Wednesday, June 30, 2010

Kimgongomgongo asilia!!!
Hivi huu ni utamaduni wetu au umasikini?

Monday, June 28, 2010

Watanzania tumsaidie balozi wetu mrembo wa shindano la warembo wa ulimwengu Tanzania 2010 atakapokuja Las Vegas kushindana na wenzake toka pande mbali mbali za Dunia. Kwa habari zaidi tafadhali nenda kwenye facebook Miss Universe Tanzania 2010. 
MWAKA UMEPITA TOKA UTUTOKE  KIMWILI  LAKINI SIKU ZOTE UTAKUWA NASI KIROHO!!!!


Wednesday, June 23, 2010


JUNI 22, 2010

Afrika ya Kusini 2 Ufaransa 1


Argentina 2 Ugiriki 0


Korea ya Kusini 2 Nigeria 2


Uruguay 1 Mexico 0

Nigeria na Ugiriki nyumbani, Ufaransa mashakani, nao wenyeji wafurahisha.

BUTI JIWE KUKAMUA MJINI EMMEN,HOLLAND
Jumamosi 26-06-2010
Mwanamziki Buti jiwe aka Henry Galinoma,Jr. mwenye maskani yake nchini Uholanzi anatarajiwa kutingisha jukwaa la onyesho kubwa la Midzomerhout Festival,mjini Emmen, huko Holand.  Mwanamziki huyo wa mziki wa dansi wa afrika mashariki amechaguliwa kuwa ndiye mwanamziki pekee wa kiafrika nchini Uholanzi kuwakilisha katika onesho hilo, ambapo pia atawaongoza jukwaani wanamziki watakao kwenda na mwavuli wa jina la "Africa Breezze".  Mwanamziki Buti Jiwe ameachia hewani album iliyobeba jina la "Samahani" ambayo inatamba katika vituo vingi vya redio ndani na nje ya Tanzania, hata hivyo Buti Jiwe ameahidi kuachia Remex ya album hiyo, kabla ya kumalizika mwaka 2010, hili kuhakikisha washabiki na wadau wa mziki wanapata mdundo wenye kuleta "Raha" katika burudani ya mziki.Buti Jiwe amewaomba wadau na washabiki wa mziki walio ndani na nje ya Bongo kukaa mkao wa kula!! CD za Buti Jiwe zinahitaji pia msambazaji mzalendo, atakaye sambaza CDs katika nchi za afrika mashariki.

Tuesday, June 22, 2010

LEO KATIKA KUKUMBUKA SIKU YANGU NILIYOZALIWA,  NINGEPENDA WATANZANIA WOTE  NJE NA NDANI YA TANZANIA TUWAOMBEE VIONGOZI WETU WAPATE HEKIMA NA BUSARA YA  KUTUONGOZA  ILI NCHI YETU INEEMEKE KWA MAZURI.

TUWAOMBEE WAACHE "UBINAFSI",  KWANI NDIO CHANZO CHA MATATIZO YETU MENGI NCHINI.  NA TUWAOMBE WALIOSHINDWA UONGOZI WAACHIE!!  WAKO WATANZANIA WENGI WENYE UWEZO MKUBWA WA KUWEZA KUIONGOZA  NCHI, TENA WENYE MTAZAMO NA UPEO WA HALI YA JUU.

WATANZANIA WALIPA KODI NAWAOMBA MUONYESHE UCHUNGU NA PESA YENU KWA KUWA WADADISI  NA NI NINI MNAFAIDIKA NA ULIPAJI WA KODI HIYO.

WATANZANIA MLIO NDANI NA NJE TUSIKUBALI TENA KUENDELEA KUWA "WANANCHI" BALI TUWE "WENYENCHI" KWA KUSHIRIKI KWENYE MAAMUZI MUHIMU NCHINI MWETU.  TUWACHE KUTOA MALALAMIKO WAKATI SISI WENYEWE NDIYO TULIOWACHAGUA VIONGOZI WABOVU. UCHAGUZI UKO NJIANI NA TUNA HAKI YA KUTOMPA KURA ZETU YE YOTE AMBAE HAFAI.

TANZANIA TUNAWEZA KUPIGA HATUA KUBWA YA MAENDELEO KWA WATU WETU NA NCHI YETU.  UONGOZI SIO "AWAMU"  BALI NI DHAMANA.

NAMUOMBA MWENYEZI MUNGU ANIJALIE AFYA NJEMA NA MAISHA MAREFU NA NAMSHUKURU KWA HAPA ALIPOKWISHA NIFIKISHA!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!!
Kweli pesa inaweza ikakosa thamani nakuwa kama karatasi ya kawaida!!!!!!!!!
Hatimaye Cristiano Ronaldo atoa ukame wa magoli na kufunga alilolifanyia mazoezi na Portugal wawararua Korea ya Kaskazini mabao saba bila!!!
Chile washeherekea ushindi wa bao 1 bila kwa Switzerland
Spain wawachapa Honduras 2-0

Monday, June 21, 2010

It's just for the love of the Game!!!!!

Matumaini ya Kombe kubakia kwenye ardhi ya Afrika yazidi kudidimia baada ya Ivory Coast kuchapwa 3-1 na Brazil. 
New Zealand wawachanganya Italy kwa kuwalazimisha kutoka nao 1-1
Paraguay 2  Slovakia 0

Sunday, June 20, 2010

Netherland wakishangilia ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Japan!
Ghana yaendelea kuonyesha machachari,  yatoka sare 1-1 na Australia
Cameroon yachapwa 2-1 na Denmark na kuwa timu ya kwanza ya Afrika kuaga michuano!
June 18th, 2010

England 0 Algeria 0

Slovenia 2 USA 2

Germany 0 Serbia 1

Friday, June 18, 2010

KOBE NA LAKERS MABINGWA KWA MWAKA WA PILI MFULULIZO!!!


Katika mchezo ambao ulikuwa na kina aina ya ushindani kama itegemeavyo katika fainali za NBA, vijana wa Lakers waliweza kuwazihirishia wapenzi wao kwamba bado wao ni mabingwa kwa ushindi wa vikapu 83-79 dhidi ya washindani wao wa jadi Celtics na hivyo kuunyakua ubingwa kwa mwaka wa pili mfululizo.
Wanaigeria hoi kwa Wagiriki watundikwa 2-1
Mexico wawavunja moyo Wafaransa, wawatandika 2-0
Korea ya Kusini yachapwa 4-1 na Argentina

Thursday, June 17, 2010

MIAKA MINGINE MITANO?

WENYEJI HOI!!!!!
Kikosi cha Uruguay chawatoa imani Waafrika ya Kusini kwa kipigo cha 3-0, na mwamuzi nae achangia kuwaliza...
Spain ambao ni tegemeo la wengi kuwa mabingwa wa michuano hii ya kombe la dunia, wapigwa na butwaa kwa kurundikwa 1-0 na Switzerland!