Friday, November 30, 2012

MISS EAST AFRICA DEC 7 WAJUE HAPA




Warembo watakaowania taji la Miss East Africa 2012 wakiwa katika vazi la ufukweni, jijini Dar es salaam. Shindano hilo litafanyika tarehe 7 December 2012 (Ijumaa wiki ijayo), kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es salaam.


Mashindano haya Yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd na kudhaminiwa na TANAPA, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, Ethiopian Airlines, Seascape Hotel, Darlings Hair, Ako Catering, DTP, Satguru, na Clouds FM.

Wednesday, November 28, 2012

NAPE AONGOZA MAELFU MAZISHI YA SHARO MILIONEA, MUHEZA‏



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (Watatu kulia, waliobeba jeneza) akishiriki kubeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi, kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga. (picha na Bashir Nkoromo)



Mwana FA akitoa salam kwa niaba ya Wanamuziki wa Bongofleva, wakati wa mazishi hayo

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na Rais wa Bongo Movies Simon Mwakifyamba na Ofisa Habari wa Airtel Jackson Mbando, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashirb Nkoromo).

Mwili wa Marehemu ukiswaliwa kabla ya kwenda kuzikwa.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akitoa pole za Chama Cha Mapinduzi (CCM) alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye mazishi ya aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea,leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).



Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akimpa pole Zaina Mkieli, Mama wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya na filamu, Hussein Ramadhani maarufu kwa jina la Sharo Milionea, alipokiwakilisha Chama Cha Mapinduzi kwenye mazishi ya msanii huyo, leo kwenye Kijiji cha Lusanga, Muheza Tanga. (Picha na Bashir Nkoromo).

ARUSHA NA KENYA MAMBO TAMBARARE SASA



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano Novemba 28, 2012 tayari kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa barabara ya Arusha-Namanga-Athi River pamoja na Mkutano wa Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utaozungumzia maendeleo ya miundombinu. Kiongozi wa Jumuiya ya Waislamu wa Ismailia Mtukufu Aga Khan naye alikuwepo hapo uwanjani

Tuesday, November 27, 2012

HASHEEM THABEET NBA SUPER STAR



Throw it down, big man. 
The best 94-second collection of Hasheem Thabeet's NBA career:
Thabeet finished with a career-high 13 points and grabbed 10 rebounds, his best performance on the boards  in the Thunder's 114-69 destruction of the Bobcats on Monday night. The 13-and-10 outing gave Thabeet his first career double-double in his 148th NBA game.

JB MPIANA ATUA KUWASINDIKIZA MASHUJAA BAND IJUMAA


Mwanamuziki JB Mpiana (waliokaa katikati) akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam

NYOTA wa muziki wa dansi barani Afrika, JB Mpiana ametua jijini Dar es Salaam jana tayari kwa maonyesho kadhaa, likiwamo lile la uzinduzi wa albamu ya Mashujaa Band inayokwenda kwa jina la Risasi Kidole, litakalofanyika Ijumaa katika viwanja vya Leaders Club, Dar es Salaam.

Kabla ya shoo hiyo ya Ijumaa, JB Mpiana ambaye amekuja na kundi lake zima la Wenge Musica BCBG, likiwahusisha wanamuziki wake za zamani na wapya, atauwasha moto jijini Arusha kesho kabla ya kufanya kweli jijini Mwanza Jumapili.

Akizungumza katika Hoteli ya Double Tree iliyopo Masaki, Dar es Salaam, JB Mpiana ameahidi kutoa shoo ya aina yake ambayo anaamini itakonga nyoyo za Watanzania.

Alisema kuwa amefurahisa sana kuja Tanzania kwa mara nyingine, ikiwa ni pamoja na mapokezi aliyoyapata, akiahidi kutoa burudani ya nguvu kwa Watanzania kuwalipa mapokezi waliyomwonesha.

