Friday, February 26, 2010

 HAYATI BALOZI DAUDI MWAKAWAGO

Blogu hii ya jamii imepokea kwa masikitiko makubwa sana msiba wa mpendwa wetu Mzee Balozi Daudi Mwakawago.

Wengi tuliotokea kupata kumfahamu Balozi Mwakawago wakati wa uhai wake tuna kila jema la kumsifia.
 Balozi Mwakawago alikuwa ni mtu wa watu, muungwana ambae ana utu wa ubinadamu, hakupenda makuu na hakuwa na ubinafsi. Alilitumikia taifa lake katika kipindi chote cha maisha yake kwa heshima na moyo mkunjufu, ndani na nje ya Tanzania na kuliletea taifa letu heshima ya kipekee.

Wakati wa uwakilishi wake kwenye Umoja wa Mataifa hapa New York, tuliishi nae kiungwana sana, kwani yeye na familia yake walikuwa wakarimu sana kwa kila Mtanzania.

Pamoja na majukumu mazito ya kikazi, lakini Balozi Mwakawago na familia yake siku zote walikuwa karibu sana na Jumuia nzima ya Watanzania, iwe ni kwa raha au matatizo. Waliweza kutumia muda wao hafifu kutuliwaza, kutupongeza na kucheka nasi.

Ingawa tumempoteza Mzee wetu, lakini maisha yake ni fundisho kubwa kwetu na kumbukumbu zake tutabaki nazo daima.

Rambi rambi za dhati kwa familia nzima ya  Mzee Mwakawago  wakati huu mgumu wa kipindi cha maombolezi.
Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu!

-FUNDI RAMADHANI-

1 comment: