Saturday, February 27, 2010Hapa sio Bongo bali ni sehemu fulani hapa New York inaitwa College Point na ni maarufu sana kwa kila spare za magari kwa bei che. Madimbwi hata nchi kubwa za wenzetu yako!!!
Mwanamziki mkongwe HAMISI KITAMBI amefariki dunia leo 26 February 2010 Dar-es-salaam,

MAZISHI YATAFANYIKA JUMAMOSI saa 7.00 mchana 27-02-2010 MAGOMENI,Ifunda ,jirani na shule ya Mzimuni, Jijini  Dar-es-salaam.Mwanamziki mkongwe wa dansi Bw.Hamisi Kitambi,amefariki dunia siku Ijumaa alfajiri ya tarehe 26/02/2010  katika Hospatali ya Muhimbili.

Marehemu aliwahi kupigia bendi za Msondo Ngoma ,kabla ya kupata maumivu ya mguu yaliotokana katika hajali alipokuwa safarini na bendi ya msondo ngoma . Marehemu pia alikuwa mwanamziki nyota enzi za Tabora jazz, ambako alipigia bendi ya Tabora kabla ya kuhamia Juwata Jazz sasa Msondo Music band.

Kwa taarifa zaidi tafadhali mnaweza kuwasiliana kwa simu na familia ya marehemu kwa simu namba 0713 802370 Almasi Kassanga, au Bi. Mwamini Kitambi simu namba 0712 217740Mwenyezi mungu amlaze mahala pema peponi

Amin

Friday, February 26, 2010GET YOUR COPY WHILE SUPPLIES LAST!

Available online at Barnes and Noble, Amazon and Autor House
 HAYATI BALOZI DAUDI MWAKAWAGO

Blogu hii ya jamii imepokea kwa masikitiko makubwa sana msiba wa mpendwa wetu Mzee Balozi Daudi Mwakawago.

Wengi tuliotokea kupata kumfahamu Balozi Mwakawago wakati wa uhai wake tuna kila jema la kumsifia.
 Balozi Mwakawago alikuwa ni mtu wa watu, muungwana ambae ana utu wa ubinadamu, hakupenda makuu na hakuwa na ubinafsi. Alilitumikia taifa lake katika kipindi chote cha maisha yake kwa heshima na moyo mkunjufu, ndani na nje ya Tanzania na kuliletea taifa letu heshima ya kipekee.

Wakati wa uwakilishi wake kwenye Umoja wa Mataifa hapa New York, tuliishi nae kiungwana sana, kwani yeye na familia yake walikuwa wakarimu sana kwa kila Mtanzania.

Pamoja na majukumu mazito ya kikazi, lakini Balozi Mwakawago na familia yake siku zote walikuwa karibu sana na Jumuia nzima ya Watanzania, iwe ni kwa raha au matatizo. Waliweza kutumia muda wao hafifu kutuliwaza, kutupongeza na kucheka nasi.

Ingawa tumempoteza Mzee wetu, lakini maisha yake ni fundisho kubwa kwetu na kumbukumbu zake tutabaki nazo daima.

Rambi rambi za dhati kwa familia nzima ya  Mzee Mwakawago  wakati huu mgumu wa kipindi cha maombolezi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu!

-FUNDI RAMADHANI-
Kweli maisha yamepanda! Eti kuvuka ili daraja kwenda Staten Island/New Jersey ni dola kumi na moja? Hii ina maana ya kwamba kwa mtu anayepata kima cha chini cha mshahara (Dola 7.75), ili aweze kuvuka hili daraja itamlazimu afanye kazi masaa mawili!!!
Hivi ndivyo jinsi wengine ujipatia riziki yao ya kila siku...
Kila unaponunua kopo au chupa ya soda/bia unalipia senti tano zaidi katika bei ya ununuzi, na ukiamua kurudisha kopo/chupa tupu ina maana utarudishiwa hiyo senti tano yako, lakini ukiamua kuitupa na kuchafua mazingira basi ndipo hawa jamaa ujipatia riziki yao kwa kukusaidia kwa hiyo kazi.

Wednesday, February 24, 2010

Kuna msemo wa Kiingereza unasema " Picha inajieleza mara Elfu Moja".... Labda hawakukosea!!!!
Wakati kina mama wanapoamua kuji-express jamaa wanatamani ardhi ipasuke...