“Nina imani waandaaji wamefanya maandalizi ya kutosha, nimekuja na wanamuziki wangu wote 25, nimekuja na vifaa vyangu vyote vilivyopo katika kundi langu, ili kutoa burudani ya kutosha kwa Watanzania.

“Nimewaletea albamu inayojulikana kwa jina la Biloko (chakula), watanzania wajiandae kula, yaani kupata burudani ya nguvu kutoka kwangu na kundi langu,” alisema JB Mpiana.

Kati ya wasanii aliokuja nao, alisema wapo wale wa zamani aliokuwa nao enzi hizo ndani ya kundi lake hilo lilipoanza kutamba katika anga ya muziki, na wengine wapya ambao wapo fiti.

Katika programu yake hapa nchini, amesema atapiga nyimbo zake za zamani na mpya ili kuwapa watanzania fursa ya kupata vionjo vya zamani na vipya, kuweza kupima ubora wa kazi hizo.

Akizungumzia muziki wa Tanzania, amewataka wasanii wa hapa nchini kujituma na kuzipenda kazi zao na kuiheshimu waweze kufanikiwa katika kazi zao hizo.

Juu ya kiongozi wa safu ya unenguaji, alisema safari hii inaongozwa na mwanadada Zambrota, ikiwa ni baada ya kufariki kwa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo, Monica.

“Nimefurahi sana kuja Tanzania kwa mara nyingine, wapenzi wa burudani wajiandae kupata shoo ya nguvu kutoka kwa JB Mpiana,” alisema mkali huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kampuni ya QS Muhonda, Joseph Muhonda, waratibu wa maonesho hayo, amesema kuwa ni matarajio yao wakazi wa Dar es Salaam, Arusha na Mwanza, watafurahia shoo hiyo kutoka kwa JB Mpiana na Mashujaa kutokana na maandalizi ya nguvu waliyofanya, akiwataka wakazi wa maeneo hayo, kujitokeza kwa wingi.

Alisema kuwa katoka onesho la JB Mpiana jijini Arusha, atatumbuiza katika ukumbi wa Triple A kuanzia saa tatu usiku, wakati Desemba Mosi atakuwa katika ukumbi wa Villa Park kuanzia saa tatu usiku.

“Maandalizi yote yapo sawa, kila kitu kimekamilika, tuliahidi JB Mpiana anakuja na kweli amekuja kama mlivyomuona,” alisema na kuongeza kuwa JB Mpiana atasindikizwa na wasanii wa Bongo Fleva kama H Baba, MB Doggy, Ney wa Mitego na wengineo.

SHARO MILIONEA AFA AJALINI TANGA... NI YA VIFO VYA WASANII WA FILAMU BAADA YA MLOPELO NA JOHN MAGANGA SIKU CHACHE ZILIZOPITA... ALIPATA AJALI YA KWANZA JANUARI 2012 SAA 2 ASUBUHI, YA LEO NOVEMBA 27 SAA 2 USIKU IMECHUKUA MAISHA YAKE


Marehemu Sharo Milionea

MSANII wa filamu, Hussein Mkiety a.k.a Sharo Milionea amefariki usiku wa leo kufuatia ajali ya gari iliyotokea eneo la Maguzoni, Songa, Muheza.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Constatine Masawe,Sharo alikuwa peke yake garini wakati ajali hiyo ikitokea na mwili wake uko katika hospitali ya Teule, Muheza. 


Kamanda Masawe alisema Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVRToyota Harrier akitokea Dar es Salaam kwenda Muheza alipofika eneo hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake. 


Hii ni ajali ya pili kwa Sharo kupata mwaka huu baada ya Januari 5 kunusurika katika ajali ya basi alilokuwa amepanda la Taqwa likitokea Burundi kuelekea Dar es Salaam kupinduka katika eneo Mikese, Morogoro saa mbili na nusu asubuhi.

Sharo ambaye alikuwa amekaa kwenye siti ya mbele kabisa alipoteza simu tu katika ajali hiyo ambayo ilijeruhi abiria wengine vibaya.

Kifo cha Sharo kinafuatia vifo vya wasanii wengine wawili wa filamu nchini ndani ya wiki moja, Mlopelo aliyetamba na kundi la Kaole na John Maganga aliyetamba na filamu ya 'Mrembo Kikojozi' aliyocheza na Aunt Ezekiel. 

Vifo hivyo vinakumbushia msiba wa Steven Kanumba, ambaye pia alifariki ghafla. 

Sharo atakumbukwa kwa ubunifu wake katika uigizaji akitoka kama mchekeshaji msafi tofauti na wachekeshaji wengi waliomtangulia ambao waliamini vichekesho ni lazima kuvaa kama katuni, kujaza nguo tumboni ili kuonekana na matumbo makubwa ama kujipaka masizi.

Akipendeza kwa mavazi nadhifu, Sharo Milionea alipata umaarufu kwa msemo wake wa "kamata mwizi meeen" na "Ooooh mamma!" huku akijipangusa mabega katika pozi za kibrazameni.

Katika siku za karibuni amekuwa akitawala vioo vya televisheni kutokana na kushiriki tangazo la kampuni ya huduma za simu ya Airtel akiwa na mchekeshaji mkongwe King Majuto, ambapo msemo wake mwingine wa "umebugi meen!" umetawala hasa midomoni mwa watoto.





Marehemu Mlopelo

Marehemu Steven Kanumba

Monday, November 26, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZINDUA UWANJA WA NDEGE WA MPANDA MKOA MPYA WA KATAVI



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, leo katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar Chombo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka jiwe la msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliopo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja huo uliopo Mkoa wa Katavi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Hiyari ya Moyo chenye maskani yake, Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Mama Monica, chenye maskani yake, Maji Moto Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Mbunge mstaafu, Chrisant Mzindakaya, akijumuika na wasanii wa ngoza ya asili kucheza ngoma ya kabila la Wakonongo wa Inyonga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi. 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, leo katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar Chombo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka jiwe la msingi, kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliopo Mkoani Katavi. Uzinduzi huo umefanyika leo katika uwanja huo uliopo Mkoa wa Katavi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Hiyari ya Moyo chenye maskani yake, Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Mama Monica, chenye maskani yake, Maji Moto Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, leo kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi.
Mbunge mstaafu, Chrisant Mzindakaya, akijumuika na wasanii wa ngoza ya asili kucheza ngoma ya kabila la Wakonongo wa Inyonga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi.

Ripoti Ya Nchi Maskini Sana Duniani Ya Mwaka 2012





RIPOTI YA NCHI MASIKINI SANA DUNIANI MWAKA 2012
UKWELI WA MAMBO NA TARAKIMU


Geneva, 26 Novemba 2012 – Ripoti ya Nchi Maskini Sana Duniani ya Mwaka 20121, yenye kichwa kidogo cha habari Kutumia Fedha Zinazotumwa na Raia Wanaoishi Nga’ambo na Weledi Wao Kujenga Uwezo wa Uzalishaji, imetolewa leo.


Mwelekeo wa uhamiaji
Ø Idadi ya watu ambao wamehamia Ulaya kutoka Nchi Maskini Sana (LDCs) iliongezeka kutoka milioni 19 mwaka 2000 kufikia milioni 27 mwaka 2010. Hii ni sawa na 3.3% ya wakazi wote wa nchi hizo.


