Tuesday, May 29, 2012

MZEE IDD SIMBA ASOMEWA MASHTAKA NANE KATIKA MAHAKAMA YA KISUTU LEO

Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara wa zamani, Idd Simba akiongozwa na askari Polisi wakati alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka nane likiwemo la kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu pamoja na kulisababishia hasara Shirika Usafiri Dar es Salaam (UDA) ya Sh. bilioni 2.3. Mshtakiwa huyo alifikishwa mahakamani hapo pamoja na washtakiwa wengeni watatu. (Picha zote na Mpiga Picha wa Habari Mseto Blog).

Wakili Said Hamad El-Maamry (kushoto) akizungumza na Idd Simba Mahakamani hapo.

Mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo, Aliyekuwa Diwani wa Sinza, Salim Mwaking'nda akiwa katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mchana.

No comments:

Post a Comment