Thursday, May 31, 2012

DADA JOY ANDY NA CLASS OF 2012 GRADUATION


Dada Joy Andy Akiwa na Smile Lenye Ujazo Baada Ya Graduation Yake Na Kupata Nondo Zenye Ujazo Wenye Wiwango, Dada Joy Amegraduate Katika City University of New York Queens College. na Kupata Bachelor Of Business Administration In International Business, And Bachelor Of Arts In Economics. Hongera sana na Tunakutakia Mafanikio Mema Mbeleni.
Hapa Dada Joy Akiwa na Marafiki Wakipata Picha Ya Kumbukumbu


Wednesday, May 30, 2012

HOSPITALI YA TUMBI YAANZA KUPOKEA MSAADA WA MASHUKA

 Afisa Uhusiano wa Maxinsure akionyesha mashuka alioyakabithi katika hosptali ya Tumbi hivi karibuni.


 Meneja Madai wa Kampuni ya Maxinsure ,Bw. Ian Kifunta akishikilia mashuka ya msaada wakati walipokua wanatembelea hospitali ya Tumbi hivi karibuni.
PICHANI: Afisa Uhusiano wa Maxinsure akiongea na waandishi wa habari walipoenda kukabidhi misaada katika hospitali ya Tumbi, kushoto kwake ni Mganga mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Issac Lwari.


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk Issach Lwari akiwaonyesha wafanyakazi wa Maxinsure mashine mbovu,iliyokua ikinyooshea nguo za hospitalini hapo.

Hospitali ya Tumbi ya mjini kibaha yapokea msaada wa mashuka 50 yenye thamani ya shillingi za kitanzania 500,000 kutoka katika kampuni ya Bima ya Maxinsure hivi karibuni, Msaada huo ukiwa umetokana na na taaarifa iliyotoka katika gazeti maarufu moja nchini,likiwa linaelezea kuhusu upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.
Kampuni ya Maxinsure ndio imekua kampuni ya kwanza kabisa nchini kuitikia wito huo, huku Bima kuu ya Afya ya nchini ikihahidi kutoa mashuka pia hivi karibuni.
“Tunashukuru sana kampuni ya Maxinsure kwa kuguswa na tatizo letu,tunategemea kupata mashuka zaidi na tunaomba makampuni mengine yaweze kujitokeza kutusaidia, kwani hili sio tatizo pekee linaloikabili hospitali yetu”.Alisema Mganga mkuu wa hospitali ya Tumbi,Dk.Issach Lwari akishukuru kwa msaada alioupokea
Kwasasa Hospitali ya Tumbi ina mashuka yapatayo 900 huku ikiwa bado na uhitaji wa mashuka yasiopungua 1,124.
DK. Lwari alitaja matatizo mengine kama ,mashine za kufulia, upungufu wa damu na pia hospitali iyo inakabiliwa na ukosefu wa Vipimo mbalimbali ,swala linalopelekea kuwashauri wagonjwa wachukue vipimo katika hospitali nyingine.

Tuesday, May 29, 2012

MZEE IDD SIMBA ASOMEWA MASHTAKA NANE KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, Idd Simba akiongozwa na askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka nane likiwemo la kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara Shirika Usafiri Dar es Salaam (UDA) ya Sh. bilioni 2.3. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu. (Picha zote na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog).

Wakili Said Hamad El-Maamry (kushoto) akizungumza na Idd Simba Mahakamani hapo.

Mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salim Mwaking'nda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.

Monday, May 28, 2012

PICHA YA MLIPUKO WA BOMU NAIROBI LEO.

 Jengo la pili kutoka kulia ndio lililolipuliwa, Kwa mujibu wa Nation.co.ke ni watu 30 waliojeruhiwa, polisi walikanusha kwamba sio bumu ni shoti ya umeme la shirika la umeme Kenya limekanusha kwa kusema sio shoti manake hakuna transfoma kwenye eneo la tukio ila ingekuepo ndio kungekua na uwezekano wa shoti.


