MAKUU
1.
Buhigwe
Kasulu
Kigoma
Buhigwe
2.
Busega
Magu
Mwanza
Igalukilo
3.
Butiama
Musoma
Mara
Nyamisisi
4.
Chemba
Kondoa
Dodoma
Chemba
5.
Gairo
Kilosa
Morogoro
Gairo
6.
Ikungi
Singida
Singida
Ikungi
7.
Itilima
Bariadi
Shinyanga
Itilima
8.
Kakonko
Kibondo
Kigoma
Kakonko
9.
Kalambo
Sumbwanga
Rukwa
Kalambo
10.
Kaliua
Urambo
Tabora
Kalua
11.
Kyerwa
Karagwe
Kagera
Rubwera
12.
Mbogwe
Bukombe
Shinyanga
Mbogwe
13.
Mkalama
Iramba
Singida
Nduguti
14.
Mlele
Mpanda
Rukwa
Inyonga
15.
Momba
Mbozi
Mbeya
Ndalambo
16
Nyang’hwale
Geita
Mwanza
Nyang’hwale
17.
Nyasa
Mbinga
Ruvuma
Mbamba Bay
18.
Uvinza
Kigoma
Kigoma
Lugufu
19.
Wanging’ombe
Njombe
Iringa
Waging’ombe

Kwa taarifa hii, Wananchi wote wanaalikwa kutumia haki yao ya kisheria kutoa kwa maandishi maoni, mapendekezo na pingamizi kama zipo kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa maeneo husika na maslahi ya Taifa kwa ujumla. Maoni, pingamizi au mapendekezo hayo yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo: -

Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,
S. L. P 1923,
DODOMA.

Fax- 026-2322116

 Imetolewa na: -

 Katibu Mkuu,
Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


9 Septemba, 2011