Sunday, April 28, 2013

ILE HARAMBEE YA ADOLPH BRIAN ILIYOKUA IFANYIKE LEO NEW YORK SASA HAITAKUWEPO BAADA YA WAFADHILI KUJITOKEZA KUGHARAMIA MAZISHI


Adolph, Brian au Thadeo Lwakajende Enzi ya uhai wake
TUNAPENDA KUWATANGAZIA KWAMBA ILE HARAMBE YA ADOLPH BRIAN ILIYOKUWA IFANYIKE LEO JUMAPILI SAA 10 JIONI NEW YORK, HAITAFANYIKA TENA BAADA YA KUJITOKEZA WAFADHILI KUTOKA BUKOBA NA NEW YORK WATAKAO GHARAMIA GHARAMA ZA MAZISHI YA MAREHEMU YATAKAYOFANYIKA JUMATANO MAY 1, 2013

RATIBA YA MAZISHI NI KAMA IFUATAVYO

     VIEWING:            LEE.O.WOOD FUNERAL HOME
                                      23 EAST 2ND STREET
                                     MT.VERNON,NY,10552   
                                    TIME:  10:00 AM/ 4 ASUBUHI

     MAZISHI :                  MT.PLEASANT CEMETERY 
                                      80 COMMERCE STREET
                                       HAWTHORNE,NY,10532 
                                       TIME: 1:00PM/7 MCHANA

KWA MAELEKEZO ZAIDI WASILIANA NA:

   RAHMA ADAM.........617 818 7657
  PETER LUANGISA...917 681 6971
  RASHIDI KAMUGISHA...973 703 4596
  BERNARD KIVUGO.......973 580 7166
  WILLIAM VEDASTO......973 551 2916
Samahani wakubwa zangu kumetokea wafadhili wa gharama za mazishi naomba muweke huu ujumbe badala ya ule niliowatumia mapema
TAFADHALI MTAARIFU MTANZANIA MENZAKO UKIPATA UJUMBE HUU. 

ANITHA ATWAA TAJI LA MISS ELIMU YA JUU MORO 2013
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.

Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary Aloyce (kulia) na mshindi wa tatu, Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao kutawazwa kuwa ndio washindi wa shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Tarchisic Mtui, akijinadi mbele ya majaji na kivazi cha ubunifu alichokitengeneza kwa majani ya mti, Muashock wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya juu mkoani humo.

Washiriki wa shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakicheza shoo ya ufunguzi wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange, akijinadi mbele ya majaji na kivazi cha ufukweni wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.

Mshiriki wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning mkoa wa Morogoro, Hellen Mhando akipita jukwaani kujinadi mbele ya majaji na kivazi cha usiku wakati wa Shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.

Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja maara baada ya kutwajwa wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce,Hellen Mhando, Tausi Idd na Asnath Mwakitwange.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ‘Bongo Fleva’ Barnaba Boy akitumbuiza mashabiki wa tasnia ya urembo wakati wa shindano la kumsaka Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakati wa wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.

MUUNGANO DAY NDANI YA NEW YORK KULIPENDEZAJE


Mh.Balozi Ramadhan Mwinyi ndiyo alikuwa mgeni mharikwa katika sherehe hizo za maadhimisho ya miaka 49 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika jijini New York. Sherehe hiyo ilihudhiliwa na watanzania wengi kutoka katika miji ya jilani na New York kama New Jersey, Delaware, Massachusetts na Connecticut. Watanzania waliungana kwa pamoja kwa kula chakula na kucheza music sambamba na vinywaji baridi.
Katibu wa jumuiya ya watanzania New York bwana Shaban Mseba akisoma risala katika sherehe hizo za muungano
Mwenyekiti wa jumuiya Hajji Khamis akiongea machache mbele ya watanzania waliojitokaza katika sherehe hizo zilizofanyika New York katika kitongoji cha New Rochelle.
Dr Chemponda alikuwa nae kama anavyoonekana katika picha akiongea machache juu ya jinsi gani anavyo ujua muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mama Ashura Duale nae anaujua sana muungano wa Tanganyika na Zanzibar na alikuwa mmoja ya washuhuda wa uchanganyaji mchanga wa pande zote mbili za Tanganyika na Zanzibar
Hii ndiyo cake ya muungano ikiwa mezani
Ukodak wa pamoja katia ya Dr Chemponda, kushoto mama Ashura katikati, na kushoto kwa mama Ashura ni mama mwenye nyumba wa Mh. Balozi Mwinyi, Na kulia na Mh. Balozi Mwinyi
Ukodak mbele ya cake 
Mh. Balozi akikata Cake tayari kwa kuwalisha wana muungano walio jitokeza katika sherehe hizo
Mh. Balozi Ramadhani Mwinyi akimrisha kipande cha cake mama mwenye nyumba wake kabla ya watu wengine awajapata nafasi hiyo. Kwa picha zaidi ya sherehe hizo zilizofanyika katika jiji la New york bofya read more.

Saturday, April 27, 2013

MANENO 18 YA MSG YA VITISHO MBUNGE LEMA ANAYODAI KUTUMIWA NA MKUU WA MKOA ARUSHA

Baada ya ishu zake Mahakamani kumalizika na kumpa ushindi, Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema (Chadema) ameingia tena kwenye headlines baada kutokea kifo cha Mwanafuzi wa chuo cha Uhasibu Arusha.

Mwanafunzi huyo aliuwawa juzi na kupelekea wenzake kufanya mpango wa kuandamana hadi kwa mkuu wa Mkoa kulalamika kuhusu matukio ambayo yamekua yakiwapata Wanachuo wa Uhasibu na kuripotiwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.

Mbunge Lema anasema juzi wakati anatoka nyumbani alikuta Wanafunzi wamekusanyika hivyo ikabidi asimame kujua kinachoendelea, akaambiwa ni Mwanafunzi kauwawa jana yake kwa kuchomwa kisu.

Yeye kama mbunge wa Arusha mjini ikabidi ampigie simu Mkuu wa Mkoa aliekubali na kuja chuo cha Uhasibu kuzungumza na Wanafunzi waliokua wanalalamika kufanyiwa matukio mengi ya kutisha.

Mkuu wa mkoa alipofika Wanafunzi walishindwa kumuelewa na kuanza kuzomea, ni kitendo kilichofanya polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi kutawanya umati uliokusanyika na kutuliza fujo pia ambapo Mbunge Godbless Lema nae ilibidi akimbie na kuliacha gari lake chuoni hapo ambapo anavyodai Lema, baada ya hilo tukio akaja kupata taarifa kwamba yeye ndio chanzo cha fujo hivyo anatafutwa na polisi.

Kwenye mahojiano na TheTZA millardayo.com Lema alisema haogopi kutafutwa na polisi na wala hajifichi manake yeye ni baba wa familia na ni Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alishakaa jela zaidi ya siku kumi hivyo hata kupelekwa polisi hakumtishi kabisa.
Huyu ndio Mwanafunzi alieuwawa kwa kuchomwa kisu.

Kuhusu msg anayodai kutumiwa na Mkuu wa Mkoa baada ya hilo tukio, namkariri Lema akisema “ujumbe alionitumia Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoka kwenye simu yake ya mkononi unasema….. Umevuka kiunzi cha kwanza, nitakuonyesha kwamba mimi ni Serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi….. hiyo ndio msg yenyewe, nimshukuru sana Mungu kwa ambavyo amemfanya Mkuu wa Mkoa kutuma msg kama hii, nimemjibu kwa kupata ujumbe wake na niko tayari kwa lolote… tunakaribia kuprint DVD kuonyesha tukio lilivyoanza mpaka mwisho”

Kwenye sentensi nyingine Lema amesema “hiyo DVD ikitoka itaonyesha ni kiasi gani Rais Kikwete anatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kuhusu Wakuu wa mikoa Tanzania, nimeongea na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa na nafikiri kuna hatua ambazo kama chama tutazichukua”

Baada ya polisi wa Arusha kuthibitisha kumsaka ili kumkamata Lema, alisema “Nataka waje wanikamate, wanikute barabarani wanivunje waniue kama walivyofanya kwa Mwangosi kule Iringa lakini siwezi kwenda Polisi kujisalimisha, najisalimisha Polisi kwa sababu gani? namuogopa nani, huyo Mulongo? mimi nijifiche Mulongo? wamekamata gari yangu Land Cruiser mke wangu amekwenda kuichukua wamemnyima gari, niliacha gari chuo cha Uhasibu kwa sababu kulikua hakuna namna ya kuchukua gari… kila mtu alikua anatafuta namna ya kukimbia… “

“Mke wangu amekwenda kuchukua gari anakutana nayo inaburuzwa, nilifunga gari na funguo lakini imefunguliwa…. wametumia funguo gani? na mimi ni Mbunge sijapigiwa simu na R.C.O? wanikamate huko njiani wanikamate wanipige waniue lakini mimi siogopi Kamanda, toka Mkuu wa Mkoa amekuja kufanya kazi Arusha nimekwaruzana nae zaidi ya mara nne au mara tano”


Hata hivyo millardayo.com ilimpigia simu Mkuu wa Mkoa ili kufahamu upande wa pili lakini simu yake haikupokelewa…. kama hivi hapa chini….