Mlipuko huo ulifanya baadhi ya majengo mengine ya karibu kutingishika ambapo ulitokea kwenye saa saba na dakika kumi leo mchana, mpaka sasa haiko wazi ni wangapi wamejeruhiwa au kupoteza maisha.
Inaaminika kwamba ni idadi kubwa ya watu waliopelekwa hospitali kutokana na kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu Nairobi Kenya leo Moi Avenue street, ulipuaji huo wa bomu unaaminika kufanywa na kikundi cha wanamgambo wa Al Shabaab Somalia.

Sunday, May 27, 2012

ZANZIBAR KWACHAFUKA

ZANZIBAR KWACHAFUKA

Mmoja wa waandamanaji wa Kundi la Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara  ya  Kiislamu (JUMIKI) Kisiwani Unguja, Zanzibar akionyesha kitambaa kilicho na damu mapema leo asubuhi wakati wakiendelea na maandamano yao ambayo yamesababisha vurugu kubwa kisiwani humo, hali iliyosababisha kuchomwa moto kwa moja ya makanisa pamoja na baadhi ya magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na njia wapitazo.
  Waandamanaji wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam (JUMIKI) wakiendelea na maandamano yao mapema leo asubuhi.
Askari wa Jeshi la Polisi kikosi cha kuzuia Ghasia wakifanya doria katika mitaa mbalimbali ya Zanzibar mapema leo asubuhi. (Picha kwa hisani ya Blog ya Issa Michuzi)

Friday, May 25, 2012

RAIS KIKWETE APOKEA UJUMBE MAALUM KUTOKA KWA RAIS ROBERT MUGABE WA ZIMBABWE

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe uliowasilishwa na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Bwana, Sidney Sekeremayi, Ikulu ndogo mjini Dodoma leo asubuhi.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Bwana Sidney Sekeremayi, ambaye ni mjumbe maalumu wa Rais Robert Mugabe Ikulu mjini Dodoma leo asubuhi. Picha na Freddy Maro.

THE UN SECRETARY-GENERAL MESSAGE ON AFRICA DAY

United-Nations-Secretary-General-Ban-ki-Moon


UNITED NATIONS INFORMATION CENTRE – DAR ES SALAAM
 May 25, 2012                                                            UNIC 
2012/03/15

 PRESS STATEMENT

Each year, Africa Day provides an opportunity to acknowledge the achievements of the peoples and governments of Africa and to reaffirm the support of the United Nations for their efforts to build a better future. 

The United Nations commends Africa’s recent efforts to consolidate its peace and security architecture, and to reject unconstitutional changes of power.  

We will continue to work with Africa in building durable peace, ending armed conflicts, boosting democracy, and promoting respect for fundamental human rights, especially the rights of women and youth.

Africa is a dynamic continent undergoing fundamental transformation.  Even during the world economic crisis, Africa’s economies continued to expand, and growth forecasts remain positive.  

However, the benefits are not reaching all Africans.  Poverty, hunger, and disparities in health, education, and participation in society, are preventing hundreds of millions of Africans from fully realizing their potential.  

Greater effort is needed by all to achieve the Millennium Development Goals by 2015.

 The growing number of success stories across Africa indicates that broader social and economic progress is realistically attainable for most Africans.  I have personally seen the dividends of investing in women’s and children’s health and sustainable agriculture. 

 I have spent many hours with African leaders who are committed to peace, human rights, democracy and good governance.

The challenge is to extend these advances and ensure they reach all Africans, especially the continent’s poorest and most vulnerable people.  In particular, we must address the spectre of hunger – from the highly visible periodic food emergencies to the hidden disgrace of stunting that is affecting a new generation of African children.  

 Many of these issues are on the table at the UN Conference on Sustainable Development next month in Brazil. 

 Rio+20 is a once-in-a-generation opportunity to mould the future we want – a future where climate change and desertification are no longer threats; where devastating maternal and child mortality, and diseases such as TB and HIV/AIDS, are consigned to the past; where all people have access to safe drinking water and adequate sanitation. 

 From renewable energy to thriving oceans, from empowered women to productive partnerships between governments, civil society and business, Rio+20 is our chance to deliver for all, particularly Africa.  

On this observance of Africa Day, as the world tries to forge a renewed global partnership for sustainable development, I pledge to work with Africa’s leaders and people to implement an agenda that addresses Africa’s needs – an agenda that will set the continent on the path to the future we all want: dynamic, equitable and sustainable growth that benefits all Africans.

POLISI YAPIGA STOP MAANDAMANO YA CHADEMA

<><> <><>
JESHI la Polisi limepiga marufuku matembezi ya amani (maandamano) ambayo yameombwa kufanywa kesho na Chama Cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema).
Huku, jeshi hilo likibariki Mkutano wa chama hicho kufanyika kwenye viwanja vya Jangwani.
Polisi limefikia hatua hiyo, baada ya kubaini kuwa hakuna sheria yoyote inayoruhusu chama cha siasa kufanya matembezi au maandamano isipokuwa mkutano.
Mei 26 Chadema, kilituma maombi ya maandishi (barua) kwa jeshi hilo kuruhusu matembezi hayo ya amani, kutoka sehemu mbalimbali za jiji hadi viwanja vya Jangwani panapofanyika mkutano wa hadhara leo.
Lakini jana Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Afande Suleiman Kova alisema, “Hakuna sheria yoyote ya Uchaguzi inayoeleza chama cha siasa  kufanya matembezi, hivyo hatukubaliani na ombi lao lakini hili la mkutano ruksa kufanya hivyo”
Kwa mujibu wa Kamanda Kova, Chadema iliwasilisha barua ya kuomba kibali cha kufanya mkutano, lakini kabla ya kujibiwa Mei 26 kiliwasilisha barua nyingine ili kupata kibali cha matembezi ya amani.
“Walisema wanachama wao hawana nauli, kutoka kwenye maeneo ya jiji kwenda viwanja vya Jangwani, lakini mbona jana walifika Mahakama Kuu kwa magari na mabasi, kwa hili hatuwezi kukubali”alifafanua.
Pia, polisi limesema mwanachama yoyote ambaye atapuuza amri hiyo, jeshi litamchukulia hatua za kisheria ikiwemo kukamatwa.
Kamanda aliwaonywa Wanachama kutodanganyika na wakuu wao wa chama kwa kufanya matembezi hayo, kwani jeshi linamchukulia hatua  za kisheria Mwananchi sio chama cha siasa.
Kwa mujibu wa Kamanda huyo, jeshi la polisi halipendi kuona amri zake zikipindishwa, au kugombana na vyama vya siasa.
Alienda mbali zaidi akisema, mji wa Dar es Salaam, unatakiwa kuwa na amani wakati wote, hivyo amri hiyo wana hakika itatekelezwa.
Kwa upande mwingine Kova, alionya juu ya Mkutano huo wa leo, akisema uwe wa amani na utulivu.
Alisema polisi wako tayari kutoa ulinzi wakati wote wa mkutano huo ili kuhakikisha kunakuwa na amani.

WABUNGE WA UKRAINE WAZICHAPA KAVU KAVU MJENGONI

 Wabunge wa nchini Ukraine wakizichapa kavukavu wakati wakiwa katika moja ya Kikao cha Bunge nchini humo baada ya kupishana msimamo kuhusu matumizi ya Lugha ya Kirusi wakitaka itumike katika Mahakama za nchi hiyo.  Wabunge wa chama cha Rais Viktor Yanukovich, wanataka lugha ya Kirusi ikubaliwe kama lugha rasmi ya pili nchini humo jambo ambalo wabunge wa vyama vya upinzani wanapinga vikali kupitishwa kwa sheria hiyo ambayo ingeruhusu lugha ya Kirusi kutumiwa katika mahakama.
Wabunge hao wakiendelea na sinema yao ya kuonyeshana umwamba ndani ya ukumbi huo wa Bunge.

