Friday, April 20, 2012

WENYEVITI WA KAMATI ZA BUNGE ZA FEDHA ZA UMMA WAKUTANA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, BUNGENI DODOMA


Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza makamu mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) Mhe. Deo Filikunjombe wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Katikati ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zitto Kabwe. Balozi Sefue, alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha

Katibu Mkuu kiongozi, Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. John Cheyo (katikati) wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Zainabu Vulu. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha.

Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah akimkabidhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, vitabu vya orodha ya Wabunge pamoja na kanuni za kudumu za Bunge wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma, leo.
Katibu Mkuu kiongozi Balozi Ombeni Sefue (Kulia) akizungumza na mwenyekiti wa kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) Mhe. Agustino Mrema wakati alipofanya ziara ya kikazi Bungeni Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Idd Azzan. Balozi Sefue alifanya ziara ya kikazi Bungeni kwa lengo la kujitambulisha

No comments:

Post a Comment