Tuesday, October 7, 2008

Siku zote hatuna budi kumuenzi Baba wa Taifa kwa kutujengea umoja, ambao ni moja ya sifa kubwa tuliyonayo Watanzania. Alikuwa mstari wa mbele kuikomboa Afrika kutoka kwa wakoloni na vibaraka wao.
Ni mmoja wa viongozi Duniani ambaye siku zote aliiweka nchi na watu wake mbele na ubinafsi nyuma. Alikuwa na uchungu na nchi na huruma wa wanyonge kote Duniani.
Mungu ibariki roho ya hayati Baba, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na tutakukumbuka daima na milele.

No comments:

Post a Comment