Thursday, May 24, 2012

ONLY IN NEW YORK CITY WE HAVE A REALLY NAKED COW BOY

Naked Cow Boy In The City..

MTANZANIA DR ENGINEER SHABAN KACHUA ATUNUKIWA RASMI SHAHADA YAKE YA UDAKTARI WA FALSAFA NCHINI CANADA.

Dr Engineer Shaban Kachua mwenye joho lenye rangi nyekundu na Bluu akiwa na waafrika wenzake wakati wa alipotunukiwa Shahada yake ya Udaktari wa falsafa Nchini Canada.
Hapa Dr Kachua akiwa amekaa mstari wa mbele kabisa na wahitimu wenzake.
Mama Mzazi wa Dr Kachua (mwenye blauzi nyeusi), akiwa na Mama mkwe wake, wote kwa pamoja walishiriki katika tukio la kihistoria la kutunukiwa Shahada ya PHD kwa mtoto wao nchini Canada.
Mrs Dr Shaban Kachua (Jemima) akiwa na furaha pamoja na watoto wao walishiriki katika shughuli ya kutunukiwa Mume wake shahada ya udaktari wa Falsafa (PHD).

Kwa sasa Dr Shaban Kachua anaishi Nchini Canada pamoja na familia yake. Sisi kama watanzania wenzake tunapenda kumpongeza sana kwa kuweza kuipeperusha vema Bendera yetu, tunapenda kumshauri pia, elimu yake hiyo aweze kuitumia pia kulisaidia Taifa lake la Tanzania hasa katika nyanja hiyo ya Sayansi, kwa kutambua zaidi tuna upungufu mkubwa wa wanasayansi katika Taifa letu.
 
HONGERA SANA

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA -MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA TCRA

Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano.Sayansi na Teknolojia, January Makamba, akipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)  Profesa John Nkoma, wakati alipotembelea Makao Makuu ya ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania zilizopo Jengo la Mawasiliano Taower Sinza  ,barabara ya Sam Najoma jijini Dar es Salaam ili kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
 Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia Januari Makamba akimsikiliza Mhandisi Mfawidhi wa Mawasiliano ya Redio wa  Mamlaka ya Mawasilioano Tanzania. Mhandisi,.Johannes Magesa, wakati alipokuwa akitoa maeleza juu ya kutambua muingiliano wa mawasilia kwa frequecy za redio wakati waziri huyo alipotembelea TCRA kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo . kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Profesa John Nkoma

John Mnyika wa CHADEMA aibuka Kidedea Mahakama Kuu Dar es Salaam

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika uchaguzi wa mwaka 2010, hukumu iliyotolewa leo na Mahakama Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam. Pichani wafuasi wa Chadema wakiwa wamembeba juu kwa juu mara baada ya kutangazwa mshindi.

Wednesday, May 23, 2012

SKOLA NDIKWIKI BIRTHDAY AND FUNDRAISING.

Skora Ndikwiki Birthday And Fundraising For Kasulu Community Org(Kigoma-Tanzania)Orphan Children Centre, June 25th, 2021,  Address 27 John St Tamagua, Pa 18252, USA

WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA SHULE YA MSINGI MAKUMBUSHO KAMA WANAVYOONEKANA DARASANI LEO HII .


HAWA NI BAADHI YA WANAFUNZI WA DARASA LA KWANZA  KATIKA SHULE YA MSINGI MAKUMBUSHO YA JIJINI  DAR ES SALAAM WAKIWA DARASANI, SIJUI WAPO WANGAPI, WATOTO HAWA HULAZIMIKA KILA MWEZI KULIPA Tsh1000 YA MTIHANI WA MWEZI,Tsh 1500 YA MTIHANI WA TERM,Tsh500 YA KILA SIKU YA UJI HAPO BADO TIUSHENI,USAFI, MLINZI,LEBO,VIDUMU,FAGIO, NA MADAFTARI PIA HULAZIMISHWA KUNUNUA HAPOHAPO.

Tuesday, May 22, 2012

MWANAMKE WA UJIJI KILA KITU KATIKA ZIWA.

Kuosha vyombo, kufua na mengineyo.
Pichani ni Ujiji, leo mchana.

NENO FUPI LA USIKU HUU NA JOHN CHIBUDA

Ndugu zangu,

Mtanzania mwenzetu John Shibuda ameibua hoja ya ukabila. Nakubaliana na John Shibuda kwenye hoja ya kutaka haki yake ya kutangaza nia ya kuwania Urais wa nchi hii iheshimiwe. 

Shibuda ana haki hiyo. Na haitakuwa mara ya kwanza kwake kututangazia Watanzania nia yake hiyo.
Lakini, inasikitisha, kuwa hoja ya pili ya John Shibuda imechangia kuua hoja yake ya kwanza; ni hoja ya ukabila. 

Shibuda anaonekana kututaka Watanzania tujadili ukabila na hususan chama chake cha Chadema na ukabila ulio ndani ya chama hicho.

John Shibuda ni mmoja wa viongozi ninaowaheshimu sana kwa mchango wao kwa taifa letu. Naamini, kuwa John Shibuda anaheshimika na wengi wengine hapa nchini. Lakini, kwa kutuletea hoja ya Chadema na ukabila,  nahofia John Shibuda amepotea.  

Hoja yake haina msingi. Imejengeka katika hisia kuliko uhalisia. Yumkini, John Shibuda amekuja na hoja hii sasa, ama , kwa bahati mbaya, au kukusudia. Hilo la mwisho halina kusudi la kujenga, bali kubomoa. Inasikitisha.

Maana, hoja ya ukabila haina umaarufu katika nchi yetu kwa sasa. Watanzania wa sasa hatuendekezi ukabila. Kauli ya Shibuda kuwa anabaguliwa katika chama chake cha Chadema  kwa vile ni Msukuma haikupaswa kutamkwa kwa mtu kama Shibuda.  Na haikupaswa kutamkwa na yeye na bado akaendelea kubaki katika chama anachoamini kina ubaguzi wa kikabila na huku yeye mwenyewe akiwa muathirika wa ubaguzi huo.

Na kwa vile hana ushahidi wowote wa kuthibitisha anachosema, Shibuda anachochea moto ambao Watanzania hatuutaki. Ukabila ni moto wa hatari, kama ilivyo kwa moto wa udini.

Kama Shibuda analalamika kuwa anabaguliwa kwa vile ni Msukuma, ingekuwaje basi, John Shibuda angeitwa Ramadhan Shibuda? Je, angeongeza dai la pili; kuwa anabaguliwa Chadema kwa vile ni Muislamu. Si Mkatoliki?

Kama John Shibuda anadhani kauli zake za ukabila zinakisaidia Chama chake cha zamani cha CCM, basi, napo anakosea; maana, kwa CCM kuhusishwa sasa na kauli za Shibuda za ukabila, kunakiharibia zaidi CCM kuliko kukijenga kwa Watanzania walio wengi.  Lililo bora kwa CCM sasa ni kujitenga na kauli za Shibuda juu ya ukabila . Maana, Watanzania wa leo si wa jana.  Ni wepesi sasa wa kubaini hila na ghilba za wanasiasa. Wengi wanaonekana kusikitishwa na hoja ya John Shibuda juu ya kubaguliwa kwa vile ni Msukuma.  Wanasikitika kwa vile wanadhani hoja imejengeka katika hila na ghilba kwa wananchi.

John Shibuda afahamu ukweli huu;  Watanzania walio wengi  kwa sasa wanataka mabadiliko. Wanaiona sasa mishale ya saa ya mabadiliko ikisonga mbele. Wanamwona hata Rais wao, Jakaya Kikwete akisaidia kusukuma mabadiliko hayo.Ni mabadiliko ya kimfumo. Ni wangapi walifahamu kuhusu uwepo wa CAG miaka mitatu iliyopita?  Upinzani bungeni, ndani ya chama tawala, na uwepo wa ofisi ya CAG iliyopewa nguvu umeanza kurudisha matumaini ya Watanzania.

