Monday, December 29, 2008Wengi walikuwepo katika kusheherekea miaka kumi ya kuzaliwa kwa mtoto Kombo, kama picha zinavyoonyesha hapo juu.
Sunday, December 28, 2008Hivi ndivyo ilivyokuwa jana wakati wa kusheherekea siku ya miaka kumi ya kuzaliwa mtoto Kombo Ramadhani. Hongera mtoto Kombo na Mwenyezi Mungu akujalie miaka mingine mingi.HAPPY 10TH BIRTHDAY KOMBO

Saturday, December 27, 2008

COMMON SENSEMy parents told me about Common Sense early in my life and told me I would do well to call on her when making decisions. It seems she was always around in my early years but less and less as time passed by. Today I read her obituary. Please join me in a moment of silence in remembrance, for Common Sense had served us all so well for so many generations.Obituary: Common Sense Today we mourn the passing of a beloved old friend, Common Sense, who has been with us for many years. No one knows for sure how old she was since her birth records were long ago lost in bureaucratic red tape. She will be remembered as having cultivated such valuable lessons as knowing; when to come in out of the rain,why the early bird gets the worm,life isn't always fair,and maybe it was my fault.Common Sense lived by simple,sound financial policies(don't spend more than you earn)and reliable parenting strategies(adults, not children are in charge). Her health began to deteriorate rapidly when well intentioned but overbearing regulations were set in place.Reports of a six-year-old boy charged with sexual harassment for kissing a classmate; teens suspended from school for using mouthwash after lunch; and a teacher fired for reprimanding an unruly student,only worsened her condition.Common Sense lost ground when parents attacked teachers for doing the job they themselves failed to do in disciplining their unruly children.It declined even further when schools were required to get parental consent to administer aspirin, sun lotion or a sticky plaster to a student,but could not inform the parents when a student became pregnant and wanted to have an abortion. Common Sense lost the will to live as the Ten Commandments became contraband; churches became businesses;and criminals received better treatment than their victims.Common Sense took a beating when you couldn't defend yourself from a burglar in your own homeand the burglar could sue you for assault.Common Sense finally gave up the will to live after a woman failed to realize that a steaming cup of coffee was hot. She spilled a little in her lap, and was awarded a huge settlement.Common Sense was preceded in death byher parents, Truth and Trust;her husband, Discretion;her daughter, Responsibility;and her son, Reason.She is survived by three stepbrothers;I Know my Rights,Someone Else is to Blame,and I'm a Victim. Not many attended her funeral because so few realized she was gone.If you still remember her, pass this on.If not, join the majority and do nothing.
Thank You!

Thursday, December 25, 2008

Sheikh-Yahya Hussein ni mtabiri mkubwa wa mambo mbali mbali na anajulikana sana Tanzania na Afrika Mashariki. Je! utabiri wake utakuwa vipi kwa mwaka 2009?

NINAPENDA KUWATAKIA
WADAU WOTE
PO POTE MLIPO DUNIANI
SIKUKUU NJEMA YA
KRISMAS
NA
HERI ZA MWAKA MPYA

Wednesday, December 24, 2008

Raisi mteule bwana Obama, yuko likizo fupi Honolulu, Hawaii akijiliwaza na hali nzuri ya hewa kabla ya kutawazwa rasmi Urais hapo Januari 20, 2009. Sehemu nyingine nyingi Marekani kwa sasa ni baridi na barafu la nguvu.

Jamaa wakiwa wamesheheni kwenye treni wakitokea kwenye sherehe ya kidini nchini Pakistani. Sidhani kama hawa jamaa wana sheria inayozuia usafiri mbaya kama huu uwezao kusababisha mahafa makubwa.

Saturday, December 20, 2008

Hayati Mbaraka Mwishehe alikuwa ni mwanamusiki mashuhuri sana Tanzania na Afrika Mashariki.

Wednesday, December 17, 2008


Ni tofauti sana na Marais wote waliopita...ANAELEWA!!

Mshambuliaji machachari enzi hizo "Zamoyoni Mogella" akifanya vitu vyake.