Tuesday, February 23, 2010

Ingawa huduma za hawa jamaa ni muhimu wakati usafiripo kwenye mabarabara yetu yakwenda mikoani, lakini mara nyingi huduma hizo uchanganyika na kero hasa pale inapotokea kwamba unavamiwa na manjinga kama kumi hivi na wote wanataka ununue biadhaa ya aina moja na kila mmoja anadai ununue kwake!

Sunday, February 21, 2010

Kuuliza si ujinga! Hivi ni nini hasa maana ya ukaguzi wa namna hii katika majeshi? Hata kwa kuangalia picha hii nimejaribu sana kutafakari madhumuni na malengo yake lakini bado nina utata...
EGYPT, SOUTH AFRICA IN SAME NATIONS CUP GROUP


Defending champions Egypt were drawn in the same 2012 Africa Cup of Nations qualifying group as 2010 World Cup hosts South Africa on Saturday.


Sierra Leone, who beat and drew with Bafana Bafana (The Boys) in the last Nations Cup elimination competition, and Niger complete Group 7, which promises to be among the toughest.


Egypt will be seeking a record fourth consecutive title when Gabon and Equatorial Guinea co-host during January 2012 the next version of the biennial African football showpiece.


The Pharaohs defeated Ivory Coast on penalties in the 2006 final, Cameroon 1-0 in Accra two years later and Ghana by the same score in Angola last month with 'super sub' Mohamed Gedo Nagy snatching the late winner.


Only group winners are guaranteed places at the tournament so South Africa have their work cut out as they attempt to reclaim a place among the African elite after failing to qualify for Angola.


Every draw delivers a so-called 'group of death' and the 2012 Nations Cup is no exception with four-time champions Cameroon facing Senegal and Democratic Republic of Congo plus lowly Mauritius.


While Cameroon have reached every tournament since 1996, Senegal and DR Congo missed out of the 2010 finals and will be champing at the bit to prove they are not spent forces.


Group 4 is going to be no less fascinating as World Cup qualifiers and 2010 Nations Cup semi-finalists Algeria share it with Morocco, Tanzania and the Central African Republic.


Togo were the only 2010 Nations Cup qualifiers not included in the draw after being disqualified because the organisers said illegal "government interference" led to their withdrawal after a fatal ambush in Angola.


A team official and assistant coach were killed in the attack as the team crossed from Congo to Cabinda and a reserve goalkeeper had to be airlifted to South Africa after sustaining serious injuries.


The Switzerland-based Court of Arbitration for Sport (CAS) will rule on a Togo appeal against the ban from the 2012 and 2014 Nations Cup and if successful the west Africans will be included in a revised draw.


There are three groups containing two 2010 Nations Cup qualifiers -- Zambia and Mozambique share Group 3, Ivory Coast and Benin are in Group 8 and Tunisia and Malawi are among the Group 11 quartet.


The Confederation of African Football released the draw in the southern DR Congo mining city of Lubumbashi, where the annual African Super Cup match will be staged on Sunday between local club TP Mazembe and Stade Malien of Mali.


Draw
Group 1: Mali, Cape Verde Islands, Zimbabwe, Liberia

Group 2: Nigeria, Guinea, Ethiopia, Madagascar

Group 3: Zambia, Mozambique, Libya, Comoros Islands

Group 4: Algeria, Morocco, Tanzania, Central African Republic

Group 5: Cameroon, Senegal, Democratic Republic of Congo, Mauritius

Group 6: Burkina Faso, Gambia, Namibia, Mauritania

Group 7: Egypt (holders), South Africa, Sierra Leone, Niger

Group 8: Ivory Coast, Benin, Rwanda, Burundi

Group 9: Ghana, Congo, Sudan, Swaziland

Group 10: Angola, Uganda, Kenya, Guinea Bissau

Group 11: Tunisia, Malawi, Chad, Botswana


Note: Group winners plus best three runners-up qualify for finals with co-hosts Gabon and Equatorial Guinea

Saturday, February 20, 2010

CRISPIN NA REZA WALIMEREMETA


Reza Karia Mziray(Mrs. Kinabo) kwa kweli alipendeza sana na ukiongezea tabasamu na d...

Bwana na bibi jinsi walivyopendezeana!!!
Crispin M. Kinabo, Reza, Harrieth na Simon Kinabo

Jamani madada... Reza K., Reza M., na Harrieth D. kwa kweli walimeremeta!!!

Mambo hayo!!!

Mama Matovu(shangazi) akimfurahia mwanae!

Baba mzaa chema(Godwin Karia Mziray) akiteta jambo na dada yake(mama Matovu).

Wazazi wakitambulishwa kwa madoido ya hali ya juu!

Sendoff haijakamilika bila ya mduara... mambo ya kivazi yalikuwa African style!!!
Panapofuka moshi! chini kuna moto
KILIMANJARO MUSIC AWARD ! Je!  itautambua mchango wa wanamziki

wa tanzania walio nje ya nchi au?Ni juzi tu Kili Award imetangaza lengo lake la kuwapa tuzo wanamziki na bendi za mziki
nchini. Lakini wimbi kubwa linaonekana kuvamia meza ya kamati ya Kili Award,kwani tayari malalamiko
kutoka kwa wadau na washabiki wa mziki nchini,wanadai kuwa katika uteuzi wa nani? apewe tuzo za Kili
kuna hewa ya ubaguzi,hewa hiyo ya ubaguzi inajipenyeza bila wanakamati kujua!!


Washabiki na wadau wamziki wanalalamika kwa nini? kamati ya Kili Award itambue mchango na kuwapa
tuzo hizo wanamziki wa nchi jirani kwa kigezo cha East African best artist,badala ya kuwapa wanamziki
wa tanzania walio nje ya nchi? ambao kazi zao na nyimbo zao zinafanya vizuri sana ndani na nje ya nchi,
isitoshe wanamziki wa tanzania na bendi zao walio nje ya nchi wamekuwa mambalozi wazuri wa kulitangaza
taifa katika njia ya mziki.


Wadau wanaendelea kulalamika kuwa hiwapo kamati ya Kili Award inaweza kuzitambua kazi za wanamziki
kutoka nchi jirani,kuna ugumu gani ? wa kuzitaambua kazi za wanamziki wa Tanzania walio nje ya nchi,
wakati mchango wao ni mkubwa kuliko wa wanamziki wa nchi jirani.


Moja katika ya watunzi na waimbaji wa kitanzania walio nje ni mwanamziki nyota Ebrahim Makunja aka
Kamanda Ras Ebby Makunja,anayeongoza bendi ya The Ngoma Africa aka FFU yenye makao ujerumani,
Ras makunja anajulikana kwa tungo za nyimbo zake ambazo mara nyingi zimekuwa zinagusia maswala ya
jamii yakiwemo "Rushwa",Ulevi,mateso ya watoto n.k pia nyimbo zake kama vile "Apache wacha Pombe",
"Rushwa ni hadui wa haki" "Wivu ni Kidonda" n.k ambazo zinafanya vema katika vituo vya redio vya ndani na  nje ya nchi pia zinapatikana www.myspace.com/thengomaafrica mchango wake ni mkubwa kwa jamii kuliko  wa wanamziki wa nchi jirani ambao kamati ya Kili Award itawapa tuzo.


Wanamziki wengine ambao wanafanya vema ni Ras Nas anaefanyia shughuli zake Norway,Fresh Jumbe Mkuu anayefanyia kazi zake Japan.


Wimbi la malalamiko ya wadau na washabiki kama hayatatiliwa maanani na kamati ya Kili Award,basi kamati itajikuta inawapa Award wanamziki mabao sio walengwa katika Kili Award,na matokeo yake ni kuwatosa watoto wa tanzania ambao wanaitangaza tanzania kimataifa katika njia ya mziki.Kamati ya Kili Award hisipo angalia kwa undani nini?nia na madhumuni ya Award hiyo itajikuta ikitoa award ya Kili kwa wanamziki wasio walengwa kwa kigezo cha "huruma" wakati inaheleweka wazi kuwa penye "haki" hakuna huruma.

Friday, February 19, 2010

Thursday, February 18, 2010

Wednesday, February 17, 2010

This is the other side of Tanzanian city living, sio ajabu kabisa baada ya miaka 48 ya kujipatia uhuru kukuta nyumba za udongo mijini mwetu.
Hii ni sababu mojawapo ambayo mzungu hatakaa kumsahau "NDULI" Idd Amin Dada!!!