Naam, Watanzania hawataki tena kurudi katika mfumo wa Chama kimoja  kilichoshika hatamu. Majaribio yote ya kuua upinzani, kufuta fikra huru, yatazidi kulaaniwa na walio wengi katika nchi hii.

Hivyo, John Shibuda hawezi tena leo kurudisha nyuma mshale wa saa ya mabadiliko; hata kwa ajenda ya ukabila. Na hili ni Neno Fupi la Usiku Huu.

Maggid Mjengwa,
Kigoma.
0788 111 765KICHWANI AMEBEBA UTAJIRI LAKINI HAUMSAHIDII CHOCHOTE ZAIDI YA KUGANGA NJAA

Anazurura nao mitaani. Samaki hawana soko la uhakika. Pichani ni Kigoma Mjini, jana jioni.

MREMBO WA WIKI HII, LATIFA MAHUNDI WA BROOKLYN NY.

Pita pita za kamera ya fundi wa kombo mjini.

FLAVIANA MATATA AZULU KABURI LA MAMA YAKE MZAZI KUKUMBUKA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA

Mwanamitindo, Flaviana Matata (wa pili kulia) akiomba dua katika kaburi la mama yake Mzazi maeneo ya Igoma mkoani Mwanza katika siku ya kukumbuka ajali ya MV Bukoba iliyoua watu takribani 1000  Mei 21, 1996.  Flaviana mbali na kukumbuka waliofariki katika ajali hiyo akiwamo mama yake mzazi pia alikabidhi msaada wa vifaa vya kuokolea maisha  kwa Shirika la Kiserikali la Usafiri wa Maji Mwanza.
 Mwanamitindo wa kimataifa wa mitindo Tanzania, Flaviana Matata akikabdhi moja ya kifaa cha kuokolea maisha katika vyombo vya  usafiri wa majini katika Ziwa Victoria kwa Elias Makori aliyemwakilisha  Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  jana. Flaviana alikabidhi vifaa hivyo kwa Shirika la Kiserikali la Usafiri wa Maji Mwanza (Mwanza MerineCompany Limited)  ikiwa moja ya kuadhimisha siku ya hudhuni ya ajali ya meli ya MV Bukoba iliyotokea Mei 21 mwaka 1996 na kuuwa watu zaidi ya 1000 akiwemo mama yake mzazi.

Monday, May 21, 2012

BIRTHDAY GIRL DINER HAMISA MAHUNDI WA BROOKLYN NY.


Hamisa Juu Na Latifa  An Chini Ni Hamisa na Baia.

 Hamisa Na Latifa
 Cake ya birthday
 Hamisa Akizima Mishumaa


Picha ya Pamoja Kabla ya kuanza Dina...

Sunday, May 20, 2012

BERNADETTE SERUHERE HAPONGEZWA KWA KUCHANA VIZURI MTIHANI WA KUINGIA CHEKECHEA HONGERA SANA.

Hapa Akiwana best friend wake Maziko alie kuja kumopa shavu rafiki yake.

Zawadi ni zawadi wewe pokea best Maziko akimpatia zawadi ya game.

Amani Hiwe kwako Baba Hapo ndo Bernadette ndo anavyo mwambia baba yake peace kwa kunileta uku dunia.

Licha ya kuwa Genius kimasoma pia anaiza kuimba uncle ni noma hongera na kila la kheli maishani

GEOFFREY LWEGALABAMU HALA NDONDO ZAKE MANHATTANVILLE COLLEGE WHITE PLANS NY

Akiachia Smile La Afya Kwa Faraha Ya Kuitimu Chuoni Hapo. Mahafari yaliyo Fanyika Wknd Hii.

Hapa akikabiziwa Mkoba wake safiiiii!!!

Bwana Geoffrey Kiwa na Mama Zake Mama Mkubwa Na Mdogo Kupa Shavu Mtoto Wao.


Kama Kawa Mwana Glob Ny Ebra Alikuwepo Pia.....