ISSUE YA UKIMWI-MADIWANI MBOZI WAPIGWA SHULE

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi wakisikiliza kwa makini wakti wakipata maelezo ya mchakato wa kuongeza hamasa ya kwa wananchi juu ya tohara, kwa ujumla mwitikio umekuwa mkubwa tangu operesheni ondoa mkono wa sweta iliyoanza mwezi huu kupitia hospitali ya wilaya ya Mbozi ambapo wastani wa watu 600 hujitokeza kila siku kunyofoa mikono ya sweta hata hivyo uwezo kwa siku ni watu 70tu!

Mh Makunganya akiwa anafuatilia mijadala

Mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti UKIMWI wilaya Mbozi CMAC mh Mgula akisoma kimemo "bila shaka kutoka kwa mmoja wa madiwani aliyetaka kujua vipande vya mikono ya sweta vinapelekwa wapi? kila anayefanyiwa suna angekuwa anapewa kipande chake akakifukie mwenyewe nyumbani!!!
Mwezeshaji na mnasihi katika hospitali ya wilaya ya Mbozi Bi Fumbo akifafanua jambo ambapo alieleza kuwa asilimia 80 ya wanawake wanabakwa licha ya kupata watoto kwenye kaya zao hawajawahi fika mshindo katika tendo la ndoa kutokana na akina baba kuwafakamia bila kuwaandaaa
na Danny Tweve wa Indaba Blog
Halmashauri ya wilaya ya MBOZI kupitia kitengo cha kudhibiti UKIMWI imeendesha warsha ya siku moja kwa wenyeviti wa kamati za kudhibiti UKIMWI za kata pamoja na mambo mengine kuzungumzia kampeni ya tohara kwa wanaume inayoendelea kutekelezwa kupitia hospitali ya wilaya ya Mbozi
Akizungumza kwenye warsha hiyo mratibu wa Kudhibiti UKIMWI wilaya Bwana Oscar Mgani alieleza kuwa katika kipindi kirefu wanachi wamekuwa wakihamasishwa kutoa mikono ya sweta, na sasa mwitikio umepanuka hadi kwa watoto wadogo 
Katika hali ya kuonyesha watu wanakumbwa na aibu kwa kuendelea kuwa na mkono wa sweta baadhi ya wazee wenye umri mkubwa wamekuwa wakiongozana na watoto hadi hosipitalini wakidai wanawapeleka vijana wao kutahiri lakini wakishafika ndani kwenye eneo la upasuaji mdogo wao wenyewe ndiyo wanaanza kuvua suruali ili wapate huduma!
katika mijadala mbalimbali iliyoendeshwa katika warsha hiyo miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni umuhimu wa kuhamamasisha wananchi wanaoishi na vvu kujiunga na vikundi vya waVIU vijijini ili waweze kunufaika na fulsa zinazotolewa na serikali za mitaa pamoja na program za UKIMWI wilayani.

MADIWANI WAUJIA JUU WARAKA KUTOKA TAMISEMI, KISA KUZIBA MIANYA

kutoka kushoto ni Makamu mwenyekiti ALAN MGULA, akifuatiwa na Mwenyekiti ERICK AMBAKISYE na akifuatiwa na DED MBOZI Levison Chilewa

michango ilianza hivi
Hawa watunga sheria wa baraza la Mbozi wakiwa hewani kama hivyo wakati kikao kikiendelea

Mh Emily Mzumbwe akichambua suala la uchangiaji wa hisa kwenye benki ya wananchi wa Mbozi ambapo limeonekana kurudisha reverse na madiwani baada ya kutaka mchakato huo usipelekwe puta kwa maelezo kuwa lazima wananchi waelimishwe pole pole namna ya kuchangia hisa zao badala ya kukata juu kwa juu sehemu ya fedha kwenye mauzo ya kahawa yao
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya MBOZI wakisikiliza majadiliano 
Kulia wa kwanza ni katibu tawala Mbozi bwana Lazaro Mwankenja akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji Mbozi bwana Levison Chilewa wakifuatilia upepo unavyokwenda kwenye baraza hilo 

AFISA utumishi Bwana Zabron Lulandala akifuatiwa na afisa Mipango wilaya bwana Ngoi wakifuatilia mijadala kwenye baraza la madiwani leo
Baadhi ya watendaji kutoka ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Mbozi pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya wakifuatilia mijadala kwenye baraza hilo leo

Hali hiyo ilijitokeza baada ya madiwani kupitia kamati zao kuanza kulalamika hatua iliyofikiwa ya kuzuiwa kwenda kukagua miradi wakiwa kwenye kamati zao na badala yake kupewa maelezo kuwa kuna waraka unaozuia kamati hizo kutokana na kukosekana ufanisi!

