PICHANI: Afisa
Uhusiano wa Maxinsure akiongea na waandishi wa habari walipoenda
kukabidhi misaada katika hospitali ya Tumbi, kushoto kwake ni Mganga
mkuu wa Hospitali ya Tumbi Dk. Issac Lwari.
|
Mganga Mkuu wa Hospitali ya
Tumbi Dk Issach Lwari akiwaonyesha wafanyakazi wa Maxinsure mashine
mbovu,iliyokua ikinyooshea nguo za hospitalini hapo.
Hospitali
ya Tumbi ya mjini kibaha yapokea msaada wa mashuka 50 yenye thamani ya
shillingi za kitanzania 500,000 kutoka katika kampuni ya Bima ya
Maxinsure hivi karibuni, Msaada huo ukiwa umetokana na na taaarifa
iliyotoka katika gazeti maarufu moja nchini,likiwa linaelezea kuhusu
upungufu wa mashuka katika hospitali hiyo.
Kampuni ya Maxinsure ndio
imekua kampuni ya kwanza kabisa nchini kuitikia wito huo, huku Bima kuu
ya Afya ya nchini ikihahidi kutoa mashuka pia hivi karibuni.
“Tunashukuru sana kampuni ya Maxinsure kwa kuguswa
na tatizo letu,tunategemea kupata mashuka zaidi na tunaomba makampuni
mengine yaweze kujitokeza kutusaidia, kwani hili sio tatizo pekee
linaloikabili hospitali yetu”.Alisema Mganga mkuu wa hospitali ya
Tumbi,Dk.Issach Lwari akishukuru kwa msaada alioupokea
Kwasasa Hospitali ya Tumbi
ina mashuka yapatayo 900 huku ikiwa bado na uhitaji wa mashuka
yasiopungua 1,124.
DK. Lwari alitaja matatizo mengine kama ,mashine
za kufulia, upungufu wa damu na pia hospitali iyo inakabiliwa na
ukosefu wa Vipimo mbalimbali ,swala linalopelekea kuwashauri wagonjwa
wachukue vipimo katika hospitali nyingine.
No comments:
Post a Comment