Baada ya ishu zake Mahakamani kumalizika na kumpa ushindi, Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema (Chadema) ameingia tena kwenye headlines baada kutokea kifo cha Mwanafuzi wa chuo cha Uhasibu Arusha.
Mwanafunzi huyo aliuwawa juzi na kupelekea wenzake kufanya mpango wa kuandamana hadi kwa mkuu wa Mkoa kulalamika kuhusu matukio ambayo yamekua yakiwapata Wanachuo wa Uhasibu na kuripotiwa lakini hakuna hatua zozote zinazochukuliwa.
Mbunge Lema anasema juzi wakati anatoka nyumbani alikuta Wanafunzi wamekusanyika hivyo ikabidi asimame kujua kinachoendelea, akaambiwa ni Mwanafunzi kauwawa jana yake kwa kuchomwa kisu.
Yeye kama mbunge wa Arusha mjini ikabidi ampigie simu Mkuu wa Mkoa aliekubali na kuja chuo cha Uhasibu kuzungumza na Wanafunzi waliokua wanalalamika kufanyiwa matukio mengi ya kutisha.
Mkuu wa mkoa alipofika Wanafunzi walishindwa kumuelewa na kuanza kuzomea, ni kitendo kilichofanya polisi kuanza kupiga mabomu ya machozi kutawanya umati uliokusanyika na kutuliza fujo pia ambapo Mbunge Godbless Lema nae ilibidi akimbie na kuliacha gari lake chuoni hapo ambapo anavyodai Lema, baada ya hilo tukio akaja kupata taarifa kwamba yeye ndio chanzo cha fujo hivyo anatafutwa na polisi.
Kwenye mahojiano na TheTZA millardayo.com Lema alisema haogopi kutafutwa na polisi na wala hajifichi manake yeye ni baba wa familia na ni Mbunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, alishakaa jela zaidi ya siku kumi hivyo hata kupelekwa polisi hakumtishi kabisa.
Huyu ndio Mwanafunzi alieuwawa kwa kuchomwa kisu.
Kuhusu msg anayodai kutumiwa na Mkuu wa Mkoa baada ya hilo tukio, namkariri Lema akisema “ujumbe alionitumia Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutoka kwenye simu yake ya mkononi unasema….. Umevuka kiunzi cha kwanza, nitakuonyesha kwamba mimi ni Serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi….. hiyo ndio msg yenyewe, nimshukuru sana Mungu kwa ambavyo amemfanya Mkuu wa Mkoa kutuma msg kama hii, nimemjibu kwa kupata ujumbe wake na niko tayari kwa lolote… tunakaribia kuprint DVD kuonyesha tukio lilivyoanza mpaka mwisho”
Kwenye sentensi nyingine Lema amesema “hiyo DVD ikitoka itaonyesha ni kiasi gani Rais Kikwete anatakiwa kufanya mabadiliko makubwa kuhusu Wakuu wa mikoa Tanzania, nimeongea na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr. Slaa na nafikiri kuna hatua ambazo kama chama tutazichukua”
Baada ya polisi wa Arusha kuthibitisha kumsaka ili kumkamata Lema, alisema “Nataka waje wanikamate, wanikute barabarani wanivunje waniue kama walivyofanya kwa Mwangosi kule Iringa lakini siwezi kwenda Polisi kujisalimisha, najisalimisha Polisi kwa sababu gani? namuogopa nani, huyo Mulongo? mimi nijifiche Mulongo? wamekamata gari yangu Land Cruiser mke wangu amekwenda kuichukua wamemnyima gari, niliacha gari chuo cha Uhasibu kwa sababu kulikua hakuna namna ya kuchukua gari… kila mtu alikua anatafuta namna ya kukimbia… “
“Mke wangu amekwenda kuchukua gari anakutana nayo inaburuzwa, nilifunga gari na funguo lakini imefunguliwa…. wametumia funguo gani? na mimi ni Mbunge sijapigiwa simu na R.C.O? wanikamate huko njiani wanikamate wanipige waniue lakini mimi siogopi Kamanda, toka Mkuu wa Mkoa amekuja kufanya kazi Arusha nimekwaruzana nae zaidi ya mara nne au mara tano”
Hata hivyo millardayo.com ilimpigia simu Mkuu wa Mkoa ili kufahamu upande wa pili lakini simu yake haikupokelewa…. kama hivi hapa chini….
No comments:
Post a Comment