Ndipo miongozo mwenyekiti, azimio na maneno mengine ilipoanza kusikika, lakini mwishowe ikawa ngumu kurudisha wwaraka huo TAMISEMI na badala yake madiwani kukubaliana nao kwa shingo upande

Hatua hiyo ilifikiwa\ baada ya ufafanuzi kutolewa kuwa kimsingi serikali za mitaa pamoja na kuwa ni muhimili muhimu katika kuunganisha wananchi na kuleta maendeleo haimaanishi kuwa serikali kuu haina nguvu ya kuelekeza jambo mbele ya serikali za mitaa. 

Na kwamba kwa kutambua hilo ndiyo sababu halmashauri kwa sehemu kubwa kama siyo asilimia 95% hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu, hivyo pale inapoagizwa baadhi ya mabadiliko ngazi za chini hakuna lugha ya kuyapamba maelekezo hayo bali kuyatekeleza

Ndipo diwani mmoja akasimama na kuomba mwongozo kisha akachomekea na azimio! hata hivyo mwenyekiti wa baraza hilo akatoa ufafanuzi kuwa serikali haiwezi kuazimiwa kwakuwa baraza hilo limeundwa pia kutokana na maelekezo na miongozo kutoka juu hivyo waheshimiwa wawe wapole kwanza!
katika hatua nyingine suala la uanzishwaji wa benki ya wananchi ya Mbozi leo limeendelea kupigwa dana dana ya kukubaliana kuto kubaliana! baada ya madiwani kuunga mkono kuanzishwa kwa benki hilo lakini wakitaka wananchi waleweshwe pole pole na pia wapate ziara ya kwenda kujifunza mikoa mingine namna ya benki hizo zinavyofanya kazi
Katika hali inayoonyesha kuwa wimbi hilo lilishawekwa mapema, kila aliyenyanyuka alikuwa akiongezea misumali ya kuzuia kuharakishwa kuchangisha shilingi 200 kwa kilo ya kahawa kwaajili ya uanzishaji wa benki hiyo ambapo baada ya maelezo ya ufafanuzi ya mkurugenzi mtendaji wilaya ya MBOZI, bado suala hilo liliamuliwa kwa kutakiwa kwanza wapewe ziara na baadaye wananchi waelimishwe namna bora ya kushiriki uanzishaji wa benki hiyo.
indabaafrica blog

Friday, April 26, 2013

Uganda Govt wants four children per woman

The Government wants each Ugandan woman to produce only four children in the next 27 years to curb the acute population growth, a planning expert has disclosed.
Sarah Nahalamba, a senior planner, gender and social development, National Planning Authority. Photo by Francis Emorut

“In order to have sustainable population growth the government intends to lower the fertility rate of women to produce four children per woman,” Sarah Nahalamba, a senior planner, gender and social development at the National Planning Authority (NPA) said.

SIKUKU YA MUUNGANO ILIVYO FANA UKO TANZANIA

.

Ndege za kivita zikifanya maonesho katik sherehe za Miaka 49 ya Muungano jijini Dar es salaam leo.
Zenye rangi ya njano zinazomwaga rangi za bendera za Taifa ni ndege za mafunzo na zingine za kijivu
ni za kivita.
 
 
Jukwaa kuu lilipambwa kwa umaridani katika Uwanja wa Uhuru, Dar
Msafara wa Rais Jakaya Kikwete ukiwasili uwanjani
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride la jeshi la magereza
Rais Jakaya Kikwete akikagua gwaride
Mke wa rais, mama salma kikwete

Askari polisi wakipita mbele ya Rais kikwete (hayupo pichani)

ndege ya kivita ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTz)
 
Jiji lilipendeza kila mahala bendera ya Taifa zilisimikwa, hapa ni barabara ya Kilwa, Dar
 
Watoto ombaomba wakiomba maeneo ya Agha Khan jijini Dar
Foleni ya magari ilionekana wakati viongozi wa kitaifa wakienda Uwanja wa Uhuru, Dar, hapa ni Barabara ya Kilwa
Askari wa usalama barabarani wakidhiti magari ili kupitisha misafara ya viongozi