Monday, April 30, 2012

HIVI PUNDE KUTOKA SUMBAWANGA, MBUNGE WA SUMBAWANGA MJINI BWANA AESHI HILALY AVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA LEO ALIKUWA MBUNGE KUPITIA CHAMA TAWALA CHA CCM.

Kesi ya uchaguzi ya kupinga kutangazwa kwa ndg Aeshi Hiraly CCM kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini leo mashahidi wa pande zote mbili wamehitimisha kutoa ushahidi wao mbele ya jaji wa mahakama kuu mh Jaji`Bethuel Mpakani Kasefu Mmilla “J.4”(Judge incharge mahakama kuu Mbeya). Kesi hiyo inasikilizwa katika mahakama kuu mjini Sumbawanga, ambapo hoja za msingi zilizokuwa zikisikilizwa ni, moja, mchakato mzima wa uchaguzi kugubikwa na rushwa iliokuwa ukitolewa na mgombea wa CCM na pili ni uchakachuzi wa matokeo uliopelekea kutangazwa kwa bw Aeshi. Katika kesi hiyo iliyofunguliwa na bw Noberth Yamsebo aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA (mlalamikaji) anayetetewa na wakili mmoja toka mbeya na upande wa washitakiwa unatetewa na mawakili wanne. Kesi hiyo ilianza kusikilizwa rasmi tangu tarehe 27/03/2012 na leo tarehe 14/03/2012 ndio mashahidi wote wamemaliza kutoa ushahidi wao, upande wa mlalamikaji ulikuwa na mashahidi 25 na upande washitakiwa ulikuwa na mashahidi wanne tu ambao wawili kati yao “ bw Vitusi Silago mchambuzi wa mifumo manispaa ya Sumbawanga na bi Silvia Siriwa aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa na msimamizi mkuu wa uchaguzi wa jimbo la sumbawanga mjini” (kwa sasa yuko halmashauri ya wilaya ya Ileje kama mkurugenzi) ndo wamefunga pazia la mashahidi. Vielelezo mbalimbali vilitolewa upande wa mlalamikaji na mashahidi kama ushahidi kuihakikishia mahakama kutilia manani hoja za msingi za kesi hii, moja kati ya vielelezo hivyo ni fomu mbalimbali zilizotumika kujaza, kujumlishia na kutangazia matokeo ya ubunge ambazo zilitumiwa kuchakachulia matokeo, mashahidi upande wa mlalamikaji walitoa ushahidi wao dhidi ya mgombea wa CCM ukiwepo wa kununuliwa pombe, kununuliwa baiskeli, kupewa fedha cash, ununuzi wa shahada za kupigia kura, ununuzi wa vinanda “keyboard” kwa ajili ya kwaya za makanisa mbalimbali na kuwa vyote hivyo vilitolewa kwa mashariti ya kumpigia kura mgombea wa CCM bw Aeshi

RAIS DKT JAKAYA MRISHO KIWETE AWASILI TANGA TAYARI KWA KUSHUHUDIA SHEREHE ZA MEI MOSI ZITAKAZO FANYA TANGA KITAIFA MWAKA HUU HAPO KESHO NA YEYE MH RAIS AKIWA MGENI RASMI.

Hapa Mh Rais akisalimiana na watu walio jitokeza uwanjani hapo kuja kumpokea, kama unavyomona kati ya watu hao ni viongozi wa CUF chama cha upinzani kwa kuonesha upendo na Amani tuliyo jijengea Watanzania bila kujari Dini Siasa wote ni kitu kimoja.

Wadada wa kanisa nao awakubaki njuma kuonesha upendo wao kwa Mh Rais. Kama unavyo ona wakisalimia nae.

Mungu Ibariki Tanzania Yetu...

MWANA DADA LINAH SANGA AKIWA PAGAWAWISHA WAKAZI WA NEW YORK NA VITONGOJI VYAKA KATIKA SHOW ILIYO FANYANYIKA WKND HII KATIKA THE BASS LINE CLUB MT VERNON.


AJ Obao nae akiwa sambamba na Linah kukonga nyoyo za wa penzi waliojitokaza katika show hiyo.

Warembo wakipata kivuli cha picha ya kumbu kumbu na Linah.


Mambo waka wakaaaaaaa tu kila mtu na alivyo jisikia kwa raha zake....

Wera weraaa!!!

Friday, April 27, 2012

MWENYEKITI WA CCM RAIS JAKAYA KIKWETE AKIONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM

 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Kikao Chamati Kuu Ya CCM Ikulu Jiji Dar..


CHADEMA KUPITIA MH. TUNDU LISSU YAIBUKA KIDEDEA KESI YA UBUNGE SINGIDA MASHARIKI.

Wakili wa waleta maombi Wanaccm Godfrey Wasonga akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Tundu Lissu hayajatangazwa
Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge.
Mbunge wa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu akifutwa machozi na mke wake wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo,ni halali.

KAMATI KUU YA CCM YARIDHIA RAIS KUVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI .


Thursday, April 26, 2012

RAISI KIKWETE AONGOZA WATANZANIA SHEREHE ZA MUHUNGANO.