Ø Nchi Maskini Sana Duniani zinatoa 13% ya wahamiaji duniani kote---idadi ambayo inalingana na mgawo wa LDCs katika idadi ya wakazi wote duniani (12.1%).
Ø Wahamiaji wanne kati ya watano kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zinazoendelea (Kusini) na mmoja tu kati wa watano ndiye anaishi kwenye nchi zilizoendelea (Kaskazini).
Utumaji fedha


Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa na raia waliohamia ng’ambo kwenda kwenye nchi zao kiliongezeka mara nane kati ya mwaka 1990 na 2011: Kutoka dola bilioni 3.5 kufikia dola bilioni 27. Tangu mwaka 2008 kiasi cha fedha kimeendelea kuongezeka pamoja na kuwepo na anguko la kiuchumi duniani.
Ø Mwaka 2011 kiasi cha fedha zilizotumwa kwenda nchini Tanzania kutoka Uingereza zilikuwa dola milioni 4.5, kutoka Canada dola milioni 3.2 na kutoka Kenya dola milioni 2.5.
Ø Mwaka 2011, fedha zilizotumwa kwenda LDCs zilikuwa kama mara mbili ya thamani ya uwekezaji wa moja kwa moja (FDI) katika nchi hizi (dola milioni 15), na kiwango hiki kilizidiwa tu na Misaada Rasmi Kutoka Nje, yaani ODA (dola bilioni 42 mwaka 2010), kama chanzo cha fedha kutoka nje ya nchi.
Ø Kiwango cha fedha zinazotumwa kutoka nje kama kingegawanywa kwa mwananchi mmoja mmoja kiliongezeka kutoka dola 10 kama kila mtu angepokea hadi dola 30 kati ya mwaka 2000 na 2010.


Ø Fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje zina umuhimu wa pekee kwa LDCs ikilinganishwa na nchi zilizo katika makundi mengine. Katika LDCs, fedha zinazotumwa na raia kutoka nje zinachangia 4.4% kwenye pato la nchi na 15% ya thamani ya bidhaa zinazouzwa nje. Kiwango hiki ni kikubwa kwa mara tatu ikilinganishwa na nchi nyingine zinazoendelea (ambazo siyo LDCs).


Ø Kuanzia mwaka 2008 hadi 2010, kiasi cha fedha kilichotumwa kutoka nga’mbo kinalingana na zaidi ya moja ya tano ya pato la taifa la nchi za Lesotho, Samoa, Haiti na Nepal.
Ø Tangu mwaka 2009 hadi 2011, nchi za Nepal na Haiti zilipata fedha nyingi za nje kutoka kwa raia wao walio ng’ambo kuliko zile ambazo nchi hizi zilipata kutokana na mauzo ya bidhaa nje.


Ø Kwa LDCs tisa, kiwango cha fedha zinazotumwa na raia wanaoishi nje kilizidi kile cha uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (FDI) na misaada rasmi kutoka nje (ODA) kati ya mwaka 2008 na 2010. Hizi ni nchi za Bangladesh, Haiti, Lesotho, Nepal, Samoa, Senegal, Sudan, Togo na Yemen. Kwenye nchi nyingine nane za kundi la LDCs, katika kipindi hicho hicho, fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo zilizidi FDI: Benin, Burundi, Comoros, Ethiopia, Gambia, Guinea-Bissau, Kiribati na Uganda.


Ø Theluthi mbili ya fedha zinazotumwa na raia kutoka ng’ambo kwenda kwenye LDCs zinatoka kwenye nchi zinazoendelea.
Ø Duniani kote, gharama ya kutuma fedha zinafikia 9% ya kiwango cha fedha kilichotumwa; kwa LDCs gharama ni kubwa zaidi kwa theluthi moja (12%).


Ø Kama nchi zilizo kusini kwa Jangwa la Sahara zingelipia gharama za uhamishaji fedha kwa wastani wa gharama inayolipwa duniani kote, mapato yao yangekuwa yaliongezeka kwa dola bilioni 6 mwaka 2010.


Ø Asilimia 66 ya fedha zilizohamishwa kwenda kwenye LDCs kati ya mwaka 2009 na 2011 ni za nchi tatu tu: Bangladesh, Nepal na Sudan.


