Showing posts with label Nyerere. Show all posts
Showing posts with label Nyerere. Show all posts

Wednesday, December 3, 2008

Mwalimu Nyerere akiwa na Bibi Titi Mohamed ( mwasiasa mwanamke wa mwanzo ), kwenye mkutano wa TANU katika viwanja vya Jangwani. Hii inaonyesha jinsi gani kina mama wetu tayari walikuwa mstari wa mbele kisiasa, na kama sikukosea kwa nchi kama Marekani kina mama walikuwa bado si ruksa kupiga kura achilia mbali kuwa viongozi.

Tuesday, October 14, 2008


Pamoja na tofauti zetu lakini "Sisi bado ni wamoja". Tuendelee kutafuta jinsi ya kuuimarisha na kuulinda UMOJA wetu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Tuanamkumbuka Baba wa Taifa, mojawapo ikiwa ni jitihada zake kuliweka Taifa mbele katika kutetea haki za wengi kama alivyofanya kwenye matembezi ya kuunga mkono "Azimio la Arusha".

Tuesday, October 7, 2008

Siku zote hatuna budi kumuenzi Baba wa Taifa kwa kutujengea umoja, ambao ni moja ya sifa kubwa tuliyonayo Watanzania. Alikuwa mstari wa mbele kuikomboa Afrika kutoka kwa wakoloni na vibaraka wao.
Ni mmoja wa viongozi Duniani ambaye siku zote aliiweka nchi na watu wake mbele na ubinafsi nyuma. Alikuwa na uchungu na nchi na huruma wa wanyonge kote Duniani.
Mungu ibariki roho ya hayati Baba, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na tutakukumbuka daima na milele.

Tuesday, September 9, 2008



Mwalimu Nyerere akiwa na familia yake Ikulu Dar es Salaam.

Alijulikana na kuheshimika na viongozi maarufu duniani kote. Hapa akiwa na JFK Ikulu ya Marekani.















Hakuwa mpenda makuu. Mwalimu alikuwa mpenzi sana wa kucheza bao. Hapa yuko na Mama Maria, Mzee Mwinyi na wazee wengine.
Baba wa Taifa