Jengo la pili kutoka kulia ndio lililolipuliwa, Kwa mujibu wa
Nation.co.ke ni watu 30 waliojeruhiwa, polisi walikanusha kwamba sio
bumu ni shoti ya umeme la shirika la umeme Kenya limekanusha kwa kusema
sio shoti manake hakuna transfoma kwenye eneo la tukio ila ingekuepo
ndio kungekua na uwezekano wa shoti.
Inaaminika kwamba ni idadi kubwa ya watu waliopelekwa hospitali kutokana
na kujeruhiwa kwenye mlipuko wa bomu Nairobi Kenya leo Moi Avenue
street, ulipuaji huo wa bomu unaaminika kufanywa na kikundi cha
wanamgambo wa Al Shabaab Somalia.
Mlipuko huo ulifanya baadhi ya majengo mengine ya karibu kutingishika ambapo ulitokea kwenye saa saba na dakika kumi leo mchana, mpaka sasa haiko wazi ni wangapi wamejeruhiwa au kupoteza maisha. |
No comments:
Post a Comment