Ø Matumizi ya simu za mkono kwenye LDCs ni makubwa zaidi (368 kwa kila wakazi 1,000) kuliko idadi ya akaunti za benki (171 kwa wakazi 1,000). Simu za mkono zinaweza vile vile kutumika katika kuhamisha na kupokea fedha kutoka ng’ambo.


Kuhama kwa utaalam 


Ø Mtu mmoja kati ya kila watu watatu wenye ujuzi mkubwa (mwenye elimu ya chuo kikuu) kutoka LDCs anaishi ng’ambo. Kwenye nchi zilizoendelea kiwango ni mtu mmoja katika kila watu 25.
Ø LDCs sita zina raia wao wataalaum wengi zaidi wanaoishi nje ya nchi kuliko wale waliobakia nchini mwao: Haiti, Samoa, Gambia, Tuvalu na Sierra Leone.


Ø Theluthi mbili ya wahamiaji wenye ujuzi mkubwa kutoka LDCs wanaishi kwenye nchi zilizoendelea; theluthi moja wanaishi katika nchi zinazoendelea.


Ø Kiwango cha kuhama kwa watu wenye ujuzi kwenda ng’ambo ni kikubwa (20% ) kwa LDCs nyingi (30 kati ya 48).
Ø Wahamiaji kutoka LDCs wenye elimu ya chuo kikuu ambao wanaishi na kufanya kazi ng’ambo inafikia milioni 2.
Ø Idadi ya Watanzania waliohamia Uingereza kwa kumbukumbu za mwaka 2000 ni 10,535.


Ø Aina ya wahamiaji inafuata ukubwa wa kipato wa nchi mwenyeji. Katika nchi zilizoendelea, 35% ya wahamiaji ni wale wenye elimu ya chuo kikuu; kwenye LDCs 4% tu ya wahamiaji wana kiwango hicho cha elimu. Viwango hivi ni kwa wahamiaji kutoka nchi zote, japo viwango ni hivi hivi kwa wahamiaji kutoka nchi za kundi la LDCs.
Ø Theluthi moja ya wahamiaji kutoka LDCs ambao wana elimu ya chuo kikuu wanaishi Marekani.




Uwezo wa kiuchumi (Uchumi mpana)


Ø Kiwango cha ukuaji wa uchumi kwa mwaka kwa LDCs tangu kipindi cha msukosuko wa kiuchumi duniani (2009-2011) ni 4.7%, ambacho ni chini ya kiwango cha kipindi cha miaka ya ukuaji mkubwa wa kiuchumi (2003-2008), yaani 7.9%. Hii ina maana kwamba kiwango cha ukuaji wa kipato kwa mwaka kwa kila mkazi kilishuka kutoka 5.4% miaka ya ukuaji mzuri wa uchumi hadi kufikia 2.4%.


Ø Wastani wa ukuaji halisi wa pato la nchi katika LDCs mwaka 2011, yaani 4.2%, ulikuwa chini ya 4.9% ya mwaka 2009 wakati wa anguko la uchumi duniani.


Ø Kile kinachojulikana kama Gross fixed capital formation kwenye LDCs kilipanda kidogo kutoka 20.7% ya pato la jumla la taifa mwaka katika miaka ya 2005-2007 kufikia 21.6% miaka ya 2008-2010. Hata hivyo, bado kilibaki chini ya viwango vya nchi nyingine zinazoendelea, ambazo zilifikia kiwango cha 30.1%.


Ø LDCs zinaendelea kutegemea sana raslimali kutoka nje. Pengo la pato linalotokana na uagizaji bidhaa na uuzaji bidhaa nje lilikuwa kubwa kwa 20% ya pato la jumla la taifa katika nchi tano za kundi la LDCs mwaka 2011, wakati LDCs nyingine 13 pengo lilikuwa asilimia 10 ya pato la jumla la taifa. 


Ø Kiwango cha utegemezi wa rasilimali kutoka nje katika kulipia uwekezaji wa ndani ya nchi kati ya mwaka 2008 na 2010 kilikuwa 15% ya pato la jumla la taifa kwa LDCs ambazo hazisafirishi mafuta nje.
Ø Asilimia 62 ya mauzo ya bidhaa nje kutoka LDCs 48 yalikuwa ni kutoka nchi tano tu: Angola, Bangladesh, Equatorial Guinea, Yemen na Sudan. Ukiacha Bangladesh, nchi zote hizi zinauza mafuta nje.


Ø Mapato ya LDC kwa mauzo ya bidhaa nje yanategemea zaidi mauzo ya bidhaa moja (mafuta), ambayo yanaingiza 46% ya jumla ya mapato yote yanayotokana na mauzo ya bidhaa nje.


Ø Zaidi ya nusu ya mauzo ya nje kutoka LDCs (54%) yalikuwa yanakwenda kwenye nchi zinazoendelea mwaka 2011, mwelekeo unaothibitisha umuhimu wa biashara ya kusini-kusini. China ndiyo iliyonunua bidhaa nyingi zaidi kutoka LDCs (26.4%) ikiwazidi Jumuia ya Ulaya (20.4%) na Marekani (19%).


ZIKO WAPI NCHI MASKINI SANA DUNIANI?
Umoja wa Mataifa unaziweka nchi 48 kwenye kundi la Nchi Maskini Sana Duniani (LDCs). Mgawanyo wao ni kama ifuatavyo.


Africa (33): Angola, Benin, Burkina Faso, Burundi, Central African Republic, Chad, Comoros, Jamhuri ya KIdemnokrasia ya Kongo(DRC), Djibouti, Equatorial Guinea, Eritrea, Ethiopia, Gambia, Guinea, Guinea-Bissau, Lesotho, Liberia, Madagascar, Malawi, Mali, Mauritania, Msumbiji, Niger, Rwanda, Sao Tome na Principe, Senegal, Sierra Leone, Somalia, Sudan, Togo, Uganda, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zambia;
Asia (9): Afghanistan, Bangladesh, Bhutan, Cambodia, Lao, Myanmar, Nepal, Timor-Leste na Yemen;
Caribbean (1): Haiti;
Pacific (5):Kiribati, Samoa, Solomon Islands, Tuvalu na Vanuatu.




Kutengeneza list ya LDCs


List ya LDCs inapitiwa upya kila baada ya miaka mitatu na Baraza la Uchumi na Jamii (ECOSOC) la Umoja wa Mataifa, kufuatana na mapendekezo ya kamati ya Sera ya Maendeleo (CDP).
Katika mapitio ya hivi karibuni, Machi 2012, CDP ilitumia vigezo vifuatavyo:
1. Kigezo cha pato la kila mtu, kwa kufuata Pato la Jumla la Nchi (GNI) kwa kila kichwa (wastani wa miaka mitatu)
2. Kigezo cha raslimali watu ambacho kinatumia viashiria kama lishe, afya, kuandikishwa shuleni na kujua kusoma na kuandika
3. Kigezo cha mazingira hatarishi ya kiuchumi. Ambacho kinatumia viashiria kama mishtuko ya kiasili, mishtuko ya kibiashara, udogo na umbali.
Nchi tatu tu zimefanikiwa kupanda daraja kutoka list ya nchi za kundi la LDCs: Botswana Desemba 1994, Cape Verde Desemba 2007 na Maldivs Januari 2011. Samoa inategemewa kupanda daraja tarehe 1 Januari 2014.


ECOSOC ilipitisha pendekezo la CDP kuipandisha daraja Equatiorial Guiones mwezi Julai mwaka 2009 na mwezi Julai 2012 ikakubali pendekezo la CDP kuipandisha Vanuatu. Hata hivyo ruhusa ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa bado itahitajika ili kuzipandisha daraja nchi hizi mbili.