Sunday, December 14, 2008


Katika kipindi cha miaka ya nyuma(1970's na 1980's), Tanzania tulikuwa tunalisakata kandanda kiuhakika sana na wengi wa wachezaji wetu walicheza kwa viwango vya juu sana. Ni nini kimetokea baada ya hapo ni swali ambalo wengi bado tunajiuliza. Pichani ni baadhi ya hao mashujaa wetu enzi hizo.
Rais mteule Barack Hussein Obama na familia yake, wakiwa wameelekeza macho na masikikio kwenye luninga usiku wa tarehe 4 Novemba. Mamillioni ya watu duniani kote walikuwa kama kina Obama katika siku hiyo ya kihistoria. Zimebakia siku chache kwa jamaa na familia yake kuingia Jumba Jeupe na matumaini ya walio wengi ni kumuona bwana Obama akiliongoza Taifa hili kurudia kwenye neema na maendeleo kwa watu wake pamoja na kulirudishia heshima duniani.
Kwa maoni ya walio wengi, Rais anayemaliza muda wake(bwana Kichaka), ametuyumbisha sana kwa kutuingiza kwenye mengi ya matatizo tunayokumbana nayo kwa sasa. Historia pekee ndiyo itakayo muhukumu bwana Kichaka kwa damu nyingi aliyoimwaga Iraq na mengi mengineyo.


Friday, December 12, 2008

Tungekuwa na mpangilio mzuri, nadhani vijiji vyetu vingependeza sana. Tizama kwa mbali jamaa walivyopomorosha ghorofa.
Wadau, someni hiki kitabu!!

Wednesday, December 10, 2008

Mdau Tonny Mwingira alipokutana na Mama Migiro kwenye kiwanja cha ndege pale Ulaya alipokwenda kikazi.


Tanzania tunayo haki ya kujivunia kwa kuwa na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye Umoja wa Mataifa, Mama Asha Rose Migiro(Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa) ni ishara sahihi ya kuheshimika kwetu katika jamii ya Kimataifa, na hii inatokana na amani na umoja na msimamo wetu katika masuala mbali mbali Duniani. Tanzania imetimiza umri wa miaka 47 tokea tupate uhuru na mwelekeo wetu katika kuendeleza umoja na amani bado uko katika hali nzuri. Pongezi kwa viongozi wetu na Watanzania wote kwa ujumla.

Monday, December 8, 2008


EID MUBARAK

KWA WOTE
NA
NAWAOMBEA MAISHA MEMA NA MAREFU

INSHALLAH!!

Sunday, December 7, 2008

Mapesa yote hayo kwa mkate mmoja tu!! Mugabe ONDOKA.

Hivi hawa kweli watafika? Nasikia eti kuna nyingine ya millioni mia mbili inatolewa....


Hivi ndivyo ilivyo nchini Zimbabwe kwa sasa. Hali inazidi kuwa ngumu lakini bwana Mugabe hasikii wala haoni. Hivi kama kweli mwendo ni kwa mkokoteni, hawa wagonjwa wa kipindupindu watapona kweli? Mugabe sasa inatosha...ONDOKA!!

Thursday, December 4, 2008

MAO PRODUCTIONS

An African Party Mix
Spinning the best from Afrika
Sat Dec 6th, 2008
@ THE CALABASH
12 E First St.
MT. Vernon, NY 10550
ADMISSION
$5.00 b4 midnite & $10.00 after

DIRECTIONS AND INFO(917)709-6889

Wednesday, December 3, 2008

Mwalimu Nyerere akiwa na Bibi Titi Mohamed ( mwasiasa mwanamke wa mwanzo ), kwenye mkutano wa TANU katika viwanja vya Jangwani. Hii inaonyesha jinsi gani kina mama wetu tayari walikuwa mstari wa mbele kisiasa, na kama sikukosea kwa nchi kama Marekani kina mama walikuwa bado si ruksa kupiga kura achilia mbali kuwa viongozi.

Tuesday, December 2, 2008

Baada ya wiki moja ya kupajua rumande kukoje hatimaye Yona na Mramba wakubaliwa dhamana ya karibu shilingi billioni 2.9 kila mmoja. Yanayotokea nchini mwetu yanatuonyesha kwamba huu ni mwanzo na mengi yanafuata. Siku itafika kwa sheria na haki kuwa ni mambo ya kawaida Tanzania. Ole wenu kwa mliodhani kwamba sheria za nchi hazitawagusa.Wanangu Kombo na Hennah wakifurahia maji wakati wa kipindi cha joto kali. Kipindi cha baridi kimeshaanza hivyo kwa sasa ni makoti mazito na kukaa ndani mpaka mwakani.