Rais Dkt Mrisho Kikwete Akisalimiana na Mke wa Baba Wataifa Mama Maria Nyerere Ambae Alikuwepo Kushihudia Sherehe Hizo za Kushereke Muhungano  Jijini Dar.

Tuesday, April 24, 2012

SUMA LEE MWANA MUZIKI WA BONGO FLAVA NA MSHINDI WA TUZO MBILI ZA KILLI AWARD KATIKA WIMBO WAKE WA AKUNAGA AINGIA NEW YORK KIMYA KIMYA.

Akiwa maheneo ya Time Square Manhattan New York.


Hapa akipata Menu katika moja ya restautant za Manhattan

Hapa akiwa ndani ya moja ya usafiri wa Manhattan Nyc....maharufu kama Subway....

Hapa akiwa na mweneji wake Ny Ebra!!akikisha apotei kwani Suma Lee akuzoea kuona vikwangua Anga kama hivi vya New Yoek City....

Sunday, April 22, 2012

LINAH, AJ, WAFUNIKA COLUMBUS, OH

Linah

Aj sambamba na Linah wakiwapa burudani wapenzi wa OH na kuna za pande hizo.......

Awa ndi mpango mzima katika juakisha Linah anawapa burudani sehemu yeyote waliyopo watanzania......DMK na Mzee mzima JP.......Big up..
Wapenzi wa waliojitokeza katika show hiyo...apakutosha kwa kweli watu walikuwa full


Saturday, April 21, 2012

Taswira Za Yale Maandamano Ya Wanaharakati Wanaodai Kura ya Maoni Dhidi ya Muungano Zanzibar .

Jeshi la Polisi likitoa tahadhari kwa wananchi waliofika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni juu ya Muungano
Mdau wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muunganoakisindikizwa na polisi kuondoka sehemu ya maandamano

Kiongozi wa kikundi cha Wazanzibari wanaodai kuitishwa kura ya maoni dhidi ya Muungano Rashid Salum Adiy akizungumza muda mfupi baada ya kushikwa na polisi kwa kufanya maandamano kinyume na sheria

Kikosi maalum cha Polisi cha kuzuia fujo kikijipanga kukabiliana na wanaharakati waliofika baraza la Wawakilishi jana

Hashim na wenzake wakiwa katika gari la Jeshi la Polisi likiwachukua na kuwapeleka Madema, baada ya kukusanyika katika viwanja vya baraza la wawakilishi wakidai kuwepo kwa kura ya maoni itakayoamua kuwepo au kutokuwepo Muungan.Picha na Habari na Mdau Othman Maulid

PINDA NA ZITO WANACHEEEEEEEEKA.


Siasa ni kitu kizuri sana hasa kikitumiwa kwa malengo yanayotakiwa na hasa katiika kuleta maendeleo, daima wanasiasa huwa na malumbano na kuoneshana chuki wanapokuwa katika mambo mengi ya kutafuta maendeleo ya wananchi wao na taifa kwa ujumla. Juzi Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alizua hoja ya kutafuta saini 70 za kumuondoa Waziri Mkuu madarakani zoezi ambalo linadaiwa kukamilika hadi sasa. 

Mtu mwingine anaweza sema kwa kauli ile huenda sasa Pinda na Zitto wakawa ni maadui lakini hakika ile ni siasa na mambo ya siasa ni siasa na urafiki na ujamaa wao upo pale pale kama hivi wanavyoonekana katika picha hii iliyopigwa leo mjini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma 

Pichani za juu zinamuonesha  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge, John Mnyika wa Ubungo (kushoto), Kabwe Zitto wa Kigoma Kaskazini  na Hamad Rashid wa Wawi, kwenye jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma Aprili 21, 2012.

lakini huku mtaani washabiki wa siasa hizo saa ingine wanaumizana, kuchukiana na kushindwa kusikilizana kwa namna yeyote ile.

Friday, April 20, 2012

MAWAZIRI NANE WAJIUZULU USIKU HUU.

Habari za redio one ambazo zimethibitishwa na Katulanda Frederiki mwandishi wa Mwananchi aliye Dodoma zinasema mawaziri nane wameamua kuachia ngazi usiku huu.
Mawaziri hao ni; Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu, Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Kilimo Chakula na Ushurika Jumanne Maghembe na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.Tutaleta habari hii uthibitisho usionamashaka utakapojulikana asubuhi

Mh. Spika akubali kuwasilishwa kwa hoja ya wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imauni na Waziri Mkuu siku ya jumatatu,baada ya mh. Tundu Lissu kuomba muongozo



WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE ZA FEDHA ZA UMMA WAKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BUNGENI DODOMA


Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza makamu mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) Mhe. Deo Filikunjombe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe. Balozi Sefue, alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha

Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. John Cheyo (katikati) wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zainabu Vulu. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, vitabu vya orodha ya Wabunge pamoja na kanuni za kudumu za Bunge wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma, leo.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akizungumza na mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Agustino Mrema wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Idd Azzan. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha